Lipumba NI CCM ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba NI CCM ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bontowar, May 19, 2009.

 1. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Nasikia Lipumba naye ni miongoni mwa watu wa CCM anawayeyusha CUF

  Za ndani zaidi na zitakak
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hiyo inawezekana. Niliwahi kuuliza kama kuna mtu anaweza kututhibitishia tetesi nilizokuwa nimepata kwamba jamaa ni kijana wa Usalama wa Taifa kama akina Mrema nikakosa jibu. Kwa hiyo siwezi kuthibitisha unayosema ila mwenendo wa mambo yake unaweza kutupatia hints kama kweli ni CCM au la!! Binafsi sitashangaa kwa sababu kazi CCM na kitu kilichoisaidia kuendelea kuwatesa Watanzania ni kuweka viongozi mamluki kwenye upinzani.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ina maana usalama wa taifa ni CCM damu? no wonder wamejazana serikalini ktk nafasi nyeti za kiutawala.

  Ila kuhusu Lipumba naweza kusema kwamba yeye ni CUF ila kakosa mwelekeo na dira kutokana na ulevi wa madaraka
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Pindi wapinzani wanapokosa muelekeo na kupoteza kabisa matumaini ya watanganyika kukombolewa kutoka katika mikono onevu ya CCM husingizia CCM. Jamani tusiwape kichwa hawa wapinzani tuliwapa dhamana mwaka 1992 ya kutukomboa wana deni kwa watanzania wasifikiri hizo ruzuku tunazowapatia hazituumi, ni kodi zetu na madeni tunayowaachia watoto wetu. Kila kukicha wanakuja na visingizio tu kwani CCM ni nini? Watanzania tuzinduke hawa wanakula ruzuku linapokuja suala mabadiliko wanajitoa eti CCM imepandikiza watu shenzi type kwani mnapo wachagua kwa asilimia 99.9(hadi prof safari anasusa) huwa hamjui. Tena siku hizi nawaona hawa wapinzani ndio mafisadi wakubwa kuliko hata hao CCM, nakuanzia mwaka huu tunataka mahesabu yao yakaguliwe na taarifa ziwekwe wazi..WIZI WAKUBWA WA FEDHA ZA MASIKINI.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyo Profesa wa uchumi amethibitisja usemi wa "If you cant beat them, join them" -- yani 'kama huwezi kuwashinda basi jiunge nao.' Kaishiwa mbinu kwani ile unpopular ajenda yake ya muafaka imeshindikana na hana ujasiri kuhusu ile ajenda ya ufisadi ya Chadema.

  Halafu msisahau kuna connection ya Jussa-Rostam kwani hawa ni maswahiba wakubwa sana. Uswahiba huu ndiyo umemteka Profesa hali kadhalika Hamad Rashid -- kwani wote hawa wawili wanaonekana kubadili tyuni kuhusu vita dhidi ya ufisadi. Swali la Hamad kwa Pinda katika kikao cha Bunge kilichopita kilikuwa na mwelekeo wa tyuni hii mpya.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kwani hukuona kile kitendo chake cha kuungana na Safu ya

  Mawaziri waSerikali ya CCM, akina Simba na Mkuchika katika

  kupinga kutajwa list ya mafisadi?

  Kwasasa hana jipya, amepoteza mwelekeo, and he is good-4-

  nothing. Na nyie wana JF, mmekosa confidence?

  Au hampendi madaraka? Embu atoke huku mtu jasiri,

  agombee `Umiliki wa inji hii`, via the so called upinzani,

  tutampa full support.... Eboo!
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nimesikia Freeman Mbowe, Dr Wilbroad Slaa, Zitto Zubeir Kabwe WOTE CCM ila kule wanayeyusha watu tuu.....
   
 8. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Baba wa Taifa Hakutaka huu utitiri wa vyama kwa maana alisadiki katika msafara wa mamba, basi kenge wapo kibao tu. Ndio maana alitaka kuona ccm ileile inagawanyika katika mapande mawili, maana hapo lazima pumba ingeonekana na mchele ungeonekana. Lipumba & Co wanatumika na wanalipwa kwa hicho wanachokifanya.
   
 9. A

  Arnold Member

  #9
  May 19, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo file ya PDF mbona haifunguki ingawa nimeweza kuidownload nisaidieni tafadhali
   
 10. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  du arnold haujaingia cha kike?
   
 11. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  PDF ipi mkuu?Ni kwenye hii thread kweli?!
   
 12. M

  Msuruhishi Member

  #12
  May 19, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Lipumba, Kikwete, Lowassa na wenzao wote walitwaliwa kwenye USHUSHUSHU wakiwa bado mashuleni. Darasa la Kikwete pale Tanga School, 80% walikuwa recruited kwenye system. Ukiingia, hutoki!

  Msuruhishi
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Karibu msuruhishi jamvini naona post yako ya kwanza ni data nyeti za ushushu inavyoelekea maswali ya waungwana hapa kuhusu hizo issue yatajibiwa
   
 14. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  No no no no no no no no. Labda Zitto mzee wa Dowans.
   
 15. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #15
  May 19, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mashauri,
  sijawahi kuwa mwanachama wa CCM maisha yangu yote na ninamwomba mungu kila siku nisijiunge na chama hicho. Nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16 na sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote! Muhimu zaidi la kuzingatia ni kuwa kwetu Kigoma, CHADEMA ni zaidi ya chama cha siasa. mtu yeyote wa Kigoma mwenye akili timamu hawezi kuhama CHADEMA au hata kuwa pandikizi la CCM ndani ya CHADEMA. Kwa Kigoma, CHADEMA ni 'movement' na msaliti wa movement hutengwa - tazama Dkt. Kabourou.

  Suala la Dowans ni suala la msimamo wa mtu binafsi. Nihukumiwe kwa hilo hilo!
   
 16. A

  August JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Na naomba uwakumbushe Wapiga Kura wa Busanda, wasikubali kuwapigia CCM, au CUF au UDP, maana hizo ni njama za CCM za divide and rule, na nasikia wameanza kuangusha nguzo za Umeme, wambie hicho ni chambo kama wanachopewa samaki, nao wakiwa kama binadamu waaakili zaidi ya samaki. na wakumbuke walio waibia madini ni nani? ccm? Sasa wasikubali kuibiwa mabilioni nao wakapewa milioni.
   
 17. M

  Masatu JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Si useme tu umevuta....
   
 18. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #18
  May 19, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  sijavuta
   
 19. M

  Masatu JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tawire!
   
 20. M

  Mwakaleli Member

  #20
  May 19, 2009
  Joined: Sep 23, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana Zito kwa majibu yako mazuri, nimeyapenda. mtu anaacha kujadili kilicholetwa anarukia habari nyingine, suala linalojadiliwa hapa ni Lipumba habari ya Zito imetoka wapi. Swala la Dowans lilishaisha sasa tuangalie mambo yaliyo mbele yetu ndiyo tuyajadili. Naona si vema kuendelea kukashifiana wakati suala lenyewe lilishaelezwa, kwa staili hiyo tutakuwa hatujengi msingi ulio bora tutakuwa tunawakatisha tamaa watu wanaofanya kazi ya kulikomboa taifa letu. Asanteni tuendelee na mjadala
   
Loading...