Lipumba NI CCM ?

Mashauri,
sijawahi kuwa mwanachama wa CCM maisha yangu yote na ninamwomba mungu kila siku nisijiunge na chama hicho. Nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16 na sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote! Muhimu zaidi la kuzingatia ni kuwa kwetu Kigoma, CHADEMA ni zaidi ya chama cha siasa. mtu yeyote wa Kigoma mwenye akili timamu hawezi kuhama CHADEMA au hata kuwa pandikizi la CCM ndani ya CHADEMA. Kwa Kigoma, CHADEMA ni 'movement' na msaliti wa movement hutengwa - tazama Dkt. Kabourou.

Suala la Dowans ni suala la msimamo wa mtu binafsi. Nihukumiwe kwa hilo hilo!

Ni msimamo thabiti kwamba unakubali kuwa kwa suala la Dowans uhukumiwe kwa utashi wako wewe binafsi!! As long as your conscience is very clear on the Dowans issue you can soldier on; bahati mbaya wengi walipata hisia kuwa kijana wetu tulikwisha kupoteza kwa VIJISENTI vya Rostam!!
 
Mh Zitto,
Msimamo kuhusu Dowans ni wako binafsi, lakini kwa nature ya kampuni yenyewe , msimamo wako ni catastrophic, morally and politically!
 
sometimes i also wonder what prof.lipumba is after? he damn knows well that he can never win but he keeps running...huyu bwana analingine zaidi ya siasa...politics is madness..those you think are with you they may well be very against u...juzi mmesikia amelisifia jeshi la polisi kule busanda...kwa lipi..kuwazibibi chadema...no one is CLEAN in the oposition side...kama hata zito inasemekana ni wao...who else???? na hiyo ni njia ya kuendelea kuwatawala milele..upinzani wa kweli upo visiwani znz..
 
sometimes i also wonder what prof.lipumba is after? he damn knows well that he can never win but he keeps running...huyu bwana analingine zaidi ya siasa...politics is madness..those you think are with you they may well be very against u...juzi mmesikia amelisifia jeshi la polisi kule busanda...kwa lipi..kuwazibibi chadema...no one is CLEAN in the oposition side...kama hata zito inasemekana ni wao...who else???? na hiyo ni njia ya kuendelea kuwatawala milele..upinzani wa kweli upo visiwani znz..
Mtazamo wako,
Umekosea. Si kweli kwamba upinzani haupo Tanzania. Upo lakini mapandikizi kama nyinyi wanajifanya kutushawishi kwamba haupo ili ufe. Na hakika hautakufa maana kila sisi m wanapojaribu kuua unafufuka kutokea angle nyingine.
Kwa taarifa yako leo ni Chadema tu ndio amekuwa mpinzani wa kweli wa sisi wezi. Na hili nimelifuatilia kwa kipindi kirefu. Ni chadema tu kwa sasa ambacho ni chama makini na hakina zuruzunga. Nimeamua kuchukua na kadi yao ili niwe mwanachama wiki chache zilizopita huku kwetu Busanda na kadi yangu ni namba CDM 0135918.
Hivyo usipotoshe ukweli kwa vijisababu.
 
NI muhimu kuelewa kuwa mwelekeo wa demokrasia katika nchi hii unaongozwa na CCM yani (controlled transition). Ndio maana hakuna level playing field. CCM imeendelea kutumia sheria mbali mbali kuwabana mbavu wapinzani kwa kutumia vyombo mbali mbali kama vile mahakama na Tume ya uchaguzi. Kuenguliwa kwa mgombea wa chadema kule mbeya ni mfano mmoja tu ! Mie nilidhani NEC ingemdisqulify mgombea on serious grounds kama uraia, wizi au mambo mengine not on mere administrative issues.Je unafahamu kuwa JAPO TUPO KWENYE VYAMA VINGI , CCM haijawa registered kwa bwana tendwa na in fact tendwa hawezi kui-deregister ccm hata pale itakapovunja taratibu. Kwa kupitia taasisi kama nec, msajili wa vyama...ccm imeendelea ku-control hii transition wanavyotaka. Wajua kwamba, ule utaratibu wa kugawa ruzuku kwa vyama ulitosha tu kusambaratisha upinzani miaka ya tisini? Kesho tendwa anampa mwyekiti, keshokutwa wanampa katibu, mtondo go wanampa mhazini. Hii ilikuwa ni tekniki dhahiri ya kuua upinzani.[/COLOR][/B]
 
Sa zingine tuangalie cha kuchukua katika tunavyosikia. Hivi Kina Slaa na wenzake hata kama ni mamluki, kwa style hii wanaua vibaya na hawana faida kama wanataja wanaoitwa mafisadi wahujumu uchumi na wazandiki, sioni faida ya kuwatumia watu kama hawa kwani siku wakirudi kundini tayari mshatoboka. I like the team, ni wanasiasa hasa hawasubiri uchaguzi kama kina Lipumba na siasa zao za kitoto (kusubiri uchaguzi). Inasikitisha mtu kama Prof. Lip kupata brain atrophy mapema hivi. Kutumiwa na wapemba katika siasa za fitna. Poleni watanganyika wenzangu
 
Inawezekanaje pro Lipumba awe ccm wakati mtu huyu alifikia kupigwa na kuumizwa mkono kwa ajili ya kutetea wanyonge.. NANI ANAKUBALI KUUMIZA MWILI WAKE HALAFU AWE MAMLUKI... haiwezekani. sijaona viongozi wa upinzani walioteswa saana isipokuwa CUF...

-Mdau mmoja humu kaponda kuchaguliwa Lipumba kwa asilimia kubwa,na ati pr Safari kasusa.. Kwanza kuchaguliwa kwa ushindi mkubwa ndani ya cuf ni ushahidi tosha kua wanachama wanamkubali kwa kitendo chake cha kua mkweli na muadilifu.. Amejitahidi saana kukisambaza chama,amehangaika saana,kwa wanaomfatilia wanajua jinsi gani alivopata tabu hata kwenda kwa miguu kwa masafa marefu vijijini huku akikutana na vikwazo vingi vya ccm.. Na kuhusu pr. safari fatilia uzuri ndugu yangu nini kilichomkwamisha,pamoja na kua Lipumba anakubalika lkn ndani ya mkutano wa wanachama kabla ya uchaguzi pr. safari aliulizwa masuala muhimu alishindwa kujibu... hiyo ni miongoni mwa sababu tu...

-Mdau mwengine amechangia humu kwa kusema ati ajenda ya muafaka.pale ndo kafeli.. Ndugu yangu ccm tunaijua na kwa kauli hadharani wanasema serikali haitoki kwa karatasi.. tuliona waznz walivyoteswa,wakati wa uchaguzi jeshi lilikuwa kubwa kuliko hao wananchi,nilikuwepo kwenda kushuhudia,sikuwahi kuona machoni.. Ilifikia wa znz kuzungukwa muda wa siku tatu mtendeni hali ya kuwa wamefunga,hiyo ndio ccm.. kama Lipumba hana kosa bali muafaka ni wa cuf wote na baraza kuu ndilo linaloamua,kwa unafiki wa ccm ndio waliokataa.. Heko kwa cuf na Lipumba waliwavuta ccm mpaka wakakwama wao,na hapo cuf ndio ikajitoa wakati watz wote wanaona ccm ndio iliokataa,na kujua unafiki wao... CUF ni watu wa busara lkn ccm ni wauaji..

-Mdau huyo huyo akasema ati Lipumba kafeli kwa muafaka wakati wenzake kina zito,slaa wameanzisha mada ya ufisadi na kuja juu... Ndugu yangu upo TZ au upo nje?... Siku ya kwanza kujua habari ya ufisadi wa serikali yetu nilikuwa kenya,nikapewa karatasi ambazo zinaelezea ufisadi wa tz... nilivorudi TZ,baada ya miezi kama 6 Nikamsikia Pr Lipumba anazungumzia ufisadi na mafisadi mbele ya waandishi wa habari.. ndo mara ya kwanza tz kutajwa hadharani kuhusu ufisadi,baadae ndipo wakaja mashujaa wetu wengine kina Slaa na Zitto... nitafute kwa wakati wako nitakupa vitu kwa tarehe... Na mpaka sasa hakuna mwengine alietaja moja kwa moja kua Rais Kikwete anahusika na ufisadi isipokua Lipumba pekee... Njoo nikupe kanda..

-Mdau mwengine kasema kaungana na ccm na mkuchika kupinga ufisadi ulotajwa na mengi.. Baba amka!!!!! kwanza Hata viongozi wengine wa upinzani akiwemo mrema walimpinga Mengi... wote hawa hawakupinga ufisadi bali wamepinga njia alizotumia Bw Mengi,pamoja na maneno makali aloyatoa kwa umma.. Kama kapinga ufisadi inakuwaje ameanzisha yeye mada ya ufisadi... kua makini baba,fatilia uzuri...

-Mdau mwengine amesema kumwambia zitto awaambie wananchi wa busanda wasichague ccm,cuf nk kwani hao hawafai.. kwa upande wangu ikichukua chadema au cuf nitafurahi yote sawa lkn sio ccm.. laiti habari za cuf zingekua zinatolewa kama inavotolewa ccm na chadema ungeona jinsi gani cuf ina nguvu mikoani lkn kwa uoga wa ccm dhidi ya Cuf wamefanya kila njia kuhakikisha cuf haitajwi sana habari zake,wapo tayari chadema watajwe kuliko cuf.. Yote hii ni kwa sababu wanaiogopa Cuf...
 
Mashauri,
sijawahi kuwa mwanachama wa CCM maisha yangu yote na ninamwomba mungu kila siku nisijiunge na chama hicho. Nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16 na sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote! Muhimu zaidi la kuzingatia ni kuwa kwetu Kigoma, CHADEMA ni zaidi ya chama cha siasa. mtu yeyote wa Kigoma mwenye akili timamu hawezi kuhama CHADEMA au hata kuwa pandikizi la CCM ndani ya CHADEMA. Kwa Kigoma, CHADEMA ni 'movement' na msaliti wa movement hutengwa - tazama Dkt. Kabourou.

Suala la Dowans ni suala la msimamo wa mtu binafsi. Nihukumiwe kwa hilo hilo!
Ndugu yangu ZITTO nimekupenda sana kwa hili. Na MUNGU atakusaidia kutimiza dhamiri yako hiyo iliyo njema kabisa
 
Kuna tetesi kuwa mkutano mkuu wa CUF ulifadhiliwa na RA kwa shiling million mia mbili kuna anayejua zaidi kuhusu hili?
 
mukubwa..
Si kweli RA amefadhili mkutano mkuu wa cuf,hicho kitu hakipo,wapo matajiri wa dhati wanasaidia cuf kwa kuipenda cuf,na wanatumia mali zao kwa ajili ya cuf tena si mafisadi kama kina RA wa ccm... cuf hawana mafisadi... tafuta jengine.. nafkiri unatumwa kama sikosei... nitakutajia baadhi ya matajiri lkn kwa wakati wako... si kitu muafaka kueka wazi hapa..
 

Miongoni mwa wapinzani wa kweli,naamin mmoja ni wewe,lkn sio hao wa juu yako, bt hebu niambie smthn,kwanini chama chako hakipendi Muungano wa vyama vyengine vya upinzani,kuna nini huko ndani, la pili hebu niambie niliwahi kukuskia ukilalamika kuhusu yule mgombea wa cuf wa jimbo lako,ukisema sio cuf kweli bado ni ccm,je wanaoingia chadema tu wakitoka ccm ndio waaminifu? lkn wakiingia cuf sio waaminifu?
 
Hata mimi nimesikia Freeman Mbowe, Dr Wilbroad Slaa, Zitto Zubeir Kabwe WOTE CCM ila kule wanayeyusha watu tuu.....


Huu ni uzushi mtupu....... Sipendi wazushi kama nini....... Nawajua hawa wote, wakikosa huku watakimbilia kule.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom