Lipumba awavaa viongozi CHADEMA

Lipumba awavaa viongozi CHADEMA

huu uzi hauna ukweli wowote.wachangiaji muwe makini na nyuzi izi za kichochezi.habari haina chanzi.mleta mada katunga yake tu ili kuleta mpasuko.humu jamvini.ukawa ipo ngangari na itaendelea kuwa daima
 
Na Benedict Kaguo, Pangani

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakina nia thabiti ya kupambana na ufisadi kutokana kuchochea mgawanyiko wa Watanzania.


Alisema chama chochote cha siasa kilichoshindwa kuthamini matakwa ya wananchi wake hakina nia ya dhati ya kuwaletea ukombozi wa kweli wanaouhitaji Watanzania kwa sasa.


Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Pangani katika mwendelezo wa mikutano ya chama hicho 'kuwazindua Watanzania katika kujenga demokrasia ya kweli hapa nchi'.


Alisema wafanyabiashara wa Chadema hawawezi kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi kwa kuwa tayari wako katika mazingira ya kukumbatia rushwa, hivyo ni vigumu wao kuongoza mapambano hayo kama wanavyodai.


“Ndugu zangu wafanyabiashara na wapiga disko wa Chadema wanataka kuwang'oa mapapa ya ufisadi wa CCM ili wao manyangumi ya ufisadi waweze kuingia madarakani, hawana nia thabiti ya kupambana na rushwa,” alisema Profesa Lipumba.


Alisema aliingia kwenye siasa kwa lengo la kuwasaidia Watanzania sio kutafuta sifa kama walivyo baadhi ya wanasiasa wa Chadema.


"Sikuingia kwenye siasa kutafuta sifa, nimeingia kutumia elimu yangu kuwatafutia ukombozi Watanzania wenzangu, sasa hawa Chadema hawawezi kuiondoa CCM kwa kuwa wanachochea mgawanyiko mkubwa ndani ya nchi kwa kuwatukana Wanzanzibari waliokubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Profesa Lipumba.


Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro alisema taifa linaangamia kwa kukosekana uongozi ulio madhubuti sasa ni wakati wa Watanzania kuzinduka ili uchaguzi mkuu ujao waweze kukipa ridhaa chama makini cha CUF.


“Maisha yamekuwa ya kubabaisha huduma za afya hospitalini mama zangu mnatakiwa mwende na nyembe mnapotaka kujifungua, serikali inashindwa kununua wembe lakini wakati wa uchaguzi inaweza kununua kitenge kwa kila mwanamke Tanzania nzima,” alisema Bw. Mtatiro.


Alisema wakati wa mabadiliko ndio huu na wananchi hawana budi kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kuongoza mapambano dhidi ya rushwa, matumizi mabaya ya fedha za umma ili kuwakomboa wananchi.

Hii post vipi yasomeka 23 Machi 2011? Chanzo cha taarifa tafadhali. Vinginevyo yalenga kuihujumu UKAWA
 
Hapa ndo utagundua wanajoiita makamanda kila kukicha hata kusoma hawawezi!! Ni kukurupuka tu!!!

Pythagoras nakubaliana nawe hata mwenyewe nimeishtukia tarehe ya bandiko ni 23 Mar 2011. Bila kujulishwa chanzo cha taarifa nasita kuamini. Umpo mchezo hapa!!
 
Sidhani kama prof. Mzima anaweza kusema ivo tuwemakini jaman na watoa mada na mashaka na mtoa mada kuwa ni mwana Act-wazalendo
 
Kweli nimeamini kwenye siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu ikiwa vyama vilivyotoleana matusi ya namna hii leo wanakaa meza moja na kukubaliana,
Kweli wanasiasa wekeni akiba ya maneno.

ndio mana Zitto kawaambia waweke akiba ya maneno
 
Hawa CUF sio watu kabisa..,....Hawa jamaa hawafai kabisa na inabidi CHADEMA wakae nao mbali kabisa maana hawana mpango........Vigeu geu kama watoto

hahaha ati nini?
 
alie fufua huu uzi kanichekesha sana, maana anakumbusha mengi.
 
Inafik hatua viongozi wa ccm wanaongea hadharani kuwa ikulu itabaki kuwa yao milele unadhan wanamaanisha nini inamaana kuwa wananchi wake ni wasahaulifi hawana lolote
 
Hivi kweli mtanzania mwenye akili timamu mpaka Leo hii unaishabikia CCM kwakweli imebaki kidogo wananchi wa Tanzania nawenyewe waingizw kwenye maajabu saba ya dunia imefika muda na wapinzani waonje kama nikuiba waibe na wenyewe wasomeshe wajenge kama wenzao ccm
 
Hivi umesahau tembo, twiga wanao safirishwa wazimawazima ulaya, RICHMOND ,EPA na ESCROW ya juzi umesahau MTU mmoja anachukua billion 1.8 per day halafu badogo unamchekelea unasbikia then unaambiwa nchi maskini
 
Hivi umesahau tembo, twiga wanao safirishwa wazimawazima ulaya, RICHMOND ,EPA na ESCROW ya juzi umesahau MTU mmoja anachukua billion 1.8 per day halafu badogo unamchekelea unasbikia then unaambiwa nchi maskini

Mkuu ni kweli wananchi wameichoka ccm,je hawa jamaa chadema wakiingia watafanya nini zaidi ya kutuibia zaidi kama alivyosema msomi wetu pro lipumba.Mbowe alishasema hawezi kufanya mkutano bila helkopta wakati wananchi hata baiskeli hawana,je ni haki hiyo?ki ukweli wote ni wezi tu,Lipumba kaongea kweli
 
mtoa post usitufanye sisi machizi na ukaandika upuuzi ukajua tutaamini ujinga wako tuletee clip ambayo prof lipumba amesema maneno haya ila usilete ushangingi na umbea wa wazi namna hii, ukisoma tu unajua yya kwamba una nia mbya na lipumba kumchafua shame on you:A S-baby::A S-baby::A S-baby::A S-baby:
 
Back
Top Bottom