Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba, amerejea leo jijini Dar na kupokelewa kwa maandamano makubwa ya washabiki, wananachama na wakazi wa jiji kwa ujumla.
Umati wa watu ulisababisha barabara nyingi kufungwa ili kupisha maandamano hayo yaliyoishia viwanja vya Jangwani ambapo Prof Lipumba alihutubia wananchi.
Profesa Lipumba ambae kwa sasa anafanyakazi ya mkataba wa mwaka mmoja na UN anatazamiwa kukaa nchini kwa miezi mitatu kabla ya kwenda kumalizia ngwe ya mwisho ya mkataba wake.
Wapenzi na washabiki wa CUF walikumbwa na kiwewe kama wamepagawa walikuwa wakiimba na kumsifu Lipumba na kukejeli CCM hususan upotevu wa mabilioni ya pesa BOT.
Wananchi wengi wanaamini Lipumba na CUF wana nafasi kubwa ya kuiangusha CCM uchaguzi ujao kutokana na msimamo usioyumba wa viongozi wa juu wa CUF.