Lipumba atua Dar kwa kishindo!

Masatu...Tumezoeshwa kukuona unatetea mafisadi. Kumbe analysis zako zinatisha.
Uzuri wa JF mtu akija na data feki, basi kuna wajuzi wa mambo watamuweka sawa.

Kitila always amekuwa ana balance mambo, mara nyingi amekuwa anasimamia Kweli.keep it up
 
Mkuu ES niweke sawa..ktk baadhi ya post umeonesha kuwa upo US unaendesha Malori...hapa umesema ulishafanya Intern hao UN, hivi UN kuna intern ya Kuendesha Malori? au Ubaharia?...tuweke sawa
 
Chuma suala sio kutetea mafisadi bali ni kutetea haki na ukweli na hicho ndio ninachokiamini na kukisimamia call me CCM or mtetezi wa mafisadi lakini Im used to those accusations, wale open minded people wataona ukweli lakini mawazo mgando wataishia kusema CCM na mtetezi wa mafisadi
 
..hawa wananchi wengi ni wa nchi gani? hii tanganyika au hiyo zanzibar?

..hivi msimamo wa viongozi wa ccm juu ya kushinda uchaguzi ushawahi kuyumba?

..ni jinsi ninavyoyaona mambo tu! si zaidi!

Ndiyo matatizo ya uandishi wetu hayo, sasa "wananchi wengi" ulikaa nao saa ngapi wakakuambia hivyo? Wengi kiasi gani? Unatoa data wapi? kuna poll gani ilifanyika? Wakisema umeshikishwa na Lipumba umpambe utakataa?
 
Mkuu ES niweke sawa..ktk baadhi ya post umeonesha kuwa upo US unaendesha Malori...hapa umesema ulishafanya Intern hao UN, hivi UN kuna intern ya Kuendesha Malori? au Ubaharia?...tuweke sawa
Kazi ipo.Iron subiri majibu!
 
Chuma suala sio kutetea mafisadi bali ni kutetea haki na ukweli na hicho ndio ninachokiamini na kukisimamia call me CCM or mtetezi wa mafisadi lakini Im used to those accusations, wale open minded people wataona ukweli lakini mawazo mgando wataishia kusema CCM na mtetezi wa mafisadi

Masatu:

Kati posti yako unasema Lipumba anapenda kulialia kuwa anaonewa. Kuna posti imetoka kule ambayo inaonyesha kampuni zilizofanya ufisadi zilifunguliwa 2005 karibu na uchaguzi mkuu.

Je ni mtu gani anayeshindwa kuunganisha dots kuwa sehemu ya malipo ya uchaguzi zilitumika kwenye uchaguzi kuisaidia CCM?
 
Balali also is talented academic turned
very respected world wide, a man made significat changes to some countries .
Balali as a senior expert with permanent employement on IMF desk but sadly enough brought tragedy to tanzanians .
Mimi naomba niulize mbona msomi akitokea CCM haitwi kichwa .??? ila akitokea upinzani kwa kazi zile zile elimu ile ile shule ile ile anaitwa kichwa???

Mtanzania
mie binafsi nimekuelewa vizuri na nafikiri siku watanzania tutakapokua na mawazo kama yako maendeleo ya kweli yatapatikana.Wapinzani watupe sera na sio blah blah eti watatoa huduma huduma za afya bure,elimu bure.Sawa sie tunachotoka sera kwa njisi ipi mtapata hizo fedha za kuendesha hayo mambo.
Sio kukimbilia mikataba ya madini je madini yasipokuwapo ama yakiisha leo then ina maana wapinzani hawatakua na sera ama vipi??
wapinzani tunataka sera za kiuchumi na kama hamna jiungeni na CCM.
Kuubua ufisadi ni vyema lakini hii sio indicator ya kua eti kwa vile ufisadi umeubua tukupe nchi .
Sera zenu zikowapi?? za CCM ndio marehemu kabisa ila ni za zimwi tulijualo.
Mie binafsi naona watu binafsi wana sera nzuri kuliko chama hivyo ningeonelea CCM wawape tu uhuru wagombea binafsi.
 
nimesahau
--------------------------------------------------------------------------------

Balali also is talented academic turned
very respected world wide but except in his homeland tz, a man made significat changes to some countries .
 
Masatu:

Kati posti yako unasema Lipumba anapenda kulialia kuwa anaonewa. Kuna posti imetoka kule ambayo inaonyesha kampuni zilizofanya ufisadi zilifunguliwa 2005 karibu na uchaguzi mkuu.

Je ni mtu gani anayeshindwa kuunganisha dots kuwa sehemu ya malipo ya uchaguzi zilitumika kwenye uchaguzi kuisaidia CCM?

Bin Maryam nadhani unanifananisha na somebody else ambae akisoma atajijua ni nani... sijawahi na wala sina mpango wa kusema eti Lipumba analialia kuwa anaonewa.

Chukua taabu kidogo ya kurudi nyuma (kwenye thread hii hii) utamjua nani aliesema Lipumba anapenda kulia lia kuwa anaonewa.

Goodluck in ur exercise...
 
Sorry mate.
 
Balali also is talented academic turned
very respected world wide, a man made significat changes to some countries .
Balali as a senior expert with permanent employement on IMF desk but sadly enough brought tragedy to tanzanians .
Mimi naomba niulize mbona msomi akitokea CCM haitwi kichwa .??? ila akitokea upinzani kwa kazi zile zile elimu ile ile shule ile ile anaitwa kichwa???

Mtanzania
mie binafsi nimekuelewa vizuri na nafikiri siku watanzania tutakapokua na mawazo kama yako maendeleo ya kweli yatapatikana.Wapinzani watupe sera na sio blah blah eti watatoa huduma huduma za afya bure,elimu bure.Sawa sie tunachotoka sera kwa njisi ipi mtapata hizo fedha za kuendesha hayo mambo.
Sio kukimbilia mikataba ya madini je madini yasipokuwapo ama yakiisha leo then ina maana wapinzani hawatakua na sera ama vipi??
wapinzani tunataka sera za kiuchumi na kama hamna jiungeni na CCM.
Kuubua ufisadi ni vyema lakini hii sio indicator ya kua eti kwa vile ufisadi umeubua tukupe nchi .
Sera zenu zikowapi?? za CCM ndio marehemu kabisa ila ni za zimwi tulijualo.
Mie binafsi naona watu binafsi wana sera nzuri kuliko chama hivyo ningeonelea CCM wawape tu uhuru wagombea binafsi.

Mkamap:

Fuatia yaliotokea Poland. Wakati wanataka kuondoa u-kommunisti, kiongozi aliyeongoza alikuwa LECH WALESA. Elimu yake ilikuwa ni sawa na mtu aliyekwenda kuchukua ufundi umeme pale Chang'ombe (VETA). Alikuwa hana program yoyote zaidi ya kudai haki za watu kujiamulia mambo yao wenyewe. Watu waliosoma na wasiosoma na wenye kutaka mabadiliko walikuwa nyuma.

Mabadiliko yalipopatikana walimuachia madaraka kwa muda fulani na walipoona spidi zake ni ndogo katika mambo ya uchumi walimuondoa.

Watanzania hakuna sababu ya kuogopa mtu au chama kisicho na sera nzuri. Kinachotakiwa ni kuwaweka CCM benchi wapate shule.
 
Mkuu Chuma,

Huyo jamaa unayemuongelea sio mimi, mimi ni baharia sijawahi kusema ninaishia wapi, wala kazi ninayofanya sasa, isipokuwa nilmeishi sana US, nikasoma shule na wakati nikiwa shule niliwahi kufanya intern UN, kupitia ubalozi wa Dominican Republic, na nilikuwa kila siku ya mungu nikiwa pale ubalozini muda wangu wote nilikuwa nikishinda nao hao Spanish kwenye GA, hayo mengine sijawahi kuyasema huwa yanasemwa na wengine wakinihisi kuwa ni mimi, ila ninarudia kuwa sijawahi kujisema kuwa ninafanya hiyo suhughuli, ingawa ninaaamini kuwa unayomuongela alisoma akaweka degree zake nyumbani, na ana-own Tractor and Trailers kama mbili huko ma-US labda ungemtafuta akupe na wewe huo ujanja wa ujasirimali mkuu huko kwa wazungu, ingawa by the way nafikiri ukisoma historia ya Rais wa Zamani mwanamapinduzi wa Poland, bwana Walesa, utagundua kuwa na yeye alikuwa ameabobea kwenye sekta kama hiyo ya mkuu ya Transportation, yaaani kuendesha Trailers baadaye akawa rais wa Poland, kwa hiyo kusoma na kuendesha sidhani kama ina matatizo kama ulikuwa hujui mkuu, ingawa najua your point kuwa hujaona mtu bongo wa aina hiyo aliyepiga kitabu halafu anamiliki trucks na kuendesha mwenyewe, lakini sio mimi mkuu! By the way vipi wewe mkuu unafanya nini na sister Caroline anaendeleaje mkuu?

Mkuu Masatu,

I am not impressed na sijawahi na hoja zako za kuwatetea kina Mkapa, na Mama Meghji, na I am tooo big na hizo hoja zako za choooni just keep them to your self mkuu, mimi sijifunzi elimu toka kwa mwananchi mbongo anayeweza kumtetea Mkapa, kwangu ni out of question mkuu kabisaaa, ndio maana huwa sijihusishi na hoja zako, isipokuwa huwa ninajitahidi kukusaidia unapopigwa makombora kwenye kutetea kwako mafisadi hasa unaporushiwa matusi kama unayonirushia sasa!

Have a Good day mkuu!
 
Mkamap:

Fuatia yaliotokea Poland. Wakati wanataka kuondoa u-kommunisti, kiongozi aliyeongoza alikuwa LECH WALESA. Elimu yake ilikuwa ni sawa na mtu aliyekwenda kuchukua ufundi umeme pale Chang'ombe (VETA). Alikuwa hana program yoyote zaidi ya kudai haki za watu kujiamulia mambo yao wenyewe. Watu waliosoma na wasiosoma na wenye kutaka mabadiliko walikuwa nyuma.

Mabadiliko yalipopatikana walimuachia madaraka kwa muda fulani na walipoona spidi zake ni ndogo katika mambo ya uchumi walimuondoa.

Watanzania hakuna sababu ya kuogopa mtu au chama kisicho na sera nzuri. Kinachotakiwa ni kuwaweka CCM benchi wapate shule.

ok
ni sawa
Lakini kwa Poland aliyekua sterling wa kuua ukomunist alikua papa John Paul wa II.
WALESA alikua anatumiwa tu na huyu Pope na ndio maana Poland wanaheshimu sana kazi iliyofanywa na Pope huyu kuvunja ukomunisiti na ndio mkombozi wao na si WALESA.
Ndio huyu pope aliyechukiwa sana na makoministi wa Rusia ambao walidiriki kumtumia mafia walio mfyatulia risasi kadhaa tumboni kwake na kusababisha ungonjwa wake ambao ulimpelekea hadi kuyafika mauti.
POPE alikua ENGINE ama B52 iliyosambaratisha ukomunisti haswa Poland kwa kumtumia WALESA.
Sasa engine mhimu kwetu ni ipi???
 
mbona haisemwi kwamba baada ya kutoka kumshauri mwinyi
lipumba alikuwa mshauri wa uchumi wa museveni na uchumi wa uganda ukapaa? sasa kwa nini uganda afanikiwe na bongo ashindwe?
nadhani tatizo limeelezwa hapo juu.

kama ilivyoelezwa hapo juu un kuna kazi na kazi. zipo zile zenye mwelekeo wa kisiasa/kidiplomasia ambapo mtu inabidi aungwe mkono na serikali yake. lakini zile za utaalamu (consultancy) mara nyingi mtu ahitaji kuungwa mkono na serikali yake mfano kazi anazofanya prof. lipumba, prof. wangwe na wengine wengi.

hata nafasi aliyoingia mama tibaijuka unctad (coordinator wa ldcs) ni nafasi aliyoomba mwenyewe bila kuungwa mkono na serikali (wakati huo ndo kwanza ile ngo yake ilitoka kufungiwa). katika kinyanganyiro hicho cha kazi hiyo pia walikuwemo wazito wengine wa serikali ya bongo.

mfano wa nafasi ambazo serikali iliunga mkono wa watu wake ni ile kama ya mama migiro, balozi mchumo (common fund) na ile ya fao (miaka 1996/979 ambayo mkongwe moja wa siasa aliitolea nje nadhani baada ya kushtuka kwamba jamaa wanaompendekeza wana nia ya kisiasa.
 
Mkuu FMES, wengine hatujafanya kazi UN lakini tunajua protocol zao. Wakikutaka watakupata hata kama serikali yako haitaki maana serikali haiwezi kugoma kutoa recommendation bila sababu
,

Mkuu Kitila,

Heshima mbele mkuu, Bandora, Manongi, Mohamed Yusuf, Mama Kapalata, Mama Mula mula mdogo, wapo huko UN, utaratibu ni ule ule ni lazima serikali yako itoe kibali, in fact yule mama wa Nigeria, ndiye hasa aliyetakiwa kushika nafasi ya Mama Migiro, baada ya UN kuiomba kwanza serikali ya Nigeria kama protocol za huko UN zinavyodai, serikali ya Nigeria ikakataa hakuenda, pamoja na kutakwa kote na UN, hao niliowataja juu nao pia wangekataliwa na serikali yetu wasingeeenda mkuu ndivyo utaratibu ulivyo huko UN. Pia kule UN niliwahi kuwaona waa-Afrika kama Gen. Gambari wa Nigeria na Mikanangu wa Burundi, hawa ni viongozi wasiotakiwa kwao kabisa, lakini still ni lazima serikali itoe kibali ili wabaki huko UN ambako wamekuwa huko kwa muda mrefu sana. Mzee Masha, alikataliwa kuruhusiwa kufanya kazi hapa bongo enzi zile mwishowe UN wakamchukua, na ikabidi serikali yetu itoe kibali kwanza hiyo ni procedure ambayo haiwezi kubadilishwa kwa sababu ni Lipumba kuwa na PHD mkuu.

2. [
B]Niseme pia kwamba una haki ya kutokumpenda Lipumba as a politician, lakini sidhani kama una haki ya kujaribu kuharibu reputation yake ya kuwa an opposition leader kwa kutilia shaka spirit yake ya upinzani.[/B]

Ni kweli kabisaa mkuu simpendi huyu mkuu kisiasa, na ni haki yangu pia kusema, kwa sababu CUF ambayo yeye ni mwenyekiti ndiyo iliyochochea maandamano kule visiwani, yaliyoishia kumwaga damu ya wananchi wanyonge wasiokuwa na PHD, kama yeye, je ile damu ilimwagika for what? Ili yeye akaishi Ulaya, na Seif kupewa marupu rupu na CCM ya u-ex PM? Exactly walichofanya ni nini kuienzi ile damu? Ndo maana I have a problem na the whole ishu ya Lipumba na siasa za opposition, maana to me ni fake na ndio maana tutaendelea kuchezewa na viongozi hawa uchwara, maana kwa ninyaoyasoma hapa ianonekana kuwa tulishasahau kila kitu, mimi hapana mkuu bado ninakumbuka na ile damu iatwaandama yeye na Seif mpaka wanaenda kwa Muuumba wao.

3.
He is a talented academic turned politician. He is one of the top and respected world class economist. Sasa hilo kwamba aliharibu uchumi wakati wa Mwinyi mbona maelezo yapo, tena yametolewa siyo na yeye bali na wanauchumi duniani. Kuna kitabu kimeandikwa na mwanauchumi mzuri ukitaka naweza kukutumia. Kwa kifupi ni kwamba kila alichoshauri Lipumba wana CCM walikata kutekeleza, sasa ulitaka afanyeje? Kumbuka yeye hakuwa waziri wa fedha wala waziri wa uchumi, alikuwa mshauri wa uchumi wa Rais. Sasa kumbe kama alishauri na ushauri wake ukakataliwa ndio tuseme kwamba yeye hafai? Mpe nafasi ya kufanya maamuzi then akishindwa ndiyo tumlaumu.

Elimu ya darasani sijakataa na wala sina tatizo naye, lakini ya kuongoza siasa na uchumi, hapana hana mkuu, kama ni ushauri wake kukataliwa, mbona hatujasikia alichokifanya ku-protest, maana waliokataliwa kina Mtei na Professor Rweyemamu, tunajua walichofanya baada ya kukataliwa ushauri wao na Mwalimu, je yeye alifanya nini mkuuu?

4. [
B]Mimi nakumbuka Tambo Mbeki kipindi chote cha mapambano ya apartheid SA alikuwa nje ya nchi akikata shule na alirudi 1990, lakini ndiye aliyemrithi Mandela na wala sio akina Ramaphosa ambao siku zote walikaa mle ndani na kufungwa sana tu. I mean tusiwe narrow minded kwenye kuangalia haya mambo, ni mapana sana nasi inabidi tuwe wapana pia.[/B]PS:

Thabo Mbeki, alipewa bure na Mandela, sasa umeona mkuu imekuja time ya kusimama mwenyewe bila Mandela, yaliyomkuta kushindana ma mzee wa ground zero, Zuma, aliyesota na wananchi miaka kumi jela, huko wananchi wameamka mkuu sio kama sisi, ndio maana Lipumba anaweza kupokelewa na shangwe na kushangiliwa na wananchi kama wewe, mimi siikubali hiyo dhana ya wananchi kuhangaika na mafisadi, halafu kiongozi wao wa kuwakomboa yuko nje anafanya kazi UN, badala ya kuhangaika nao, yaaani yeye Balali wote wako nje? Hapana mkuu mimi simo humo kama ni kuwa narrrow minded so be it mkuu! Wananchi kuuliwa halafu kiongozi wao anaenda nje kufanya kazi UN, hapana mkuu ndio maana tutaendelea kuchezewa tu na viongozi wetu bongo, lakini ni lazima niwape heshima kubwa kina Zitto, Dr. Slaa, Freeman ambaye pamoja kusoma nje, kila siku yupo kwenye mapambano bongo na mpaka sasa ameniondoa wasi wasi wangu niliokuwa nao zamani kuhusu spirit yake ya upinzani, maana I have seeen the man working his tail off kuwasaidia wananchi, na ninawatakiwa maisha marefu waendele kuwaamsha wananchi kama wanavyofanya sasa, na they have my vote.

5.
Nimeweka CV ya prof Lipumba hapo chini ili angalau upate kumjua vizuri maana naona unafikiri ni kada tu kama makada wengine.

Mkuu CV ya PHD, si hata Mzindakaya anayo au? Ninachojali ni what the man has done kwa kuwakomboa wananchi na ukoloni mambo leo tulionao mkuu, huwezi kuwakomboa wananchi wako bongo kama kiongozi wa upinzani, ukiwa unaishi Ulaya, ndio maaana nitaendelea kuwaunga mkono kina Zitto, Dr. Slaaa na Freeman, so far ndio the true opposition, wengine I am sorry mkuu na hasa huyu Lipumba na ndugu yake Seif.

Ahsante Mkuuu, tuendelee kukata ishus taifa liko njia panda!
 
Mkamap:

Fuatia yaliotokea Poland. Wakati wanataka kuondoa u-kommunisti, kiongozi aliyeongoza alikuwa LECH WALESA. Elimu yake ilikuwa ni sawa na mtu aliyekwenda kuchukua ufundi umeme pale Chang'ombe (VETA). Alikuwa hana program yoyote zaidi ya kudai haki za watu kujiamulia mambo yao wenyewe. Watu waliosoma na wasiosoma na wenye kutaka mabadiliko walikuwa nyuma.

Mabadiliko yalipopatikana walimuachia madaraka kwa muda fulani na walipoona spidi zake ni ndogo katika mambo ya uchumi walimuondoa.

Watanzania hakuna sababu ya kuogopa mtu au chama kisicho na sera nzuri. Kinachotakiwa ni kuwaweka CCM benchi wapate shule.

Bin Maryam,

Check facts na dataz zako maana ulichosema hapo sio sahihi sana.

Ni kweli Lech Walesa aliongoza hayo mapambano, pia ni kweli hakuwa na elimu nzuri na nyuma yake kulikuwa na wasomi wengi wakiongozwa na Prof. Mazowiecki.

Mwaka 1989 Solidarity ya Walesa walishinda na watu walitegemea Solidarity waunde serikali na kuchukua urais. Lakini washauri wao wakasema hapana, hawakuwa tayari, wakatumia ujanja ambao ndio uliisaidia sana Poland miaka ya mwanzoni. Wakaamua kuacha kwanza kuchukua urais wakati wanajipanga na kuanda sera mpya. Kwahiyo kwa zaidi ya mwaka kulikuwa na rais mkomunist (Jaruzelski) na PM wa Solidarity.

Baada ya kuona sasa wako tayari kuongoza, mwishoni mwa mwaka 1990 wakaitisha uchaguzi wa rais na Walesa akachaguliwa kuwa rais kwa miaka mitano.

Mwaka 1995, Walesa akapoteza urais na chama cha Kikomunist kikiwa chini ya jina jipya kikachukua urais na kuongoza kwa miaka kumi.

Transition nzuri ya Poland inasemekana ilikuja kutokana na washauri wa Walesa kumwambia asichukue madaraka kwanza. Ile space ya mwaka mmoja ilitumika kujiandaa na pia kuhakikisha hasira na chuki za kutaka kufanya revenge vinapungua kwanza.

Huo ndio mtiririko wa mambo ulivyokuwa kwa Poland.
 
Balali also is talented academic turned
very respected world wide, a man made significat changes to some countries .
Balali as a senior expert with permanent employement on IMF desk but sadly enough brought tragedy to tanzanians .
Mimi naomba niulize mbona msomi akitokea CCM haitwi kichwa .??? ila akitokea upinzani kwa kazi zile zile elimu ile ile shule ile ile anaitwa kichwa???

Mkuuu Mkamap,

Heshima mbele, very strong analysis mkuu na saafi sana! Ndiyo elimu yenyewe tunayokuja kuichota bure hapa JF, ingawa bado safari ni ndefu sana!
 
mbona haisemwi kwamba baada ya kutoka kumshauri mwinyi
lipumba alikuwa mshauri wa uchumi wa museveni na uchumi wa uganda ukapaa? sasa kwa nini uganda afanikiwe na bongo ashindwe?
nadhani tatizo limeelezwa hapo juu.

Eti uchumi wa Uganda ulipaaa? Lini hiyo mkuu mbona wa-Ganda wanatusumbua na wizi wa Ng'ombe zetu mpaka sasa tunataka kufunga mpaka?
 
Eti uchumi wa Uganda ulipaaa? Lini hiyo mkuu mbona wa-Ganda wanatusumbua na wizi wa Ng'ombe zetu mpaka sasa tunataka kufunga mpaka?

FMES,

Hata mimi naona hii ya Uganda ni myth, labda ni kama watu wa West wanavyosifia kupaa kwa uchumi wa TZ, huku maskini wanazidi kuongezeka.
 
Eti uchumi wa Uganda ulipaaa? Lini hiyo mkuu mbona wa-Ganda wanatusumbua na wizi wa Ng'ombe zetu mpaka sasa tunataka kufunga mpaka?

kwani mkuu ukiibiwa ng'ombe ndio inakataa kukua kwa uchumi wa nchi?
uchumi waweza kukua ila mgawanowa pato la nchi usiwafikie wanachi aka ukafisadiwa, lakini haimaanishi uchumi haukufanya vizuri.
 
Back
Top Bottom