Lipumba atua Dar kwa kishindo!

kanda2

JF-Expert Member
Apr 22, 2007
1,318
1,225
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba, amerejea leo jijini Dar na kupokelewa kwa maandamano makubwa ya washabiki, wananachama na wakazi wa jiji kwa ujumla.

Umati wa watu ulisababisha barabara nyingi kufungwa ili kupisha maandamano hayo yaliyoishia viwanja vya Jangwani ambapo Prof Lipumba alihutubia wananchi.

Profesa Lipumba ambae kwa sasa anafanyakazi ya mkataba wa mwaka mmoja na UN anatazamiwa kukaa nchini kwa miezi mitatu kabla ya kwenda kumalizia ngwe ya mwisho ya mkataba wake.

Wapenzi na washabiki wa CUF walikumbwa na kiwewe kama wamepagawa walikuwa wakiimba na kumsifu Lipumba na kukejeli CCM hususan upotevu wa mabilioni ya pesa BOT.

Wananchi wengi wanaamini Lipumba na CUF wana nafasi kubwa ya kuiangusha CCM uchaguzi ujao kutokana na msimamo usioyumba wa viongozi wa juu wa CUF.
 
Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
0
Kanda2, tunashkuru kutuwekea hili..maana ya Chadema hua yanaletwa rasmi na MJKK na si tena Zitto wala Bwana Mdogo wa Ubungo..Bwana Mnyika

Wapinzani walitakiwa kuonesha wako pamoja ktk Hili, maana nakumbuka, nashangaa kuona wapinzani wanashindwa hata kuweka thread ya maandamano hayo.

Tunaomba wale waliopo DSM watuletee PICHA tuone hali ilikuwaje... Mpinzani yoyote aliyepo DSM atuletee data.Sie wengine tupo Bumbuli huku tukitwanga kupitia Dish.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,657
0
Wananchi wengi wanaamini Lipumba na CUF wana nafasi kubwa ya kuiangusha CCM uchaguzi ujao kutokana na msimamo usioyumba wa viongozi wa juu wa CUF.

Ukishangaa ya Akwilombe, basi utayakuta ya Hizza, kama sio ya Kaburu, hivi Lipumba kwenda huko UN si alipewa na CCM ili aje awashinde kwenye uchaguzi wa rais, are you kidding me?

Lipumba a threat wa CCM? Labda wangesema Balali!
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
2,000
Waungwana,

Hivi hayo maandamano ya nini? Mtu katoka kufanya kazi zake na kulipwa vizuri, anarudi nyumbani na kupokewa na maandamano makubwa? Labda nielewesheni, where are our priorities? Huu muda wa kushinda airport kupokea na kusindikiza wanasiasa tunaufidia vipi?

Inabidi vyama vya upinzani vianze kuwa na mawazo tofauti na CCM. Inaelekea mnakopi kila wanachofanya CCM. Kupongezana, kuandamana hata pasipo na maana wala umuhimu wowote.

Kwanini tusianze kwa kuonyesha mifano? Hakuna kupoteza muda kupokea viongozi, hakuna kutumia mashangingi, hakuna VIP lounge hata kwa safari za binafsi nk.

Hii mentality ya ukubwa na kutukuzwa ndio inatengeneza watu kama akina Mugabe, Kibaki na mafisadi wengine, hawataki kuachia utamu wa kupewa shikamoo hata kama shikamoo hiyo ni ya kebehi.

Labda vijana muanze kufikiri tofauti na kuachana na mambo ya kukuzwa na kutukuzwa. Vinginevyo tutaendelea mambo yale, siasa zile zile, watu wale wale, huku wananchi wanazidi kutumbukia kwenye maskini na kazi zao ni kusukuma magari ya wanasiasa.
 
DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,929
1,500
Wananchi wengi wanaamini Lipumba na CUF wana nafasi kubwa ya kuiangusha CCM uchaguzi ujao kutokana na msimamo usioyumba wa viongozi wa juu wa CUF.

..hawa wananchi wengi ni wa nchi gani? hii tanganyika au hiyo zanzibar?

..hivi msimamo wa viongozi wa ccm juu ya kushinda uchaguzi ushawahi kuyumba?

..ni jinsi ninavyoyaona mambo tu! si zaidi!
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,657
0
Mkuu Chuma,

Heshima yako mkuu, unatka nifafanue jinsi Lipumba, alivyo na nafasi kubwa ya kuishinda CCM au kushindwa na kupewa mgawo/Takrima juu?
 
Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
0
Mkuu ES ungefafanua issue ya mgawo au yeye kupewa nafasi UN thru CCM....

Mtanzania siasa ni Hamasa...kama kiongozi lazima hivyo vitu viwepo...na hapo ndio unaweza jua wafuasi wako unao au Huna...Ujuue hiki si kipindi cha kampeni..kupata Mass kubwa namna hii ni kuonesha Mapenzi kwa viongozi na Chama.
Pia Suala la watu kupoteza muda ni comparative term..wengi wanashinda hapa kijiweni JF wanafanya nini na wao? acha UCCM wako..
-Pia Kumbuka Leo Jumapili watu wapo mapumzikoni...

- so Wanachama, wachabiki na serious opposition lazima walikuwa na Hamu na mwenzao...

- au Ulitaka azomewe au kupigwa kama mawazir wa CCM...
 
Chuma,

Kama mawazo yenu ni hayo ndio maana mtaendelea kushindwa na hao CCM. Kama nyie na CCM hakuna tofauti, why make a change?

Hivi tayari umeshanipa UCCM?

Siasa ni sera ndugu yangu na wala sio porojo za bure labda uwe na watu wengi wajinga.

Wewe unaona watu wanashinda JF? Wanaendelea na kazi zao ikiwa ni pamoja na kusoma JF. Hivi Jumapili si afadhali ukae na familia yako kuliko kupoteza muda kwenda kuwapokea wanasiasa airport?

Hayo ndio mambo wanafanya CCM, tumechoka nayo, tunahitaji mabadiliko, lakini naona hata watu kama Lipumba ambao ningetegemea mabadiliko bado mambo ni yale yale.

Uongozi unakuja kwa sera na sio porojo za kwenye vijiwe.
 
Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
2,000
Waungwana,
Hivi hayo maandamano ya nini? Mtu katoka kufanya kazi zake na kulipwa vizuri, anarudi nyumbani na kupokewa na maandamano makubwa? Labda nielewesheni, where are our priorities? Huu muda wa kushinda airport kupokea na kusindikiza wanasiasa tunaufidia vipi?....
Labda vijana muanze kufikiri tofauti na kuachana na mambo ya kukuzwa na kutukuzwa. Vinginevyo tutaendelea mambo yale, siasa zile zile, watu wale wale, huku wananchi wanazidi kutumbukia kwenye maskini na kazi zao ni kusukuma magari ya wanasiasa.

Mtanzania,

Hili lilipangwa siku nyingi kama wiki tatu au nne, nikahoji maana ya kufanya maandamano kupeka mtu anayerudi likizo kutoka kutumikia tajiri mwingine.

Ni ukosefu wa kazi na ubunifu wa itikadi na sera unaofanya vyama vya Upinzani vionekane ni vihiyo kama CCM walivyotaka kuandamana kumpokea Kikwete kupewa Cheti cha Sullivan!
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,657
0
Mkuu ES ungefafanua issue ya mgawo au yeye kupewa nafasi UN thru CCM....

Mkuu Chuma,

Kwanza ni lazima ku-establish iwapo CUF inaongozwa na nani kati ya Seif na Lipumba, na kama goals zao between Visiwani na Bara ziko kwenye the same page, kwa sababu according to the dataz Seif husema in private kuwa hana mpango na bara,

UN asingekwenda bila waliokuwa wanamtaka kupewa okay na CCM, kama vile ambavyo Mama Migiro, asingekwenda UN bila kwanza kukubaliwa na CCM, kama vile ambavyo Marando asingekwenda EAC bila ya Okay ya CCM, na Mzee Masha pia asingekwenda EAC bila ya kukubaliwa na CCM,

By the way Mkuu Chuma, yale mazungumzo ya CUF na CCM yaliiishia wapi?
 
Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
7,953
2,000
..hawa wananchi wengi ni wa nchi gani? hii tanganyika au hiyo zanzibar?
..hivi msimamo wa viongozi wa ccm juu ya kushinda uchaguzi ushawahi kuyumba?

..ni jinsi ninavyoyaona mambo tu! si zaidi!
Zanzibar hakuna viwanja vya Jangwani
 
DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,929
1,500
Mtanzania,

Hili lilipangwa siku nyingi kama wiki tatu au nne, nikahoji maana ya kufanya maandamano kupeka mtu anayerudi likizo kutoka kutumikia tajiri mwingine.

Ni ukosefu wa kazi na ubunifu wa itikadi na sera unaofanya vyama vya Upinzani vionekane ni vihiyo kama CCM walivyotaka kuandamana kumpokea Kikwete kupewa Cheti cha Sullivan!

..rev,

..hao cuf si wajinga,wana lao jambo kufanya hivyo!

..chuma au kanda2 wanaweza tueleza!
 
Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
7,953
2,000
..kwahiyo jangwani ni SI unit ya kupima kuungwa mkono na watu? na si kura?
...Kuungwa mkono itakuwa ni sahihi kabisa, kwani miaka yote Jangwani imekuwa ikijaa watu, lkn inapofika wakati wa kura hakuna kitu, kiasi watu kupiga kelele za kuibiwa kura...
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
2,000
..kwahiyo jangwani ni SI unit ya kupima kuungwa mkono na watu? na si kura?

Tumedumazwa na CCM, ndio maana hata ujinga watu eti wanaandama kuunga mkono.

Kwanini usiunge mkono kwa kuchapa kazi zaidi?

Inabidi wapitie speeches za Obama na waone anavyosisitiza change na kufanya mambo tofauti na politics ambazo watu wamezichoka.

Sisi kila kitu kama CCM, hiyo change itatoka wapi?

Kama ulivyosema kipimo cha umaarufu wa chama sio Machingas wangapi walisukuma gari lako, bali mwaka 2010 utapata kura ngapi.
 
DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,929
1,500
...Kuungwa mkono itakuwa ni sahihi kabisa, kwani miaka yote Jangwani imekuwa ikijaa watu, lkn inapofika wakati wa kura hakuna kitu, kiasi watu kupiga kelele za kuibiwa kura...

..nionavyo mimi huo utakuwa ni ushabiki! kumuunga mkono mtu is to see him/her through! na katika politics ni kumpigia kura!
 
DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,929
1,500
Tumedumazwa na CCM, ndio maana hata ujinga watu eti wanaandama kuunga mkono.

Kwanini usiunge mkono kwa kuchapa kazi zaidi?

Inabidi wapitie speeches za Obama na waone anavyosisitiza change na kufanya mambo tofauti na politics ambazo watu wamezichoka.

Sisi kila kitu kama CCM, hiyo change itatoka wapi?

Kama ulivyosema kipimo cha umaarufu wa chama sio Machingas wangapi walisukuma gari lako, bali mwaka 2010 utapata kura ngapi.

..hebu tusaidie,hii change itatokea wapi? wakina nani wataileta tuwaunge mkono?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom