BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,013
Posted Date::1/29/2008
Lipumba asikitishwa umasikini baada ya kurejea toka Ulaya
Na Muhibu Said
Mwananchi
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema hali ya maisha kwa Watanzania inaendelea kuwa duni tofauti na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete ya kutoa maisha bora kwa kila Mtanzania.
Profesa Lipumba alisema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa, kwenye Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni siku mbili tangu arejee nchini akitokea Uswisi alikokuwa akifanya kazi maalum za Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo(WTO).
Nimerejea nyumbani, nimekuta wananchi bado wako hoi bin taaban, alisema Profesa Lipumba.
Alisema hali hiyo inatokana na kupanda kwa gharama za mahitaji muhimu, kama vile chakula na kusababisha kuongezeka kwa makali ya maisha kutokana na wananchi kushindwa kumudu gharama zake.
Leo ukihitaji unga wa sembe ni Sh700 hadi 1,000 kwa kilo, kila kitu hakigusiki. Yale maisha bora kwa kila Mtanzania yaliyoahidiwa mwaka 2005, yamekuwa kitendawili, alisema Profesa Lipumba.
Alisema wakati Watanzania wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha, nchi imesheheni raslimali mbalimbali, kama vile madini, ardhi, bahari, mabonde ambazo serikali imeshindwa kuweka mipango ya kuzitumia ili kuwakwamua wananchi katika ugumu wa maisha unaowakabili.
Wananchi kwa kweli hawana sababu ya kuwa maskini. Nchi ina dhahabu, almasi. Tuna ardhi kubwa, lakini hatuna mipango. Umeme ambao ni sehemu muhimu katika kuongeza ajira kwa wananchi, haushikiki, alisema Profesa Lipumba.
Alisema mwaka huu, Malawi wanatarajia kuanza kuuza madini ya Urenium ambayo yanapatikana pia Tanzania lakini hayawanufaishi Watanzania.
Profesa Lipumba alisema bei ya dhahabu katika soko la dunia hivi sasa imefikia dola 926 kwa aunsi moja.
Lakini akasema kutokana na mkataba uliopo kati ya serikali ya Tanzania na wawekezaji kwenye sekta ya madini, bei ya dhahabu inauzwa kwa dola 240 nchini, hali ambayo inawanufaisha zaidi wawekezaji kuliko Watanzania.
Mbali na hilo, alisema nchi inakabiliwa na ukosefu wa ajira, kiasi ambacho vijana wanapojaribu kujifanyia biashara ndogondogo ili kujipatia walau mlo mmoja kwa siku, serikali badala ya kuwawekea mazingira mazuri imekuwa ikiwashambulia na kuwanyanganya mali zao.
Ufisadi umekithiri. Yaliyotajwa Benki Kuu ni madogo, sawa na tone la barafu katika bahari, alisema Profesa Lipumba.
Alisema huku Watanzania wakikosa mikopo kwa ajili ya kukabiliana na hali ngumu ya maisha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imetumia mabilioni ya shilingi za walipakodi kujenga minara pacha ambayo gharama zake hazijawahi tumiwa na nchi tajiri kama Marekani na Uingereza.
Wakati huo huo, Profesa Lipumba amelaani hatua ya Mwakilishi wa Jimbo la Mkanyageni (CUF), Haji Faki kusimamishwa kazi za ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa muda wa siku 21, kuanzia juzi baada ya kukataa ama kuthibitisha au kuomba radhi kutokana na kauli yake kuwa mfanyabiashara wa kampuni ya Bopar Enterprises.