Lipumba asikitishwa umasikini baada ya kurejea toka Ulaya

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Posted Date::1/29/2008
Lipumba asikitishwa umasikini baada ya kurejea toka Ulaya
Na Muhibu Said
Mwananchi

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema hali ya maisha kwa Watanzania inaendelea kuwa duni tofauti na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete ya kutoa maisha bora kwa kila Mtanzania.

Profesa Lipumba alisema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa, kwenye Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni siku mbili tangu arejee nchini akitokea Uswisi alikokuwa akifanya kazi maalum za Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo(WTO).

“Nimerejea nyumbani, nimekuta wananchi bado wako hoi bin taaban,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema hali hiyo inatokana na kupanda kwa gharama za mahitaji muhimu, kama vile chakula na kusababisha kuongezeka kwa makali ya maisha kutokana na wananchi kushindwa kumudu gharama zake.

“Leo ukihitaji unga wa sembe ni Sh700 hadi 1,000 kwa kilo, kila kitu hakigusiki. Yale maisha bora kwa kila Mtanzania yaliyoahidiwa mwaka 2005, yamekuwa kitendawili,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema wakati Watanzania wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha, nchi imesheheni raslimali mbalimbali, kama vile madini, ardhi, bahari, mabonde ambazo serikali imeshindwa kuweka mipango ya kuzitumia ili kuwakwamua wananchi katika ugumu wa maisha unaowakabili.

“Wananchi kwa kweli hawana sababu ya kuwa maskini. Nchi ina dhahabu, almasi. Tuna ardhi kubwa, lakini hatuna mipango. Umeme ambao ni sehemu muhimu katika kuongeza ajira kwa wananchi, haushikiki,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema mwaka huu, Malawi wanatarajia kuanza kuuza madini ya Urenium ambayo yanapatikana pia Tanzania lakini hayawanufaishi Watanzania.

Profesa Lipumba alisema bei ya dhahabu katika soko la dunia hivi sasa imefikia dola 926 kwa ‘aunsi’ moja.

Lakini akasema kutokana na mkataba uliopo kati ya serikali ya Tanzania na wawekezaji kwenye sekta ya madini, bei ya dhahabu inauzwa kwa dola 240 nchini, hali ambayo inawanufaisha zaidi wawekezaji kuliko Watanzania.

Mbali na hilo, alisema nchi inakabiliwa na ukosefu wa ajira, kiasi ambacho vijana wanapojaribu kujifanyia biashara ndogondogo ili kujipatia walau mlo mmoja kwa siku, serikali badala ya kuwawekea mazingira mazuri imekuwa ikiwashambulia na kuwanyang’anya mali zao.

“Ufisadi umekithiri. Yaliyotajwa Benki Kuu ni madogo, sawa na tone la barafu katika bahari,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema huku Watanzania wakikosa mikopo kwa ajili ya kukabiliana na hali ngumu ya maisha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imetumia mabilioni ya shilingi za walipakodi kujenga minara pacha ambayo gharama zake hazijawahi tumiwa na nchi tajiri kama Marekani na Uingereza.

Wakati huo huo, Profesa Lipumba amelaani hatua ya Mwakilishi wa Jimbo la Mkanyageni (CUF), Haji Faki kusimamishwa kazi za ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa muda wa siku 21, kuanzia juzi baada ya kukataa ama kuthibitisha au kuomba radhi kutokana na kauli yake kuwa mfanyabiashara wa kampuni ya Bopar Enterprises.
 
Huyu naye ni msanii tuu,yaani anakuja tuu ikiwa karibu na kuchukua form ya uraisi,bora hata kina Dr Slaa na Zitto wanafanya kitu kinaeleweka na ninaweza kuwaita wapinzani wa kweli,lakini huyu ni story tuu hana mpya na wala sera yeyote..he's just a big talk and do nothing!
 
bora hata kina Dr Slaa na Zitto wanafanya kitu kinaeleweka na ninaweza kuwaita wapinzani wa kweli,lakini huyu ni story tuu hana mpya na wala sera yeyote..he's just a big talk and do nothing!

Mkuu Koba,

Heshima mbele mkuu, hayo ndio exactly maneno yangu mkuu toka juzi, ahsante kwa kuyarudia na kuyaweka sawa zaidi, that is exactly how I feel!
 
Lakini jamani kama hawa jamaa wanalipa kodi ya dhahabu kwa mkataba wa bei ya 240$ wakati sasa hivi bei ni zaidi ya 900$...kweli kuna haja ya kuangalia akili za wote waliotuingiza katika hiyo mikataba,yaani tumeibiwa mpaka unabaki kucheka tuu badala ya kulia.
 
Mkuu Koba,

Heshima mbele mkuu, hayo ndio exactly maneno yangu mkuu toka juzi, ahsante kwa kuyarudia na kuyaweka sawa zaidi, that is exactly how I feel!

...mku huyu jamaa tangu 1995 kazi yake ni kuchukua form tuu ya uraisi,halafu sasa hivi anakuja kutaka kujitafutia sifa kuongelea migodi wakati kina Zitto walishachafuliwa mpaka kufukuzwa bungeni na tulikuwa hata hatujui yuko wapi na hata kusema chochote hakusema,huyu bora aende kwao tabora akagombee ubunge asaidie maendeleo lakini kwenye National politics is just a big failure na si chochote si lolote.
 
"Nimerejea nyumbani, nimekuta wananchi bado wako hoi bin taaban," alisema Profesa Lipumba.

Sasa yeye kweli alitegemea kwa huo muda aliokaa ulaya angerudi kukuta umasikini umekwisha Tanzania?

Kwa mwendo huu upinzani Tanzania sijui...
 
Ufisadi umekithiri. Yaliyotajwa Benki Kuu ni madogo, sawa na tone la barafu katika bahari," alisema Profesa Lipumba.
Najaribu kutafakari hii sentensi
1. Kwamba (BOT)ni kitu kidogo mno ambacho ukilinganisha na ufisadi uliokuwepo (kwa ujumla)
2.Kwamba with no time kitayeyuka na kuacha bahari kama ilivyo.
 
Mimi nilivyosoma kichwa cha hii habari mara ya kwanza sikutaka kuendelea, nilijua ni udaku.

Hivi kweli Prof. Lipumba anaweza kudhani umaskini ungepungua kwa hiyo miezi sita aliyokaa Ulaya?

I am willing to give him the benefit of the doubt on this one. I hope he was misquoted.
 
Huyu naye ni msanii tuu,yaani anakuja tuu ikiwa karibu na kuchukua form ya uraisi,bora hata kina Dr Slaa na Zitto wanafanya kitu kinaeleweka na ninaweza kuwaita wapinzani wa kweli,lakini huyu ni story tuu hana mpya na wala sera yeyote..he's just a big talk and do nothing!

Hivi form za urais karibu zitatoka eeh? some-one help me!
 
Wakuu sjawahi kucheka lakini nimecheka sana na hii thread! Yaani jamaa katoka kwenye winter kakuta joto Dar, vumbi, njaa anashtuka? sasa afadhali yake yeye ni Profesa na mtu wa matawi ya juu...apige picha huko vingunguti na Kwembe...wanaotoka posta kwenye dala dala wamesimama..na foleni ya masaa matatu kufika Ubungo...kwa kweli bongo hatufi ila cha moto tunakipata!!Huyu jamaa alete utalaamu wake basi tusaidiane kuikomboa nchi? tuwawajibishe hawa mafisadi...
 
Mimi nilivyosoma kichwa cha hii habari mara ya kwanza sikutaka kuendelea, nilijua ni udaku.

Hivi kweli Prof. Lipumba anaweza kudhani umaskini ungepungua kwa hiyo miezi sita aliyokaa Ulaya?

I am willing to give him the benefit of the doubt on this one. I hope he was misquoted.

Mtanzania,

Im equally givig u benefit of doubt on this one. Some-one must b using ur password.

Alichofanya Lipumba ni kulinganisha kauli mbiu ya CCM wakati wa kumnadi mgombea na hali halisi on the ground kwa sasa. Sijaona mahala kwenye story hiyo Lipumba anasema assessment yake ina based on "miezi sita" na hauitaji calculus kujua safari ya kilometa 1000 inaanza na hatua moja. Sasa baada miaka miwili ya kauli mbiunmaisha bora kwa kila mtanzania tungetegemea walau ka-hatua kamoja nadhani by inference a learned Prof ana maanisha hivyo.

...mku huyu jamaa tangu 1995 kazi yake ni kuchukua form tuu ya uraisi,halafu sasa hivi anakuja kutaka kujitafutia sifa kuongelea migodi wakati kina Zitto walishachafuliwa mpaka kufukuzwa bungeni na tulikuwa hata hatujui yuko wapi na hata kusema chochote hakusema,huyu bora aende kwao tabora akagombee ubunge asaidie maendeleo lakini kwenye National politics is just a big failure na si chochote si lolote.

Mkuu huyu jamaa ana haki kama raia yeyote yule kugombea kwa mujibu wa sheria za nchi, ni failure well ma-failure ni sisi wananchi ambao toka 2000 tumekuwa tunampa kura mpaka anashika nafasi ya pili even wetu Mwenyekiti Mbowe was squarely beaten in the last general election.

Unadai wakina Zitto ndio wamechafuliwa na kufukuzwa bungeni na yeye anakuja kutafuta sifa, kufukuzwa bungeni na kupigwa mpaka kuvunjwa mkono na kuwekwa ndani na kufunguliwa kesi kupi ni "kuchafuliwa" sana. Zitto alichoafanya kwa taarifa yako ni kile kilicho balikiwa na umoja wa ushindani bungeni kama team work ambao kiongozi wake ni Mh Hamad Rashid lakini kama kawaida mna spin ionekana Chadema tu. What about Mwenyekiti wetu aliekuja kugundua umuhimu wa shule uzeeni kule HULL alipo akija na kuchukua form hatakuwa anajitafutia sifa? Mbona huku watu "wanachafuliwa" ilhali yeye yupo UK.

Lakini jamani kama hawa jamaa wanalipa kodi ya dhahabu kwa mkataba wa bei ya 240$ wakati sasa hivi bei ni zaidi ya 900$...kweli kuna haja ya kuangalia akili za wote waliotuingiza katika hiyo mikataba,yaani tumeibiwa mpaka unabaki kucheka tuu badala ya kulia.

Koba,

What a u turn! sasa hayo ungeyajua kama Prof Lipumba asingekuja kwenye "winter break" where is Zitto aliepo on the ground? mbona hajatuambia haya?

Huyu naye ni msanii tuu,yaani anakuja tuu ikiwa karibu na kuchukua form ya uraisi,bora hata kina Dr Slaa na Zitto wanafanya kitu kinaeleweka na ninaweza kuwaita wapinzani wa kweli,lakini huyu ni story tuu hana mpya na wala sera yeyote..he's just a big talk and do nothing
!

Well that summarizes everything...
 
Hivi kweli Prof. Lipumba anaweza kudhani umaskini ungepungua kwa hiyo miezi sita aliyokaa Ulaya?

Achilia mbali miezi sita, mabadiliko yanayotokea ndani ya mwezi mmoja tu au hata chini yake yanaweza kuwa na madhara makubwa sana kwa wananchi.
 
Wakuu sjawahi kucheka lakini nimecheka sana na hii thread! Yaani jamaa katoka kwenye winter kakuta joto Dar, vumbi, njaa anashtuka? sasa afadhali yake yeye ni Profesa na mtu wa matawi ya juu...apige picha huko vingunguti na Kwembe...wanaotoka posta kwenye dala dala wamesimama..na foleni ya masaa matatu kufika Ubungo...kwa kweli bongo hatufi ila cha moto tunakipata!!Huyu jamaa alete utalaamu wake basi tusaidiane kuikomboa nchi? tuwawajibishe hawa mafisadi...

Masanja,

Umenikumbusha jambo moja ambalo lilinotokea mimi. Nilipofika Europe safari ya kwanza nilikuwa bado naiona Tanzania babu kubwa. Hiyo ni miaka ya 90. Baada ya miaka minne nilirudi TZ likizo, yaani sikuamini, ilikuwa utafikiri nimeshushwa sijui wapi. Mimi mwenyewe nilikuwa shocked, Dar iliyokuwa kichwani ilikuwa tofauti sana na niliyokuwa naiona.

Kwasasa kila nikirudi sipatwi na hiyo shock tena. Hilo tatizo hata Wakenya waliniambia linawakumba, walikuwa wanaona nchi yao babu kubwa sana na kututambia wengine. Waliporudi likizo na wengine wakapita na Dar, wakaja ni watu wamebadilika na kuanza kusagia Nairobi.

Prof. Lipumba ametoka nje mara nyingi, sitegemei na yeye akumbwe na kaugonjwa ambako kalitupata wengine tuliporudi nyumbani mara ya kwanza.
 
Achilia mbali miezi sita, mabadiliko yanayotokea ndani ya mwezi mmoja tu au hata chini yake yanaweza kuwa na madhara makubwa sana kwa wananchi.

Nungunungu,

Unaweza kuiharibu TZ kwa mwezi mmoja, kama tunavyoona Kenya, lakini huwezi kubadili maisha ya wananchi na nchi kwa ujumla kwa miezi sita.
 
Huku ndiko kubwabwaja au Mbweko usio na Mbwa. Sikutegemea kama maneno haya yanatoka kinywani mwa Prof. wa Uchumi. Anasikitika, kwani alifikiri akirudi toka Ulaya angekuta umasikini wa WaTZ umeisha? Kwa sera zipi?

Huu ndio uzandiki, hii kauli naifananisha na ya JK aliposema Hajui Umasikini wa WaTZ unatokana na nini. Umasikini wa Tanzania hauwezi kuisha kwa siku moja hata kama yeye atapewa nchi leo. Is a long process. Ni lazima kuweka misingi ya ukuaji wa uchumi kuanzia ngazi ya Familia hadi taifa kwa ujumla, kusimamia vyema rasilimali zetu zote akiwemo yeye lipumba na waTZ wote. Siasa safi na maadili bora.

Nyerere alijitahidi sana katika hili lakini tumekosa wa kuliendeleza. Tuna watu wenye uchu wa kwenda ikulu na kauli za ajabu.

Unasikitika!!! Then after? Ukishamaliza kusikitika ndo majibu ya umasikini wetu? Muwe mnachuja kidogo kaulizi zenu
 
jamaa yuko zake mbele kimyaaaa! Akitua utamsikia na analysis zake za uchumi! We dont want leaders like this! This time badili nyimbo mkuu tumekuwahi!
 
yeye alikuwa wapi asisaidiane na wenzake kina slaa na wenzie kuwafichua mafisadi wanaotafuna nchi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom