Lipi kweli kuhusu pombe kali? Valeur, konyagi n.k | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipi kweli kuhusu pombe kali? Valeur, konyagi n.k

Discussion in 'JF Doctor' started by ze encyclopedia, Nov 22, 2011.

 1. ze encyclopedia

  ze encyclopedia JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 271
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  msaada tutani, wengine wanasema ukinywa pombe kali unakuwa strongly erect, lakn madaktar wanasema pombe inaua nguvu za kiume? Lipi la ukweli
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wenye uwelewa watakuja maana hata wengine tunahitaji majibu.
   
 3. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye nyekundu ndio jibu linatoka, wewe unamwamini nani kati ya hao? "Daktari" ni mtaalamu wa tiba, sina uhakika na hao "Wengine" wao ni wataalamu wa nini?
   
 4. kinyoba

  kinyoba JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 1,238
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ni kweli hiyo pombe kali Kama konyagi inasaidia na madaktari wanasema ukizidisha ndo inakuharibu badala ya kukusaidia. The same to other types of pombez!
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Na kwa nini at first place umeuliza hili swali
  Unataka ukalianzishe na wewe
  Au ushaona wadudu hawapandi vyema
   
 6. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Dah....kumbe huyu mheshimiwa ndio kajiunga! Wataalamu msaidieni nadhan kuna jambo linamsibu

   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Na visisimua mwili vingine.
   
 8. v

  valid statement JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  valuer 2 na nusu ishanitendaga mno, asubuhi najiuliza nilifikaje nyumbani? Kamkweche kangu hakana hata mchubuko, nkasema, hii product noma! Inafuta memory!
   
 9. S

  Shedrack msechu New Member

  #9
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nalofikiri hilo la kwanza(strongly erect)sbabu hata ss tumewaona. Kuhusu nguvu za kiume pia nitatizo ht ww unajua ukilewa hufikiri kabisa wala hupati mihemko
   
 10. ze encyclopedia

  ze encyclopedia JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 271
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mi naitaji kufahamu tuuu jamani, upya wangu ktk kurasa hizi isiwe sabb. Kwan huwa nackia tu . Hapana tatizo lingine nan mimi siendi pombe kabsaaaaaaaaa
   
 11. B

  Bayo Senior Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukipiga pombe kali unakua strong kwa muda huo kiukweli ila wanasema in long run inakuathiri na kupunguza hizo nguvu
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Pombe ina magonjwa 60 kwa binadamu

  MOJA ya vyanzo vinavyolipatia taifa mapato kupitia makusanyo ya kodi ni pombe.
  Lakini pamoja na faida zote tunazozipata, ukweli unabaki palepale kwamba pombe ina athari katika maisha ya binadamu.

  Mwanzoni mwa mwaka huu wataalamu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na madaktari wastaafu walikutana na wanahabari jijini Dar es Salaam na kuzungumzia juu ya mkutano utakaozungumzia athari za pombe katika jamii.

  Mkutano huo unaotarajia kufanyika Jan 13 hadi 14 mwaka huu mkoani Arusha, utashirikisha nchi za Afrika Mashariki.
  Watunga sheria na wataalamu wengine kutoka serikalini watahudhuria huku ujumbe wa mkutano huo ni: ‘Kilevi si bidhaa ya kawaida na ni kikwazo katika maendeleo.’

  Mkurugenzi Msaidizi na Katibu wa Magonjwa yasiyoambukiza, Dk. Joseph Mbatia, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anasema serikali ipo mbioni kutengeneza sera itakayohusu utumiaji wa pombe ili kupunguza athari zake katika jamii.

  Dk. Mbatia anasema wamelazimika kutunga sera hizo baada ya kuona matatizo yanayotokana na pombe yanaongezeka kila kukicha.
  Anasema kabla ya sera hizo kupitishwa watafanya utafiti katika maeneo mbalimbali ili

  kujua ni jinsi gani jamii inavyolichukulia suala la pombe na madhara yake.
  “Mfano, katika vijiji vichache tulivyofanya utafiti, wananchi walikuwa wakijitetea kwamba pombe imewasaidia kuendesha maisha yao…lakini ukweli ni kwamba pamoja na faida ambazo zimekuwa zikiorodheshwa, hasara ni nyingi kuliko faida.

  “Kwa mfano, bima zimekuwa zikilipwa kutokana na ajali zinazosababishwa na kulewa kupita kiasi,” anasema Dk. Mbatia.
  Anabainisha kwamba sera zitakazowekwa si katika kupiga vita biashara ya pombe na badala yake zitakuwa zikiangalia njia bora za matumizi yake na kwa wale wataoonekana

  wameshaathirika watawekewa utaratibu wa kupatiwa tiba.
  Kwa upande wake Mwakilishi wa Kanda ya Afrika Mashariki ya ‘IOGT-NTO Movement’, ambao ni waandaaji wa mkutano huo, Gunnar Lundstrom, anasema bado kuna

  changamoto zinazolikabili taifa katika kupunguza athari za pombe.
  Anasema changamoto hizo ni pamoja na pombe kupatikana kwa gharama nafuu na hivyo kusababisha watu kunywa kupindukia.

  Tatizo lingine anasema ni pombe kuwa moja ya chanzo cha mapato nchini, jambo linalofanya serikali kushindwa kupiga marufuku.
  Naye Daktari mstaafu, Maletnlema Tumsifu, anasema kuna jumla ya magonjwa 60

  yanayosababishwa na unywaji wa pombe.
  Anataja baadhi ya magonjwa hayo kuwa ni mfarakano katika familia, maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, unene kupita kiasi, utapiamlo hasi, mimba kuharibika na kisukari.

  Dk. Maletnlema anasema kuna madhara ya pombe ya aina mbili. Kwanza ni kuathirika kwaa mishipa ya fahamu mwilini kote kwa kupunguzwa uwezo na pili ni kuungua baadhi ya ogani za mwili hasa tumbo pindi mtu anapokunywa.

  Anaeleza kwamba katika kuathirika mishipa ya fahamu kumetizamwa kwa hatua nne za wanywaji, hatua ya kwanza ni ile ya kuchangamka.
  Hapa mtu hujisikia mzima zaidi ya kawaida, moyo unapiga haraka, tumbo linameng’enya chakula haraka na hamu ya chakula kuongezeka.

  Hatua ya pili, mtu akiendelea kunywa anachanganyikiwa na kuzungumza sana, kukosa aibu, utu kubadilika, kutawala tabia za kimwili, hamu ya chakula kuongezeka na hapa ndipo watu wanaagiza nyama choma kwa wingi.

  Mnywaji akiendelea kunywa pombe hucharuka kutokana na neva zake za ubongo kushindwa kumiliki mwili.
  Mambo yote anayoyafanya hayana utaratibu kwani mnywaji huwa mkorofi.
  Dk. huyo anasema mnywaji huwa mkorofi na anaongea maneno yasiyo na maana, baadhi

  ya wanywaji huchukulia hatua hii kama raha yao. Hapa kitu kinachojitokeza ni kupoteza hamu ya kula.
  Hatua ya nne mtu akilewa kupita kiasi huwa hajijui na analala fofofo kutokana na

  kupoteza fahamu. Huenda akajikojolea au kutapika, inategemea na kiasi cha pombe alichokunywa.
  Wakati kwa upande wa ogani, pombe huathiri zaidi viungo vinavyopata pombe nyingi kila wakati mtu akiwa anakunywa.

  Mfano wa viungo hivyo ni mdomo, koo na tumbo, ambavyo vyenyewe hufikiwa na pombe nyingi mara mtu anapomeza.
  Tumbo likiumia inaonekana kama maumivu ya tumbo, pengine kutapika na kuharisha.

  kutokana na utaratibu wa tumboni, lazima chakula chote pamoja na sumu au madawa vinavyonyonywa tumboni vipitie katika ini kuondoa sumu na vyakula visivyohitajika.
  Na kwa sababu hii, pombe yote mtu anayokunywa hupita katika seli za ini na zinajaribu kuiondoa lakini nazo zinalewa chakari na baadhi zina kufa.
  • Ieleweke kwamba tukinywa kidogo seli chache zinakufa na tukinywa sana zinakufa seli nyingi na nafasi yake inajazwa nyuzi nyuzi za kovu. Ini huwa na mabilioni ya seli ambazo ni imara, hata mtu akinywa pombe nusu, seli zake bado zitaendelea na maisha kama inafikia kikomo ini linashindwa kufanya kazi na kujikuta njia za nyongo na mishipa ya damu inaziba. Kila ogani ya mwili inaumia kivyake, lakini tumbo na ini ni mifano wazi.
  Chanzo: https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/80412-pombe-ina-magonjwa-60-kwa-binadamu.html
   
Loading...