LinkedIn na Wabongo, Tujitathmini

LinkedIn na Wabongo, Tujitathmini

LinkedIn si neno geni kwa wengi wetu, huu ni mtandao wa kijamii wa wataalamu, Professionals ambapo kila mtu ambaye yuko interested huweka Profile yake, hii hubeba Elimu, Kazi ulizowahi kufanya, na mambo mengine kama hayo.
Ni mtandao ambao hukutanisha watu wa aina mbali mbali lakini wakati huo huo ikitoa fursa za ajira kwa watu mbali mbali.

Recruiting Agencies, International Organizations, na Companies nyingi sana hutumia mtandao kutafuta Potential Candidates lakini wakati huo huo hata Job hunters ni fursa nzuri kutafuta kazi pia.

Kwa Tanzania nimekutana na changamaoto moja kubwa sana, hatujui kujiuza (kujieleza), ukifungua Profile ya BAADHI ya Vijana wa hapa Nyumbani utakuta kaandika vitu vya ajabu kweli, kumbukeni Profile yako inasomwa na dunia nzima, kuna mashirika mbali mbali ambayo yangependa kuja kuwekeza Tanzania na hivyo hua mara nyingi hukumbilia LinkedIn, imagine wanakuta umesomea kitu wanachokitaka na uzoefu unao lakini kujieleza kule kwa Lugha ile kunakuangusha, huwezi sogea.

Tuchukulie changamoto hii ya kujieleza kama ndio point yetu ya kutoka, ni wazi kuwa wengi tumefanikiwa kwa kupitia LinkedIn, usbaki nyuma.Kule sio Facebook au Twitter pale unakwenda kujiuza ili ujipime una soko kiasi gani kwenye dunia, kama unakosa hata call moja kwa watu uliomba kufanya kazi kwao, basi rudi kaangalie ulichokiandika.

Tukiweka profile ya mtu hapa kutoka LinkedIn utashangaa, nadhani kama unashindwa kuandika vizuri basi hata copy kwa mtu mwingine halafu badilisha ilete maana kidogo. Kumbuka LinkedIn unaweza kutengeneza na kuprint CV moja kwa moja, na ni acceptable Worldwide
Nakumbuka nilipata kazi ya consultation ya wiki moja nikalamba 2.6m kupitia linkedin
 
Sio kweli umechanganya madesa.
Linkedin haiwezi kukujua bila kujiunga na kufeed data zako,cv yako.
Labda umeifanananisha na google ndio inaweza kukutambua kwa kuchukua taarifa zako kutoka mitandao mingine
Ninachojua LinkedIn inakusanya taarifa zako zinazokuhusu kutoka sources mbalimbali za mitandao japo unaweza fungua account pia yaani inakusanya taarifa zako za kitaaluma na kiprofesional yenyewe hata kama hujajiunga lengo kuwasaidia watu wanaokutafuta au wanaotaka kukujua zaidi na watu wengi wanaopenda privacy hawaipendi kabisa,
Mfano Mimi sijawai jiunga LinkedIn laki wao wanazo taarifa zangu.
 
Mkuu nakuekea link hapo upitie hio profile,then utaelewa umuhimu wa LinkedIn.Shida watanzania tuko nyuma sana ila watu wanatoboa kupitia huu mtandao
https://www.linkedin.com/in/frank-joel-mbise-a7898526
Mkuu samahani kidogo, Mimi akaunti ya LinkedIn nilikuwa nayo tangu mwaka juzi. Mwaka jana mwezi wa 9 katika kuingia ikagoma kwa kudai nimekosea password na email haviendani.

Nimejaribu Mara kwa Mara, inagoma hata wakinitumia code number kwa email,nikaenda sehemu wanataka Id yangu sijafanikiwa.

Nahitaji msaada wako wewe na bwana Elli Mshana.
 
Duh, pole sana! Hakuna alternative email?? Change password
 
Ishu kwa baadhi ataandika nini na hali yenyewe ya kwetu hapa..

Mtu amemaliza degree ajira ngumu anajiongeza na vibiashara vya hapa na pale.. ataandik nini kiwavutie watu!!?
Mkuu unaandika hata sehemu ulizofanyia fields au internships ili mradi uwe na profile kule.

Lengo ikiwa ni kutengeneza connections na watu,na kingine kule kuna kazi za level mbalimbali zinatangazwa hata za fresh graduates pia zipo.
 
Za hivyo zipo mkuu.. 2020 hii wengi wanafanya hivyo
 
Vipii kwa wajuziii wa forex wapoo hukoo au ni mambo ya kutafutaa ajira tu.

Maana naona wengi ni walioo enda shuleee
 
Ninachojua LinkedIn inakusanya taarifa zako zinazokuhusu kutoka sources mbalimbali za mitandao japo unaweza fungua account pia yaani inakusanya taarifa zako za kitaaluma na kiprofesional yenyewe hata kama hujajiunga lengo kuwasaidia watu wanaokutafuta au wanaotaka kukujua zaidi na watu wengi wanaopenda privacy hawaipendi kabisa,
Mfano Mimi sijawai jiunga LinkedIn laki wao wanazo taarifa zangu.
Hapana, sio kweli tuache upotoshaji.
 
Back
Top Bottom