LinkedIn na Wabongo, Tujitathmini

LinkedIn na Wabongo, Tujitathmini

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
61,387
Reaction score
100,504
LinkedIn si neno geni kwa wengi wetu, huu ni mtandao wa kijamii wa wataalamu, Professionals ambapo kila mtu ambaye yuko interested huweka Profile yake, hii hubeba Elimu, Kazi ulizowahi kufanya, na mambo mengine kama hayo.

Ni mtandao ambao hukutanisha watu wa aina mbali mbali lakini wakati huo huo ikitoa fursa za ajira kwa watu mbali mbali.

Recruiting Agencies, International Organizations, na Companies nyingi sana hutumia mtandao kutafuta Potential Candidates lakini wakati huo huo hata Job hunters ni fursa nzuri kutafuta kazi pia.

Kwa Tanzania nimekutana na changamaoto moja kubwa sana, hatujui kujiuza (kujieleza), ukifungua Profile ya BAADHI ya Vijana wa hapa Nyumbani utakuta kaandika vitu vya ajabu kweli, kumbukeni Profile yako inasomwa na dunia nzima, kuna mashirika mbali mbali ambayo yangependa kuja kuwekeza Tanzania na hivyo hua mara nyingi hukumbilia LinkedIn, imagine wanakuta umesomea kitu wanachokitaka na uzoefu unao lakini kujieleza kule kwa Lugha ile kunakuangusha, huwezi sogea.

Tuchukulie changamoto hii ya kujieleza kama ndio point yetu ya kutoka, ni wazi kuwa wengi tumefanikiwa kwa kupitia LinkedIn, usbaki nyuma.Kule sio Facebook au Twitter pale unakwenda kujiuza ili ujipime una soko kiasi gani kwenye dunia, kama unakosa hata call moja kwa watu uliomba kufanya kazi kwao, basi rudi kaangalie ulichokiandika.

Tukiweka profile ya mtu hapa kutoka LinkedIn utashangaa, nadhani kama unashindwa kuandika vizuri basi hata copy kwa mtu mwingine halafu badilisha ilete maana kidogo. Kumbuka LinkedIn unaweza kutengeneza na kuprint CV moja kwa moja, na ni acceptable Worldwide

linkedIn ni useful platform mimi binafsi inasaidia sana hasa kwenye professional yangu nimejiunga groups nyingi za fani yangu kuna discussions nzuri sana ambazo zimenijenga..
jambo la ujenzi wa CV ni muhimu sana na kujieleza hasa kwa lugha ya kiingereza
pia kama una muda ongeza lugha nyingine kama kijerumani ,kifaransa etc..kuna makumpuni makubwa yanahitaji sana ujuzi tulionao ila tatizo lugha ni changamoto..
Kati ya mitandao ninayoiheshimu linkedIn ni mmoja wapo, nimekutana na wajasiriamali wengi sana, nimejiunga kwenye makundi yenye tija na wengine tumehama toka kwenye makundi ya online na kuingia whattsap.

Ukikaa na wabongo wenzako unajiona wewe ni kichwa na mjanja, ukiingia linkedin utajiona wewe ni mshamba tu.
Na hasa kama dreams zako ni kufanya kazi nje ya nchi,humo kwenye linkedIn ndipo kwenyewe.Nilishapata kazi 2 nje ya nchi kupitia linkedin.Watu wanaweza wasisome CV yako yote, kwa hiyo pale kwenye Career summary ndipo unapotakiwa kumaliza biashara.
 
Asante mkuu,tunataka watu kama wewe ili wapambanaji wanaotaka kujikwamua pamoja na kuathiriwa na sera za divison five, wakwamuke kwa makala kama hizi.

Umesema ukweli,pamoja na kusoma kwetu bado kuandaa cv ni shida.

Hii ni pamoja na kushindwa kujieleza kwa lugha ya kiingereza, Wakipatikana watu kama wewe ni kweli tutatoka.

BIG UP sana.
 
Ok Ok asante na kwako pia, nadhani wengi wetu hatujui kuwa tumehama kwenye dunia ya makaratasi ya barua, tuko kwenye ulimwengu mwingine kabisa
Asante mkuu,tunataka watu kama wewe ili wapambanaji wanaotaka kujikwamua pamoja na kuathiriwa
na sera za divison five,wakwamuke kwa makala kama hizi.
Umesema ukweli,pamoja na kusoma kwetu bado kuandaa cv ni shida.
Hii ni pamoja na kushindwa kujieleza kwa lugha ya kiingereza,
Wakipatikana watu kama wewe ni kweli tutatoka.BIG UP sana.
 
linkedIn ni useful platform mimi binafsi inasaidia sana hasa kwenye professional yangu nimejiunga groups nyingi za fani yangu kuna discussions nzuri sana ambazo zimenijenga..

Jambo la ujenzi wa CV ni muhimu sana na kujieleza hasa kwa lugha ya kiingereza
pia kama una muda ongeza lugha nyingine kama kijerumani ,kifaransa etc..kuna makumpuni makubwa yanahitaji sana ujuzi tulionao ila tatizo lugha ni changamoto..
 
Mpwa nielekeze namna ya kujitangaza kule
halafu umesema kuwa utaweka cv yakule linkedin weka basi
ok ok asante na kwako pia, nadhani wengi wetu hatujui kuwa tumehama kwenye dunia ya makaratasi ya barua, tuko kwenye ulimwengu mwingine kabisa
 
Kati ya mitandao ninayoiheshimu linkedIn ni mmoja wapo, nimekutana na wajasiriamali wengi sana, nimejiunga kwenye makundi yenye tija na wengine tumehama toka kwenye makundi ya online na kuingia whattsap.

Ukikaa na wabongo wenzako unajiona wewe ni kichwa na mjanja, ukiingia linkedin utajiona wewe ni mshamba tu.
 
Mpwa nielekeze namna ya kujitangaza kule
halafu umesema kuwa utaweka cv yakule linkedin weka basi
Mpwa wangu, the way inavyofanya kazi sioni kama ni tofauti sana na mitandao mingine, na unaweza ku-sign up kwa kutumia email yoyote, kwahio ukishajiunga nao utakuwa na uwezo wa kupost kile kitu unachotaka but it should be something meaningful ambacho kina sound ki-professional. Kwa mfano najua wewe ni MC, Mpambaji na vitu vya namna hio unaweza kupost pale na details zako.

Nilipost mfano wa CV fulani ila naona Mods wameiondoa, wako sahihi kufanya hivyo. Nadhani kuiingia kule utapata mawili matatu, au ukishaweka taarifa zako ndio unaweza kuprint CV kwa LinkedIn ukapata CV nzuri sana. Ni hayo tu Mpwa wangu tukutane LinkedIn ila kule hakuna kutumia fake ID
 
Msaada tafadhali wa namna ya kujiunga na kuupload hizo details mkuu. Asante kwa kuniamsha kutoka usingizini. Be blessed!

Mpwa wangu kwa simu za Android/ windows na nyingine hio iko kama Apps nyingine za Social, ukifika pale utaipata tu labda hapa nimuombe Invisible paje juu kwenye post yangu aniwekee ICON ya LinkedIn ili watu waelewe wanapokuwa wanatafuta apps za ku-download kwenye simu zao iwe rahisi kuelewa tunachoongea.

https://www.linkedin.com
 
Last edited by a moderator:
Kati ya mitandao ninayoiheshimu linkedIn ni mmoja wapo, nimekutana na wajasiriamali wengi sana, nimejiunga kwenye makundi yenye tija na wengine tumehama toka kwenye makundi ya online na kuingia whattsap.

Ukikaa na wabongo wenzako unajiona wewe ni kichwa na mjanja, ukiingia linkedin utajiona wewe ni mshamba tu.
Mpwa hapo umenichosha hahahahahhahaaaa unaona watu walivyokuwa na CV za ajabu ajabu eeeh, halafu unaingia mtu unajifanya mjanjaaaaa kumbe Lol
 
asante mpwa kunijuza nitafuatilia ushauri huu na kuufanyia kazi
nitakutafuta kule mpwa usijali ila sitajua unatumia jina gani kule?
Elli
 
Last edited by a moderator:
2Q==
 
Back
Top Bottom