Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,086
- 6,568
Marehemu Hugo Chavez alikuwa kiongozi anayefaa na kama hapa Tanzania tungekuwa na kiongozi kama Hugo Chavez tungefurahia kuwa Watanzania.
Leo hii hili taifa lina kila aina ya rasilimali ambazo kama tungekuwa na kiongozi makini basi tusingesikia wananchi wanapata tabu. Leo hii wananchi wanahangaika kupata huduma za afya, elimu,maji na huduma nyingi za msingi.
Kama tumejitahidi awamu hii kudhibiti rushwa na ubadhirifu na kisha fedha zilizokuwa zinapotea zinaenda mikononi mwa serikali. Mbona huduma za afya zipo duni? Mbona wananchi masikini wanahangaika kulipishwa kupata huduma za afya? Kwa nini shule hazina madarasa? Wanafunzi wanafunzi wanakaa chini!
Kwa nini tukomae kujenga madaraja kama Busisi na Oysterbay wakati huduma za msingi kwa wananchi masikini hazipo?
Mbona Hugo Chavez alihakikisha rasilimali za taifa lake zinawanufaisha wananchi wote maskini kwa matajiri. Sisi viongozi wetu mnakwama wapi?