Njilembera
JF-Expert Member
- May 10, 2008
- 1,496
- 607
Mwl Nyerere akiwa na familia, pili akiwa analima ameinama hajawekewa jamvi ili asichafuke, yule anabembea, na katika kupanda mti anawekewa jamvi! Contrast ni dhahiri.
Wengi wanaomlaumu Nyerere kwa hali mbaya ya uchumi hawaangalii mfumo mzima wa wakati ule. Nyerere hakuwahi kuwekewa vikwazo rasmi, lakini ukweli vilikjuwepo. Nchi za magharibi hazikuwa na upendo naye kwa sababu ya ufadhili wake wa vyama vya ukombozi bara la afrika. Lakini hawakuthubutu kutokeza hadharani maana alikuwa na nguvu kubwa ya hoja, nakumbuka alivyokuwa anawatukana Reagan na Magreth Thatcher kule kwao (sio kwa vyombo vya hapa, hapana kule London Washington, tena akiwaita FOOLS,).
Wakati mwingine namsikitikia jinsi alivyojitahidi. Kama mnakumbuka ujenzi wa reli ya TAZARA ulipigwa mikwara na kila mtu, lakini Nyerere alisisitiza umuhimu wake na rafiki zake wachina wakaijenga. Leo hii mchango wa reli hii hauonekani sana kutokana na barabara kuu kuwepo. Lakini wkati ule waulizeni watu wa Kilombero, Iringa, Mbeya wakusimulie.