Tundu Lissu VS Mwl. J.K Nyerere

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Ukiwaaangalia kwa ukaribu wanasiasa hawa wawili wanafanana kwa kwa matendo yao na misimamo yao linapokuja suala la Uzalendo na utaifa.

Kwanza wote wawili wanaamini katika kuongea ukweli hata kama ukweli huo unachoma kuliko kunyamaza aidha kwa hofu au kujipendekeza ili upendwe na kundi fulani kinafiki. Wapo tayari kuongea walaumiwe kuliko kukaa kimya wakati wanaona wanao wajibu wa kusema.

Pili katika ulinzi wa rasimali za nchi wote wawili wanaamini kuwa Mali za Tanganyika ziwanufaishe Watanganyika. Nyerere hakuleta mchimbaji madini hta mmoja alisema Watanganyika wakiwa na uwezo watachimba haziozi hizi mali.

Ugomvi wa Lissu na wenye malaka unatokana na mtazamo uleule wa Nyerere kuwa madini ni mali za wananchi. Lissu alianza ugomvi na Mkapa na Kiwete kwa mikataba mibovu iliyo dhalilisha nchi na wananchi. Ugomvi wa Lissu na Magufuli haukuwa katika mikataba bali ulihusu matumizi mabaya ya rasimali za nchi na utawala usio na utu na demokrasia.

Wote wawili wamenusurika kuuwa kutona na misimamo yao thabiti isiyo yumbayumba kuitetea nchi dhidi ya udhalimu. Nyerere alinusulika kupinduliwa na wanajeshi waasi mwaka Lissu vilevile amenusurika kuuwa kwa kupigwa risasi na watu wasio julikana akina kingaeiou.

Wote wawili wana kariba ya ushawishi hasa pale mambo yanapo kuwa magumu. Mtakumbuka Nyerere alivyo shawishi wajumbe wa CCM kumchagua Mkapa badala ya Kikwete. Kikwete alikuwa anashinda bila Nyerere kuingilia kati na kwapoza wajumbe kuwa Kikwete tuendelee kumlea ktk chama atatusaidi baadae.

Ukija katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kila mtu alikata tamaa kuwa hakuna mtu atashindana na Magufuli. Hali ilibadilika ghafla kijana mzalendo Tundu Lissu alipochukua fomu ya Urais. Katika Mpira unaweza kusema alikuwa super sub. Kampeni zilikuwa ngumu nchi ikatikisika ghafla tuu mpaka CCM wakaomba poo kufungia kampeni za Lissu. Hata mimi niliapa kuwa nisingepoteza muda kwenda kupiga kura lakini ile amsha amsha ya Lissu nikasema ntaenda kupiga kura.

Kifupi Nyerere na Lissu wamebarikiwa na Mungu kuwa na kariba ya uongozi hata kama hawana mamlaka. Mtakumbuka Nyerere alikuwa anaogopwa hata alipokuwa amestaafu. Hivyo hivyo utaona namna Lissu anavyo ogopwa hata kutumiwa wauaji wenye siraha za kivita nyumbani kwake mtu ambaye hana mamlaka yeyote. Ndani ya Tundu Lissu unamuona Nyerere.

Tundu Lissu ndiye Nyerere Mungu aliye tupatia kwa sasa.
 
Mtu unapokunywa chai ukachanganya na cuber, utaanza kuona maisha ni sawa tu unasahau wadeni wako woote na kujiona uko matawi

Acheni kulinganisha watu na vitu
 
Ukiwa na akili za Kitumwa kamwe hauwezi ukampenda Tundu Lissu.

Ukiwa haupendi kuwa huru na endelevu siku zote utamchukia Tundu Lissu.

Ukikosa Ukomavu wa akili kamwe hauwezi ukampenda Tundu Lissu.
 
Unataka kusema na Nyerere nae alikuwa anahitaji kutumia dawa ili kichwa kitulie?
Nyerere alikuwa ni binaadamu na alikiri baadhi ya mapungufu aliyoyashiriki kwenye uongozi wake.

Mimi nakumbuka 1974 tuliswagwa kama mifugo na kulazimishwa kuhamia vijijini, huku tukiacha miji na mashamba. Nyingine ni kushiriki vita vingi barani Africa bila returns. Muungano usioeleweka mpaka leo. So akilinganishwa na wengine not bad at all.
 
Back
Top Bottom