Linganisha BMW Vs JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Linganisha BMW Vs JK

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by manyusi, Oct 25, 2010.

 1. m

  manyusi JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 274
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  KIONGOZI BWM Vs JK
  MWAKA 2000 -2004 Vs 2005-2009

  Unga 460 Vs 1000 = 217%
  Mchele 600 Vs 1200 = 200%
  Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
  Mkate 250 Vs 700 = 280%
  Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
  Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050 = 233%
  Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
  Nazi 100 Vs 550 = 550%
  Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%

  unalipwa 100,000/-kwa mwezi kwa jedwali la hapo juu kila siku lazima
  ununue unga robo 400, mchele nusu 300, uto kibaba 125, mafta taa
  kipimo 300, sabuni nusu kipande 50, sukari robo 400, maharagwe robo
  250, mkaa nusu kisado 300, nauli go & return 500, maji ya kunywa 500,
  hapo ni bachalor kwa siku ni 3,125 mara 30 = 93,750 kwa mwezi. Okay
  kodi kwa mwezi 20,000/- umeme 6000 kwa mwezi =total kwa mwezi ni
  120,000/- je hiyo 20,000/- ziada katoa wapi????? ndo hizo mwisho wa
  siku zina wapeleka jela au kuwanaachishwa kazi. Je maisha bora hapo
  atoe wapi? Na je angekuwa na mtoto wa shule au watoto wawili? hapo
  hajaumwa, hajatembelewa na mgeni akamnunulia soda, hajanunua nguo
  nyingine!!!! Huyu mnaempigia kura hayajui hayo na hatambui kama una
  familia kijijini pia. wao wanatibiwa na serikali, mafuta ya magari
  kwao ni sawa na kumuuliza bibi akupigie story ya sungura. wenzie
  wakitaka ongezo la mshahara wanajadiliwa in 2Hrs jibu tayari ila
  waalimu na wenzao.........! 3 years.

  Yeye huyu JeyKey na hao wapambe wake na hao wanajipendekeza kama
  Shigongo waulizeni watoto zao ni akinani? utaambiwa mbunge, mara yuko
  BOT mara yule wa mwisho yuko ulaya kamtembelea shangazi yake, mara
  yuko busy na tenda ya kusuply komputa Wizarani. Wewe je unae mpigia
  kura tupe wasifu wako hata hao watoto wako na wategemezi wako. Hata
  baiskeli kule kijijini huna wala wazazi wako ndo unakesha kuwaombea
  wasiumwe kwa kuwa gharama za hospitali zitakuwa zako.

  Muulize kesi za mafisadi vipi? Na je wanampango gani? utaambiwa yuko
  busy na harakati ya kutafuta ulaji kwa mara ya pili.

  Hao wapambe wake na mawaziri wanaendesha magari gani utaambiwa aah
  wana tano tano kila wizara VBV8, uliza bei zake kila moja, inatumia
  mafuta kiasi gani kwa mwezi, na majukumu yake ni yapi? Na je
  zinakoenda akina RAV4, Suzuki, BMW ndogondogo hawafiki? Utaambiwa
  wanawahi kuwasilisha agenda. KWEEELI?

  Na je hizo gharama za uendeshaji fedha zinatoka wapi? Utajibiwa kwenye
  mfuko wa serikali. Waulize serikali ina miradi gani ya kuweza
  kuendesha hayo magari tu achana na posho zao na mengineyo? Jibu ni
  KODI ZENU wananchi waungwana tulio na amani na utulivu kwetu. KWEELI
  kwa mshahara wa laki mbili zangu/zako?

  FUNGUENI MACHO NA AKILI ZENU WAUNGWANA. Wenzenu Zenji wameshaliona
  hili wameamua kujichorea MIPAKA yao Mapema.

  MTAENDELEA KUZUBAISHWA NA STORI ZA KUTUNGA NA UDAKU NA KUSHANGILIA
  MISAFARA MIREFU YA KAMPENI INAYOUNDWA KWA KODI ZENU.
   
 2. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maisha na Jk hayawezekani, atoke tu
   
 3. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  haiwezekani hata siku moja ukamchukua mkapa -mchele ukalinganisha na kikwete-pumba.
   
 4. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mwenyewe aliishawaambieni kuwa mkiona bei zinapanda mjue maisha yanazidi kuwa bora kwani watu wanauwezo wakununua hizo bidhaa a.k.a foleni za barabarani Dar ni kielelezo kuwa maisha sasa ni bora kuliko ilivyokuwa miaka ya 90! Na watu wanapiga makofi kumshangilia.
   
 5. R

  Rugemeleza Verified User

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hakuna cha kulinganisha wote hawafai ni sawa na kitumbua kucheka andazi vyote vimepikwa kwa mafuta.
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Wote ni wa CCM.

  Mmoja ana tamaa na akili mwingine ana tamaa bila akili.

  Wote huzidiwa na tamaa wakashindwa tena kuona mbali zaidi ya nyumbani kwao tu.
   
 7. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mchagueni Kiwete, mtaona Dola moja itafikia Sh 50,000 ndani ya mwaka mmoja tuu.
   
 8. m

  mkmziya2 New Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waungwana, naungana nanyi mengi, ila la kulinganisha bei za 2005 na 2010 naona si sahihi kama kigezo cha kuwalinganisha viongozi hao. Definately, bei za awali kunako 1995 ni za chini kuliko za 2005, hii ina maana Mwinyi ni bora kuliko Mkapa? Ni mtazamo tu.
   
Loading...