Linex aapa kutofanya kazi tena na Adam Juma

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,829
15,791
Kupitia kipindi cha weekend chartshow cha Clouds Tv msanii Linex amemchana vibaya Adam Juma na kumtupia lawama kwa kumfelisha kwenye wimbo wake 'Salima', amesema huo wimbo audio ilikuwa kali ila video 'iliuvuta shati', kuna baadhi ya vituo vilikataa kuucheza kwasababu ya quality mbovu, kwa sababu hiyo ameapa kutofanya kazi tena na Adam Juma hata iwe bure!
 
Maoni Yangu: Mi nadhan Linex anastress za wimbo wake kutofanya vizuri kinyume na matarajio, alikuwa na matarajio makubwa Sana kwavile Diamond yuko ndani, hiyo video sio mbovu kwa kiwango anachosema, na sidhani Kama kuna TV bongo inaweza kukataa kuucheza kwasababu ya quality, mbona wanachezaga video mbovu maranyingi tu, Linex stress zako usizihamishie kwa Adam Juma, usimtafute mchawi jipange!
 
1.Salima audio ilikuwa one the best track in Tanzania
2.Linex anadai alimpa dau kubwa 5m ambayo kwa wakati huo Adam Juma alikuwa analipwa ndogo kuliko hiyo

3.Video ya Salima ni moja ya video mbovu kwenye video za Linex

4. Uzuri wa video una impact kubwa sana kumtangaza msanii,hata Diamond kuna nyimbo zake za kawaida bali video ndio zinambeba
 
Linex ni kati wasanii wapambanaji nnaowafahamu maana amezungukwa na ma-giant kibao ila hachoki kufurukuta na anasimamia kwenye kile anachokiamini yaani style ya pekee ake.Ila bangi,usela mwingi na kuropoka vinamponza mara nyingi unawezaje kuropoka namna hii kwa video yenye budget around 5 milioni unataka ikupeleke mbaaaali ivi hapa Tz ni Tv station gani ina ubavu wa kutopiga video ya Salima kisa quality awaulize wenzake wanaweka 40 milioni na air time ni miezi miwili inatupwa kapuni nakumbuka AJ aliwahi sema wasanii wetu hawalipi vizuri naamini akiulizwa AJ atakuambia Linex amelipa 2-3 milioni sina nia ya kumtetea AJ ila hakupaswa kujiapiza kua hatofanya nae video kwa pesa zake za kuunga unga.
 
Maoni Yangu: Mi nadhan Linex anastress za wimbo wake kutofanya vizuri kinyume na matarajio, alikuwa na matarajio makubwa Sana kwavile Diamond yuko ndani, hiyo video sio mbovu kwa kiwango anachosema, na sidhani Kama kuna TV bongo inaweza kukataa kuucheza kwasababu ya quality, mbona wanachezaga video mbovu maranyingi tu, Linex stress zako usizihamishie kwa Adam Juma, usimtafute mchawi jipange!

Fuatilia mambo ndio ukomment... Channel 0 walikataa kuicheza hyo video wakasema haina Quality
 
Mkuu video yenye budget ya 5 milioni and i'm sure itakua less than that unataka ipigwe channel O c'moooon basi Diamond atakua mwehu kwa kuweka 40-50 kwenye video zake,kwa 5 milioni AJ atakodi vifaa vya kisasa kwa nani angalia video ya UTANIPENDA behind the scene ile crew yote si wangegawana laki laki tuacheni utani bwana na lawama kwa directors wa nyumbani kwa pesa ya bia.
 
Soma uelewe comment ya mwenzako kabla ya kukosoa, wapi nimeandika channel o? Hivi channel o ni TV ya bongo ee?
 
Mkuu video yenye budget ya 5 milioni and i'm sure itakua less than that unataka ipigwe channel O c'moooon basi Diamond atakua mwehu kwa kuweka 40-50 kwenye video zake,kwa 5 milioni AJ atakodi vifaa vya kisasa kwa nani angalia video ya UTANIPENDA behind the scene ile crew yote si wangegawana laki laki tuacheni utani bwana na lawama kwa directors wa nyumbani kwa pesa ya bia.

Unachanganya mambo,Linex hakutaka kufikia viwango vya Diamond ile video nafikiri hata Adam Juma akiambiwa alete list ya video zake mbovu lazima ataiweka

Kuna video nyingi zimetengenezwa na ma-director wa bongo (include Adam Juma) kwa budget ndogo kuliko hiyo 5m lakini ni nzuri.
Ile video hata kwa standard za hapa bongo ni mbovu
 
Kama unafahamu Linex utakua unanielewa,kwanza kasema kalipa 5 milioni ambayo AJ hajawahi kulipwa yeye kavunja rekodi usiniulize Mavoko kwenye pacha wangu aliweka mzigo kiasi gani naomba hata nijuzwe kituo gani kiligoma kuipiga ile video kisa ubora hapa Tz uyu Sunday awe na akiba ya maneno kwa maisha yake ya kisela vitu vingi anaunga unga atajifelisha mwenyewe nakumbuka AJ alisema ubovu wa video nyingi ni budget finyu wanaishia kuomba magari kwa washikaji kwa kua uwezo wa kukodi haupo
 
Mkuu video yenye budget ya 5 milioni and i'm sure itakua less than that unataka ipigwe channel O c'moooon basi Diamond atakua mwehu kwa kuweka 40-50 kwenye video zake,kwa 5 milioni AJ atakodi vifaa vya kisasa kwa nani angalia video ya UTANIPENDA behind the scene ile crew yote si wangegawana laki laki tuacheni utani bwana na lawama kwa directors wa nyumbani kwa pesa ya bia.

You should be big headed thinking like every best video played by chanel is of that cost you think... fuatilia ujue gharama za video za cabosnoop zilitengenezwa by how much and still got airtime...

Usichokijua ni kwamba kwa hyo hyo milion Tano adam juma almhakikishia itakuwa best video itakayokuwa na level za kimataifa.. Ndio maana baada ya kukataliwa na international chanels adam juma alimpa linex nafas ya kufanya nae video bureeeeeeee..

Unasema milion tano ni pesa ndogo kutengeneza video nzuri... Unaifaham track ya juma nature Dance with me??? kwa taarifa yako video yake haikufikia hata milion tano lakin ilikuwa nominated kwenye tuzo za kora kama miongon mwa video bora..

Fuatilia mambo
 
Kama unafahamu Linex utakua unanielewa,kwanza kasema kalipa 5 milioni ambayo AJ hajawahi kulipwa yeye kavunja rekodi usiniulize Mavoko kwenye pacha wangu aliweka mzigo kiasi gani naomba hata nijuzwe kituo gani kiligoma kuipiga ile video kisa ubora hapa Tz uyu Sunday awe na akiba ya maneno kwa maisha yake ya kisela vitu vingi anaunga unga atajifelisha mwenyewe nakumbuka AJ alisema ubovu wa video nyingi ni budget finyu wanaishia kuomba magari kwa washikaji kwa kua uwezo wa kukodi haupo
Mkuu video ya Pacha wangu ya Mavoko imefanyiwa South Africa na na Salima imefanyiwa bongo,unatagemea cost ipi itakuwa ghali na director hakuwa AJ peke yake kuna mshikaji mwingine alishiriki.Linex anaweza kuwa na matatizo yake lakini nasisitiza ile video ya Salima ilikuwa mbovu mno kuna video za bei rahisi kuliko hiyo lakini ni nzuri na uzuri wa video sio gharama tu ni script ya director
 
You should be big headed thinking like every best video played by chanel is of that cost you think... fuatilia ujue gharama za video za cabosnoop zilitengenezwa by how much and still got airtime...

Usichokijua ni kwamba kwa hyo hyo milion Tano adam juma almhakikishia itakuwa best video itakayokuwa na level za kimataifa.. Ndio maana baada ya kukataliwa na international chanels adam juma alimpa linex nafas ya kufanya nae video bureeeeeeee..

Unasema milion tano ni pesa ndogo kutengeneza video nzuri... Unaifaham track ya juma nature Dance with me??? kwa taarifa yako video yake haikufikia hata milion tano lakin ilikuwa nominated kwenye tuzo za kora kama miongon mwa video bora..

Fuatilia mambo
Haaaa haaa dance with me ya Juma ilitoka mwaka gani fananisha mapinduzi ya video kipindi kile na leo alafu changamsha ubongo wako budget ni kila kitu kwa sasa kwenye video zamani directors walikua wanakomaa bure kutengeneza jina sasa ivi pesa mbele nenda muulize Nisher video yake ya kwanza na Weusi alipewa nini(bureeee) kabisa sasa ivi hakuna kubahatisha weka mpunga watu walete vifaa na materials kwa ajili ya video narudi 5 milioni ni haiko mbali na video za kipaimara.
 
Wenzake wanaweka mzigo wa 50 million....yeye 5milion anapiga keleeele kwenye media......aende kwa godfather basi kama pumzi anayo
 
Sisi wengine tukisema Kua video mbovu zinaangusha sana wasanii mijitu inatuita Nyumbu... Hata hivyo Mpunga wa Msanii Ndio unadetermine ubora wa kichupa anachotaka.. Ile video ya Salima ina Giza sana.. Jamaa alitumia camera ya simu Motorola Bapa nadhani.
 
Back
Top Bottom