Debby the FEMINIST
Member
- May 4, 2020
- 32
- 37
Wakati dunia ikiadhimisha siku ya wanawake Duniani, wanawake wa kata ya Rutamba halmashauri ya manispaa ya Lindi wamelia na changamoto ya uchakavu wa miundombinu katika kituo cha afya cha Rutamba.
Wamelalamikia hayo baada ya wafanyakazi wanawake kutoka Mashujaa FM kufika kituoni hapo kuadhimisha siku ya wanawake ambapo miongoni mwa changamoto walizozitaja ni Pamoja na kukosekana kwa jengo la kuhifadhia maiti hali waliyoeleza kuwa, ikitokea mgonjwa amefariki mwili wake hukaa wodini na wagonjwa wengine mpaka ndugu waufuate.
Aidha wamesema changamoto nyingine ni kukosekana kwa wodi ya akina mama waliojifungua na wajawazito pamoja na kukosekana kwa huduma ya vyoo vya kutosha hali inayowalazimu baada ya kujifungua kutumia choo kimoja na wananchi wengine ambao hufika hapo kupatiwa huduma mbalimbali.
Katika hatua nyingine wameeleza kuwa, Pamoja na kuwa na umeme ila inapotokea umekatika muuguzi hulazima kuomba watu wamuwashie tochi ya simu ili kumzalisha mama mjamzito hasa nyakati za usiku kwani hata solaa iliyonunuliwa na wauguzi kupitia pesa zao binafsi imeharibika.
Kituo hicho cha afya kimejengwa mwaka 1967 na kwa sasa kinahudumia wananchi Zaidi ya 500 kutoka katika vijiji zaidi ya 8 na kukiwa na wataalmu 9 pekee.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo amesema wamefanya jitihada za kurekebisha kwa pesa zao moja ya chumba ambacho wanakitumia kama wodi japo bado wanauhitaji wa jengo la upasuaji na wodi