Lindi: Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye apata ajali akiwa safarini kuelekea wilaya ya Liwale

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mbunge wa (CCM), Jimbo la Mtama mkoani Lindi Nape Nnauye, amepata ajali baada ya gari aina ya Land Cruiser VX yenye namba T 349 DEL alilokuwa amepanda kupinduka leo asubuhi Septemba 24, 2018 katika kijiji cha Kibutuka, akiwa safarini kuelekea wilaya ya Liwale kushiriki kikao cha Kamati Kuu ya siasa mkoa wa Lindi.

Mwandishi wa Azam News mkoani Lindi, John Kasembe amesema hakuna madhara makubwa yaliyotokea kwa waliokuwa ndani ya gari na nje ya gari.

Ameeleza kuwa Nape Nnauye alikuwa njiani kwenda kuungana na ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dr Bashiru Ally anayezuru wilayani Liwale mkoani Lindi.

Hii ni mara ya Pili kupata ajali akielekea Lindi. Zaidi soma=>Nape Nnauye apata ajali Kilwa, alikuwa akitokea Dar kuelekea Lindi - JamiiForums
IMG_20180924_091035_705.jpg
IMG_20180924_091005_383.jpg
IMG_20180924_091020_560.jpg
 
Pole Nape. Ajali nyingine unapata mshukuru Mungu sana
 
Mbunge wa jimbo la Mtama amebusurika kifo baada ya gari aliyokua akisafiria kupata ajali na kupindukuka.

Ajali hiyo imetokea wilayani Liwale.
Source Radio One Stereo
 
Pole Mh Nape,ajali zimekuwa zikimuandama sana hata wakati wa kampeni 2015 alipata ajali huko huko kwake.Jaribu kuwaona wazee ukatambike kidogo kuna kitu hakiko sawa.
 
Back
Top Bottom