BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,423
- 8,229
Amandus Chinguile ni mbunge wa Magufuli hakutokana na kura za umma. Mgombea wa CHADEMA jimbo la Nachingwea, Dkt. Mahadhi Mmoto aliporwa ushindi wake na kutangazwa Amandus kimagendo.
27.10.2020, mgombea Ubunge Jimbo la Nachingwea 2020 CHADEMA, Dkt. Mahadhi Mmoto, alikamatwa (siku moja kabla ya kupiga kura) akiwa na wenzake kumi na moja wakapelekwa Mahabusu.
28.10.2020, Dkt. Mahadhi Mmoto, akatolewa mahabusu na Polisi Mahabusu (Mmoto pekee yake) akaenda kupiga Kura na kurudishwa Mahabusu. Wenzake 11 hawakupiga kura.
29.10.2020, akatolewa mahabusu na kupelekwa kwenye majumuisho ya kura. Siku hiyo wote wakasafirishwa na kupelekwa Lindi walifunguliwa kesi wakidaiwa kuharibu Mali za Serikali.
29.10.2020, Dkt. Mahadhi Mmoto akiwa gerezani., Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nachingwea, Amandus Chingule akapewa kura 36,761 na Dkt. Mahadhi Mmoto CHADEMA akapewa kura 27,801.
Hadi siku Magufuli anaapishwa kuwa Rais wa Tanzani, Dkt. Mahadhi Mmoto na wenzake 11 walikuwa gereza la Lindi wamenyimwa dhamana kwa tuhuma za kuharibu mali za Serikali na CCM.
Leo mbunge wa Magufuli anaonja joto ya jiwe kwa kuzomewa na wananchi na wakisema hawamtaki wamemchoka. Hii inatukumbusha kwamba dhulma siyo riziki. Mganga anafariki.