Lily Flower amefiwa na kaka yake

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,323
18,793
Wapendwa wa jukwaa hili pendwa la MMU,
Ningependa kuchukua fursa hii kuwajulisha kwamba, mwenzetu Lily Flower amefiwa na kaka yake wa kuzaliwa.
Tukiwa kama rafiki zake, ndugu zake, tuungane nae katika msiba huu, tukimuombea moyo wa uvumilivu wa kuweza kukabiliana na wakati huu mgumu uliopo mbele yake kwa sasa.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
Amen.
 
RIP Bro, pole sana Lily Flower, Mnyazi Mungu atakupa nguvu katka kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana Dada LilyFlower
R.I.P Bro, Mungu akulaze pema peponi Amina
 
RIP brother!!!

Pole sana LilyFlower, Mungu akupe nguvu kipindi hiki kigumu kwako.
 
Pole sana Lily... Mungu akupe nguvu ya kushinda katika wakati mgumu kama huu. You loved him but HE loved him more. Rest in peace brother...
 
Wapendwa wa jukwaa hili pendwa la MMU,
Ningependa kuchukua fursa hii kuwajulisha kwamba, mwenzetu Lily Flower amefiwa na kaka yake wa kuzaliwa.
Tukiwa kama rafiki zake, ndugu zake, tuungane nae katika msiba huu, tukimuombea moyo wa uvumilivu wa kuweza kukabiliana na wakati huu mgumu uliopo mbele yake kwa sasa.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
Amen.

Msiba uko wapi? Biblia inasema ombolezeni na wanao omboleza, tutakuwa sio marafiki wa kweli uwapo tutakuwa tunaombolezea kwenye intanet wakati mwenzetu hajafiwa ki intanetintanet. Wenye nafasi twendeni tukamtie moyo, tukamfariji, tukakae nae sakafuni. Naomba mnipe physical address mi niende, kama msiba uko hapa DSM.
 
Lily flower ...there's no way I can even try to imagine what you are going through. All I can do is pray and depend on the Lord to renew your spirits and provide you with what you need.R I P Dear bro
 
Msiba uko wapi? Biblia inasema ombolezeni na wanao omboleza, tutakuwa sio marafiki wa kweli uwapo tutakuwa tunaombolezea kwenye intanet wakati mwenzetu hajafiwa ki intanetintanet. Wenye nafasi twendeni tukamtie moyo, tukamfariji, tukakae nae sakafuni. Naomba mnipe physical address mi niende, kama msiba uko hapa DSM.

Asante sana kwa kuonyesha moyo huo.......msiba haupo Dar, upo Arusha (Karatu). Nitakavyozidi kupata taarifa ndivyo nitakavyoendelea kuwaletea, ili kama kuna members waliopo huko waweze kuhudhurua ili kumfariji mwenzetu
 
Bwana ametoa, bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe.

Pole sana LF pamoja na familia yote. Mungu awatie nguvu.

RIP kaka.
 
Back
Top Bottom