Likizo

Likizo

happiness win

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
2,461
Reaction score
1,394
Habari zenu mabibi na mabwana. Napenda kuwajulisha kuwa nimerudi likizo ingawa sikuwaaga.Likizo ina raha jamani, maana unapumzisha mwili, moyo, na akili. Si vibaya nikiwashauri wote muwe mnaenda likizo kwa faida yenu. Msing'ang'anie kuhangaika mwaka mzima bila kupumzika mkidhani ndio mtafanikisha malengo yenu katika utafutaji.

Make sure unapata muda mzuri wa kupumzika. Ikiwezekana jipangie kusafiri kwenda sehemu nyingine kipindi cha kupumzika. Sio lazima uende ulaya, hapa hapa TZ kuna sehemu nyingi za kukufurahisha na kukupumzisha kimwili na kiakili. Hata kama mambo yamebana, basi baki hapo hapo kwako ukijipumzisha.

Wape likizo hata watumishi wako, mke wako au mume wako! na utafurahia utendaji kazi wao/wake baada ya mapumziko.Kumbuka kipindi cha likizo si kipindi cha kuanzisha kazi, au shughuli nyingine, ni kipindi cha kupumzika! Furahia maisha.Usisahau kutenga bajeti ya likizo kila mwaka katika mapato yako!
 
ulikua wapi mrembo wetu.....
 
Wengine muda wote 24/7 tupo likizo
 
mwaka huu mvua hazikunyesha, mavuno hayakuwa mazuri.
Likizo tena!!!?????
tunahitaji tani 78.5 za msaada
Ngoja nitafakari hii kilimo kwanza afu ndo nichangie mada
 
Fanya kazi kama mtumwa,................ Mtumwa hana likizo.
 
MASKINI YA MUNGU REJAO WA WATU!!!
Wala usihofu my feis buku..huyu anajaribu kuona wamama wa nyumbani hawana thamani, kumbe wana mchango mkubwa sana kwa familia especially kwenye malezi ya watoto.
 
Likizo inataka uwe na pesa, wewe unakula mara moja kwa siku halafu unataka kwenda likizo
 
Wabongo kwa kupenda likizo! Kazini kwenyewe mnaingia saa nne then saa nne na nusu supu, saa sita lunch, saa saba na nusu kusoma magazeti, saa tisa mnarudi majumbani kwenu. Likizo ya nini wakati kazi hamfanyi?
 
Back
Top Bottom