Likitokea hili 1/4 ndo watabaki kwenye ndoa

Likitokea hili 1/4 ndo watabaki kwenye ndoa

1. Ukitaka kuwa na mwenzi perfect basi perfection ianzie kwako.
Kama Mke wako hakati kiuno kama geni basi wewe kata kiuno kama pangaboi LA bombadia.
2. Usitarajie miujiza mikubwa ku toka kwa mwenzio nae pia ana makosa na hukosea
3. Jifunze kuwa mvumilivu na mwenye kusamehe maisha yatakuwa rahisi kwako
4. Jiepushe na uwongo
Umesahau 'jifunze kuridhika'
 
Inaelekea mtoa mada ana wakati mgumu sana kwenye ndoa yake.
 
Pana mtunzi mmoja mahiri David mailu katika kitabu chake cha am a common man alijaribu kuongelea khabari ya kuoa na swali lilikuwa why I married? Watu wakafunguka mmoja akasema alikuwa anataka mwanamke wa peke yake ndo maana akaoa mwingine akadai huwa anashindwa kukaa muda mrefu bila kupata huduma hiyo mwingine akajibu alidhani ndoa ni kama pepo so akaamua kuoa ila wote hao walikuja kutoa points za kujilaumu kwa nini walioa kutokana na maswahibu yaliyowakuta kuna mmoja alimalizia kwa kusema to hell with marriage.
Pia kuna wengine huo sio kwamba they're in such love but for they're defence maana kuna msukumo toka kwa wazazi mbona umri unakwenda hutaki kuoa au unataka mpaka utuzike ndio uoe wazazi wakifika huko basi unaamua kuoa.
NB:kwa kuwa tunajadili vitu vya kusadikika wacha tuendelee kujadili.
 
Mi nina 5 yrs katika ndoa na sijajutia kuolewa na huyu baba so ikitokea hivo nitarudiana naye kwa moyo mmoja. Labda kwa vile bado mi mchanga katika ndoa!
 
Ikitokea Mungu akaruhusu sahiz kuturudisha nyuma muda wa kuoa au akavunja ndoa hizi na kutaka watu waoe upya

Je utamuoa tena huyo uliyenaye????

Kwangu mimi hapana na naamin 1/4 tu ndo wataoa walionao
Kisa cha kweli cha Mhaya mmoja Mkatoliki:

Amekaa na mwanamke kwa miaka kadhaa, bila ndoa ya kanisa, na kujaliwa kupata watoto.

Ikatoe mmoja wa watoto wake wa kiume alipata nafasi ya kuendelea na masomo Seminari.

Kwa kuwa wazazi hawakuwa na ndoa halali kikanisa, ilibidi wafanye hivyo.

Siku ya kubariki hiyo ndoa, bwana akaulizwa, "utamampenda ... Kwa mema na mabaya hadi kifo kiwatenganishe?" Du, jamaa akajibu "leka leka leka, padri humjui huyu alivyo mkorofi ati unitwishe msalaba wa kuishi naye milele, leka leka leka bojo"!

Huyu jamaa ni mmoja kati ya wanandoa ambao wangependa ulichoshauri.

J2 NJEMA NAWATAKIENI
 
Ikitokea hivyo wengi wata opt kubadilisha wenza wao, lakini wengi ambao wata opt hivyo baada ya muda watatamani warudiane na wenza wao wa awali.

Unajua kwa sababu wengi wetu hatujua upande mwingine ukoje, yaani hatujawahi kuishi na watu wengine then tunafikiri kwamba tuna wenza ambao hawatufai.

Ukiona couple nyingine unafikiri labda jamaa ana bahati ana mke mwema na mzuri, au ana mme mwema kuliko wa kwako. Kumbe ni vile tu uko nje, unawaona kwa nje, ukipewa uishi naye wewe utaona ayaaa kumbe ndo hivi.

Usia kwangu kwa kila mwana ndoa, ridhika na uliye naye, huyo ndo mungu amakuchagulia. Ishini kwa mapenzi mema na kuombeana heri.
Umesema vema
 
Katika uislam NDOA ni nusu ya dini (yaani ktk mitihani ya dunia hii ambayo inatakiwa upambane nayo ili mwisho wa wa siku ufaulu basi NDOA ni nusu ya balaa zooooote).

Unadhani mchezo ?
 
Back
Top Bottom