The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,780
- 8,155
Wewe hukuzaliwa hapa duniani kama jiwe, mti, mdudu wala mnyama; ulizaliwa kimaalumu kabisa kama binadamu kwa LENGO au KUSUDI maalum; unatakiwa ulijue na ulitimize kabla hujaondoka kwenye uso wa hii dunia kurudi ulikotoka!
Haupo duniani ili mradi hupo tu, la hasha, hupo kwa ajili ya KAZI AU WITO MAALUM kama Yesu na wengi wengineo unaowafahamu!
Kila binadamu ni Masihi (yaani ni Kristo), mpakwa mafuta kwa ajili ya kusudi hili au lile.
Yesu alikuwa Masihi kwa ajili ya kusudi lake, mimi na wewe ni Masihi/ Kristo kwa ajili ya makusudi mengine.
Hakuna mbegu iliyofaulu kutunga mimba na kuzaliwa na mpaka sasa ipo ipo tu ili mradi tu.
Kama wewe ulifaulu kuingia kwenye tumbo la uzazi la mama yako, ukaishi miezi tisa na ukazaliwa mpaka sasa unaishi, wewe ni Kristo, ni Masihi, yaani mpakwa mafuta. Umepakwa mafuta utimize kusudi fulani kama tabibu, mwandishi, kiongozi, fundi ujenzi, mwalimu, askari, mkufunzi wa watu fulani, msanii wa maigizo, muziki nk.
Mimi sio wewe na wewe sio Mimi.
Mimi nilizaliwa kabla yako na wewe ulikuja baada yangu; sote ni Mitume kwa makusudi maalum!
Kabla hatujawa kwenye hii miili tunakuwa raia wa kudumu kwenye ulimwengu mwingine unaitwa ulimwengu wa roho (usioonekana, unaweza ita mbinguni au vyovyote, ili mradi ni ulimwengu usioonekana, wa kiroho)
Huko kuna viongozi wetu wakuu ambao tunafanana nao, walitutangulia kuwepo, tunaweza kuwaita kila aina ya majina kama vile, Miungu, Mabwana, Wazee nk. ili mradi tu kuonesha vyeo vyao vya ukuu kuliko sisi.
Hawa Miungu, Mabwana, Wazee wa Siku (Ancestors) kila mara hukaa Kikao kuhusu nani atumwe aje duniani kwa kusudi maalum.
"Nimtume nani?"
Sauti ya Mzee wa Siku (Ancient of the days) ilisikika kwenye Kikao/ jopo la wazee wenzake.
Kisha ikaendelea, "Ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu?"
Yaani nani mwakilishi atakayekuja huku duniani kwa niaba ya hao wazee wa Siku (Gods and Lords) kwa ajili ya kusudi maalum.
Mmoja wapo kati yetu (au wale ambao hawajazaliwa huku duniani) akajibu "Mimi hapa, nitume Mimi" (Isaya 6:8)
Huyo Mjumbe Mimi au wewe akatumwa kwa kupewa maelekezo maalum... "Nenda kafanye moja mbili tatu ..." (mstari wa 9)
Ukimaliza urudi hapa.
Hivi ndivyo Wazee wetu hufanya kila sekunde, kila dakika, kila saa, kila siku, wanatuma wawakilishi wao.
Mimi nilitumwa tarehe 24/7 miaka zaidi ya 45 iliyopita for a special purpose of teaching, healing the sick, pamoja na mambo mengine, of which naendelea nayo mpaka sasa, tangu nijitambue!
Wewe ulitumwa tarehe ngapi, mwezi wa ngapi na mwaka gani?
Tell me.
Na je, wajua ulitumwa ukafanye kazi gani?
Ndiyo kazi unayoifanya hata sasa au bado unakimbia kimbia tu huku na kule bila kujitambua?
Wakati wako wa kuondoka faili lako litakuwa lina taarifa iliyoshiba au ndo yale mafaili yaliyo wazi, ya Mitume/ Masihi wazembe?
Utawaambia nini wazee wako waliokutuma huku duniani?
Tafakari.
NB: Kuna watu wanaweza kukwazwa na matumizi ya viwakilishi "Wazee, Mabwana, Miungu..." nilivyotumia, lakini hilo lisiwe tatizo, nyie wekeni maneno yenu wenyewe "Bwana Mungu" au "Bwana Yesu" au "YEHOVA" au "Allah" nk ili mradi tukubaliane sote kuwa mmetumwa for special purpose na waliotuma ni Wazee wa zamani sana (Wazee wa Siku) ambao waliwahi kukaa Kikao huko zamani na kusema "Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa SURA YETU, wakatawale . . ." (Mwanzo 1:26)
Hoja Kuu: Unakubali kwamba wewe umetumwa kwa kusudi maalum?
Fuatana nami katika sehemu ya pili ya Somo hili.