Lift ya Jengo la Millenium Towers yaanguka ikiwa na watu, kuzidisha idadi ya Watu kwatajwa kuwa chanzo

HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
69,367
94,549
Watu saba wamejeruhiwa baada ya 'lift' katika jengo la Millenium Tower - II, Dar es Salaam kuporomoka kutoka ghorofa ya 10.

Jeshi la Zimamoto limesema chanzo ni lift hiyo ambayo imefanyiwa matengenezo karibuni kuzidiwa uzito ambapo waliingia zaidi ya watu 10 kwa wakati mmoja.

---



Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji Patrick Mohammed amesema, chanzo cha lifti hiyo kuporomoka ni kuzidisha idadi ya watu tofauti na uwezo wake ambapo wakati tukio hilo linatokea ilibeba zaidi ya watu 10.

Lifti hiyo imeporomoka kutoka ghorofa ya 10 na kujeruhi watu 7 ambao wamepelekwa katika hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


Tower.png
 
Tuna matatizo sana unakuta umeandikiwa idadi ya watu ni 7 nyie mnang'ang'ana muingie 12 ingetokea kifo watu waandike Mungu kawapenda zaidi Mungu yupi huyo

Ifike wakati tuache mazoea tufuate masharti kuepusha maafa na hasara zinazoweza kuepukika
 
Back
Top Bottom