Wakati mnabebeshwa hatima yenu kupitia misemo ya wengine, sisi tunaendelea kuishi tu, na ikifika 70 wengine life ndiyo ita begin there.Maneno "life begins at 40" yana maana kuwa mtu akifika umri wa miaka 40, maisha yanakuwa bora zaidi, labda kwa sababu tayari mtu keshapata skills, experiences na namna bora ya kuyafurahia maisha. Msemo huu ulitungwa na mwanafalsafa Pitkins na umejipatia umaarufu mkubwa hapa duniani.
Katika kusomasoma kwangu nimekuja kufaham kwamba kumbe kuna watu wakifikia 40 wanapata hofu ya maisha(hapo hata mimi nikaanza kuwa na hofu), wanahisi uzee unakuja, ujana unaondoka, vile walivyokuwa wakiyafurahia maisha kama kujirusha, kula ujana vyote vinapotea ghafla.
Tunapoingia umri huu wa 40+, tunaanza kujitambua zaidi, kutambua thamani yetu zaidi na kutojali maisha na mawazo hasi ya wengine. Na hapa ndio hoja inapokuja, kwamba kwa mwafrika wa kawaida je ni kweli kwamba life begins at 40? Maana yapo mengi sana tunafatiliana, mtu kaacha yake anasumbukia ya jirani ili mradi tu amuumize au apate furaha kumuona mwenzake anaumia.
Wanasema at 46 life is at the peak, yaani kumbe ukifika 46 ndio umefikia peak ya maisha yako, baada ya hapo ile graph inaanza kushuka taratibu hadi upigwe chepe. Na wengine wanasema ukifika 40+ unatakiwa uwe tayari umefikia malengo yako kwa asilimia 90, kuzaa, kulea, career, kujenga, kusomesha...
Sasa je, nini kinaleta midlife crisis?
Kwa nini katika umri huo mara nyingi tunasemwa kuwa we're going through midlife crisis?
Je, ni kwa sababu huenda hatujafikia malengo yetu ya kimaisha na hivyo kufanya maisha kuwa na ukakasi?
Imagine katika umri huu:
● Huna mke/familia(very optional)
□ Watoto wadogo hawajaanza hata chekechea(kina sie).
● Hujawa na sehemu ya kujibanza(kijumba).
○ Hujawa stable career wise, bado unajitafuta.
Ni lazima kichwa kiwake moto, lazima stress levels ziwe juu na usipoangalia unaweza kupata sonona.
Msije na hoja ya maokoto tu.
Happy Sunday, mtuombee sie wakosefu!!
Kwamba ukifika 40 sio ndio unahangaika kutafuta mtoto, au ndio unahangaika Kujenga nyumba, au ndio unahangaika kutafuta kazi, au ndio unahangaika kufanya biashara, Ni kwamba ukifika 40 uwe umefika hatua ya kustaafu na kuchukua pension na kuanza kula kiinua mgongo chako yaan ukifika 40 ndio unaanza kula mafao ya kile umekipambania tangu ukiwa na Mwaka 1 hio ndio maana ya life begins at 40Maneno "life begins at 40" yana maana
Nah it doesn't bother me, kwa umri huu mtanange sio issue ya kuipa kipaumbele hata kidogo. Kama ulivyosema, ukiwa stable financially hayo mambo yapo tu, na utaendelea kuyafurahia...ukiwa na midlife crisis sex has no value!Au una wasiwasi utashindwa kuperfom kwenye mtanange?
Ni kujichosha akili kuwaza mambo yasiyowezekana kubadilisha hata iweje....Uzee uwe na kiasi,usizeeke sana mpaka above 90 huko Huo ni ubatili,unakosa furaha,unajua umeshuhudia mambo mengi ya kuumiza moyo,unakuwa Huwezi kujitegemea yaani matatizo ni mengi....Kuufikia ni fumbo lakini sometimes nikiwaona baadhi ya wazee wanavyoishi najifikiria mimi miaka hiyo baadae ntakuwa kwenye hali gani? Naishia kusononeka tu ila ujana ni mtamu mno kungekuwa na uwezo wa kusimamisha miaka ningesimamishia hapa kwenye ujana.
nilipokuwa mdogo nilikuwa nawaza nikifikisha miaka 40 najiua ili nife nikiwa HB, Saiv nmeongeza kwenye 70 au 80Uzee huwa unanikosesha raha sana nikiwaza itakuaje
Elezea hiyo scenario kibongobongo mkuu!!Kwamba ukifika 40 sio ndio unahangaika kutafuta mtoto, au ndio unahangaika Kujenga nyumba, au ndio unahangaika kutafuta kazi, au ndio unahangaika kufanya biashara, Ni kwamba ukifika 40 uwe umefika hatua ya kustaafu na kuchukua pension na kuanza kula kiinua mgongo chako yaan ukifika 40 ndio unaanza kula mafao ya kile umekipambania tangu ukiwa na Mwaka 1 hio ndio maana ya life begins at 40
Angalia wacheza mpira TU miaka 35 Gari liko hoi wengine 30 tu tayari pancha wengine wakina Ronaldo ndio wanakomaa hadi 38 Ila ndio hivyo akifika 40 Gari linaenda kupaki mazima haendelei km Ibrahimovic ambae ana 41 Ila bado anapiga kabumbu
Good,nilidhani una waza hiyo kitu..Nah it doesn't bother me, kwa umri huu mtanange sio issue ya kuipa kipaumbele hata kidogo. Kama ulivyosema, ukiwa stable financially hayo mambo yapo tu, na utaendelea kuyafurahia...ukiwa na midlife crisis sex has no value!
Ulikuwa na akili gani🤣🤣nilipokuwa mdogo nilikuwa nawaza nikifikisha miaka 40 najiua ili nife nikiwa HB, Saiv nmeongeza kwenye 70 au 80
Ndio utajiua?nilipokuwa mdogo nilikuwa nawaza nikifikisha miaka 40 najiua ili nife nikiwa HB, Saiv nmeongeza kwenye 70 au 80
Kibongobongo ni hivyo hivyo 40 Mwili unaanza kukukataa lazima uwekeze mapema ukifika 40 uanze kula pension yako ya kile umeweka before 40 Ila tafsiri yake nmekuelezea vizuriElezea hiyo scenario kibongobongo mkuu!!
Umejiandalia makazi? Ukijijua unapopakufikia?nilipokuwa mdogo nilikuwa nawaza nikifikisha miaka 40 najiua ili nife nikiwa HB, Saiv nmeongeza kwenye 70 au 80
Uzee una changamoto nyingi sana hasa upweke mkali mno. Nitajitahidi niache kuwaza haya nisioweza kuyabadilishaNi kujichosha akili kuwaza mambo yasiyowezekana kubadilisha hata iweje....Uzee uwe na kiasi,usizeeke sana mpaka above 90 huko Huo ni ubatili,unakosa furaha,unajua umeshuhudia mambo mengi ya kuumiza moyo,unakuwa Huwezi kujitegemea yaani matatizo ni mengi....
Kuna pakufikia tena baada ya kifo? Mbona hamsemiUmejiandalia makazi? Ukijijua unapopakufikia?
Sawa sawa na ukikaribia 70/80 utaongeza hadi 100 nani anataka kufa?nilipokuwa mdogo nilikuwa nawaza nikifikisha miaka 40 najiua ili nife nikiwa HB, Saiv nmeongeza kwenye 70 au 80
Si tumeandaliwa huko mji wenye asali..Kuna pakufikia tena baada ya kifo? Mbona hamsemi
Hapo kwenye kulinda afya yako nakuunga mkono, tujitahidi tulinde afya ili ukiwa na 50's na kuendelea uone utamu wa maisha kuliko kuanza route za hospital mengine Mungu atulinde ila tuweke jitihada katika ulaji, mazoezi.Niko 77 na ndiyo kwanza kunakucha huniambii kitu ng'wanawane [emoji16][emoji123]
Hizi ni perception za jamii tu ili pengine kuwatia hamasa na kuwaasa walioko huku nyuma wasikakawane kwenye nira za ujana bali wamakinikie zaidi kuanza maandalizi mapema maana ukifika huko 40+ hata process nyingi za mwili zinaanza kukuwashia indiketa kuwa sasa tunahama kwenye msimbo wa ujana na tunaingia kwenye utu uzima sasa.
Hii ni sawa tu na ile perception kwamba eti binti akivuka miaka 30 hajaolewa basi jua lake jema na lililong'aa sana hapo nyuma sasa linaingia machweoni. Na kuna mabinti wasiojitambua ambao kweli wakivuka 30 na bado hawajaolewa wala kuwa na familia wanapaniki badala ya kutulia na kuwekeza katika wao kama wao. Hata katika hili wapo wengi tu wanaofikia hiyo 40+ huku ramani za maisha bado zipo zigzag wanapata sonona hasa wakijilinganisha na waliosoma nao ambao wanakuwa wameshapiga hatua kubwa.
Binafsi kama ningeambiwa leo hii muda urudishwe nirudi huko kwenye 40s kitu pekee ambacho ningekirekebisha ni kuutunza mwili na kujali afya yangu sana. Nisingekunywa mipombe kupindukia na minyama choma hii. Japo ukiwa kijana huwezi kuona madhara yake, ukivuka 45 huku ndiyo sasa utaona kosa ulilofanya - na hapo kama una bahati hujapata presha, kisukari, matatizo ya figo, magonjwa ya moyo na ishu zingine kibao.
Miaka ya 40....kijana linda sana afya yako. Kila kitu kifanye in moderation (ikiwemo ulaji wa mbususu). Mengine yote ni madogo tu hasa kama unajitambua.
Hint: Usijilinganishe na classmates wako. Hypertension itakuhusu [emoji16][emoji16][emoji2221][emoji2221][emoji2221][emoji870]
View attachment 2760494
Acha kuwaza hiyo!unaweza jikuta umeoa katoto kabichiiii ka 18 kanakutia joto🤣🤣🤣Uzee una changamoto nyingi sana hasa upweke mkali mno. Nitajitahidi niache kuwaza haya nisioweza kuyabadilisha
[emoji38][emoji38]wakt ndio mda wa kutafuta au walitak watafute kwenye 15 yrs...kuna watu wana 20yrs Wanadai wamechelewa kutafta pesa