Lifahamu Gugu chawi

Lifahamu Gugu chawi

cactus mkuu!
hope mshana ataelezea vizuri,kuna jamaa yangu ni mzungu m`italiano alinipa hizo skills kuwa niupande mbele ya nyumba,wachawi kwangu watakuwa wanapaona kama kwa baba mkwe,ni kweli tangu niupande sijawahi pata bughudha yeyote kutoka kwa walozi...
Naomba tuwekee kapicha kake mkuu
 
Kuna UA niliambiwa ukiliotesha nyumbani wachawi hawawezi kufanya yao ila sijui ni UA gani hilo
Ninalo nyumbani mkuu!! Achilia mbali wachawi na wapiga zongo pia ni dawa nzuri pia kwa matatizo mbalimbali kama ya tumbo na kichwa! Wahindi wanajua na kuliheshimu sana jani hilo! Mfano mtoto akizaliwa kwenye familia ya mhindi basi jani hilo hutundikwa mlangoni kwa wiki tatu au zaidi wakiamini kuwa linamwepusha mtoto na mabalaa mengi.
 
Ukiacha Tabia yake ya kushambulia mimea, je matatizo gani mengine ya kiafya yanàyoweza kumpata mkulima kwa kuwepo kwa guguchawii shambani kwake?
Hakuna kama hatakula punje zake
 
Ninalo nyumbani mkuu!! Achilia mbali wachawi na wapiga zongo pia ni dawa nzuri pia kwa matatizo mbalimbali kama ya tumbo na kichwa! Wahindi wanajua na kuliheshimu sana jani hilo! Mfano mtoto akizaliwa kwenye familia ya mhindi basi jani hilo hutundikwa mlangoni kwa wiki tatu au zaidi wakiamini kuwa linamwepusha mtoto na mabalaa mengi.
Uzungu umetuharibu na kutupofusha na kugandisha ufahamu wetu.... Leo unapozungumzia hizi habari kama hazina majina ya kizungu ama link yake basi inaonekana ni habari ya kiswahili na ya kupuuzwa
 
cactus mkuu!
hope mshana ataelezea vizuri,kuna jamaa yangu ni mzungu m`italiano alinipa hizo skills kuwa niupande mbele ya nyumba,wachawi kwangu watakuwa wanapaona kama kwa baba mkwe,ni kweli tangu niupande sijawahi pata bughudha yeyote kutoka kwa walozi...
Ni lile lenye miiba ambalo hutumiwa kwenye Practical sekondari au?
 
Hili laweza kuwa geni kwako ama la unalijua kwa jina lingine.. Hili ni tofauti kabisa na gugu maji ambalo ni maarufu kwa wengi
Hapa ni gugu chawi kiboko ya mimea jamii ya kunde mahindi na Mwele...

Lakini kubwa zaidi ni kwamba gugu chawi aka purple witch weed punje zake ni hatari mno kwa wadanganyifu.. Watu wa Arusha wanalijua hili vema
Yani kama kuna jambo lina utata na mtuhumiwa hataki kunyoosha maelezo basi punje moja tu akipewa hutosha kabisa kumchanganya akili yote na kufunguka hasa.... Yani ataongea kila kitu
Lakini pia cha kushangaza mno ni kwama Mkundekunde unapendwa sana na wachawi katika shunghuli zao ...
mshana Jr, asante kwa kutufahamisha gugu chawi au Striga Hermonthica kwa jina la kitaalamu.

Pamoja na hasara zake za kuangamiza mazao ya chakula na biashara kwa binadamu pia una faida kama mmea dawa. Hutumiwa kutengeneza dawa ya kutibu kisukari, magonjwa ya ngozi, ukoma, vidonda ndugu, homa ya mapafu na manjano, nk, mbali ya kutumiwa na wachawi.

Lakini, faida hizo haziwezi kulinganishwa na hasara yake ya kuangamiza mazao.

Ni gugu ambalo ni gumu sana kuangamizwa kwa kuwa mbegu zake husambazwa kirahisi kwa njia nyingi kama vile upepo, mtiririko wa maji ya mvua, na wanyama.

Njia sahihi ya kuliangamiza gugu hili ni kuling'oa mapema kabla maua hayajaanza kutoa mbegu zilizokomaa.
 
Mkuu mshana jr,
Mbona picha ya kwanza ni tofauti na hii?? Tushike lipi kwani ninavyojua ile picha ya kwanza ndo yenyewe. Angalia rangi ya maua
Ni kweli kabisa Picha ya kwanza ni kipindi cha mvua hapo kila mmea hustawi inapokuja kipindi cha kiangazi gugu chawi hunyonya mimea mingine
5c0454e6d7671c0aa5c31d5e238ec0d2.jpg
a55045cbe08381a8b28c51325a9593d7.jpg
angalia hata majani ya rangi ya maua vinatofautiana Lakini ni Specie ile ile
 
mshana Jr, asante kwa kutufahamisha gugu chawi au Striga Hermonthica kwa jina la kitaalamu.

Pamoja na hasara zake za kuangamiza mazao ya chakula na biashara kwa binadamu pia una faida kama mmea dawa. Hutumiwa kutengeneza dawa ya kutibu kisukari, magonjwa ya ngozi, ukoma, vidonda ndugu, homa ya mapafu na manjano, nk, mbali ya kutumiwa na wachawi.

Lakini, faida hizo haziwezi kulinganishwa na hasara yake ya kuangamiza mazao.

Ni gugu ambalo ni gumu sana kuangamizwa kwa kuwa mbegu zake husambazwa kirahisi kwa njia nyingi kama vile upepo, mtiririko wa maji ya mvua, na wanyama.

Njia sahihi ya kuliangamiza gugu hili ni kuling'oa mapema kabla maua hayajaanza kutoa mbegu zilizokomaa.
Asante sana mwengeso nimeongeza ufahamu hapa ....pamoja na mapungufu yake Lakini linaweza kuwa na faida nyingi kumbe thanks again
 
Tafuta makala ya kitafiti iliyoandikwa na Koua, F.H.M. (2011): Striga hermonthica (Del.) Benth: Phytochemistry and pharmacological properties outline, Journal of Applied Pharmaceutical Science O1(07), pp 01-05
 
Leo tafanya hivyo kwakweli, it takes few mbs to gain a very crucial education ili ije iwe msaada kwa wengi
 
Back
Top Bottom