Lifahamu Gugu chawi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
Hili laweza kuwa geni kwako ama la unalijua kwa jina lingine.. Hili ni tofauti kabisa na gugu maji ambalo ni maarufu kwa wengi

Hapa ni gugu chawi kiboko ya mimea jamii ya kunde mahindi na Mwele
Majina mengine ni haya hapa viduha, kakindu, kichawi dume na kidevu cha mbuzi
Huku kwa kiingereza likijulikana kama witch weed (striga hermonthia -botanical name)... Mmea huu unapatikana zaidi Africa, bara Hindi na Australia

Kwanini nimekuleeni Leo gugu chawi na maelezo marefu? Gugu chawi ni tofauti na magugu mengine ambayo huzonga tu mimea. Gugu chawi lenyewe hupenyeza mizizi yake kwenye mimea tajwa hapo juu na kuifyonza chakula chote na kuufanya mmea ufe kabisa

Lakini kubwa zaidi ni kwamba gugu chawi aka purple witch weed punje zake ni hatari mno kwa wadanganyifu.. Watu wa Arusha wanalijua hili vema. Yani kama kuna jambo lina utata na mtuhumiwa hataki kunyoosha maelezo basi punje moja tu akipewa hutosha kabisa kumchanganya akili yote na kufunguka hasa.... Yani ataongea kila kitu

Lakini pia cha kushangaza mno ni kwama Mkundekunde unapendwa sana na wachawi katika shunghuli zao Lakini kiboko yake huu mmeapendwa na wachawi ni gugu chawi
Je kuna vita ya Kiroho na nguvu ya giza hata kwenye mimea?

TUTAJADILI HILI SOON BTW hatufundishani uchawi tunapanua ufahamu

1296.400x400_2.jpeg
 
Witch weed, nakumbuka enzi za agriculture. Manhot esculenta, Dativa sp.
Hilo gugu ni balaa likiingia shambani kwako, inakubidi uling'oe lingali changa halijatoa maua/mbegu na ulitie motoni.

Mpambano kiroho...mmmmmmh m mkuu ngoja wajuvi waje
 
Mkuu MziziMkavu kuna Mmea mwingine ambao huota hasa pembezoni mwa mito na chemchemi! Mmea huu uko kwa namna mbili mmoja unatoa maua yenye rangi ya dhahabu,na mwingine una maua mekundu yaliyokolea!! Na una miiba midogomidogo! Pia hutoa matunda madogo ambayo yakiiva huwa na rangi nyeusi!! Mkuu Mmea huu ni tool muhimu sana kwa wachawi!! Nakumbuka miaka ya 80's tukiwa peramiho ilipita operesheni ya kuiteketeza mimea hii!! Hata hivyo siku hizi imepungua sana! Nikipita mtoni nitaipiga picha nikutumie!
 
Mkuu MziziMkavu kuna Mmea mwingine ambao huota hasa pembezoni mwa mito na chemchemi! Mmea huu uko kwa namna mbili mmoja unatoa maua yenye rangi ya dhahabu,na mwingine una maua mekundu yaliyokolea!! Na una miiba midogomidogo! Pia hutoa matunda madogo ambayo yakiiva huwa na rangi nyeusi!! Mkuu Mmea huu ni tool muhimu sana kwa wachawi!! Nakumbuka miaka ya 80's tukiwa peramiho ilipita operesheni ya kuiteketeza mimea hii!! Hata hivyo siku hizi imepungua sana! Nikipita mtoni nitaipiga picha nikutumie!
Huo mmea unaitwa devil thorn plant /mmea wa miba za shetani .....picture coming soon
81e9dbdc1d3fbe7d750ceec80658950d.jpg
miba yake ikikauka huwa hivi
 
Kuna UA niliambiwa ukiliotesha nyumbani wachawi hawawezi kufanya yao ila sijui ni UA gani hilo
cactus mkuu!
hope mshana ataelezea vizuri,kuna jamaa yangu ni mzungu m`italiano alinipa hizo skills kuwa niupande mbele ya nyumba,wachawi kwangu watakuwa wanapaona kama kwa baba mkwe,ni kweli tangu niupande sijawahi pata bughudha yeyote kutoka kwa walozi...
 
Dawa ya gugu hilo ni kupanda mihogo katika eneo husika kwa mda wa miaka kadhaa japo haliwezi kuisha asilimia 100 maana huzaliana kuliko kawaida!
 
Hii ndio Jf ya miaka ya nyuma.gugu chawi itakuwa ndio lililokula rambirambi za Marehemu
 
Back
Top Bottom