LICENSE TO KILL: Maslahi mapana ya taifa yanapozingatiwa!

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,794
Kutoa roho ya mtu ni tofauti kabisa na kutoa roho ya mnyama ama mdudu. Kwa mnyama sana sana unaweza kulipishwa fidia hasa kama mnyama mwenyewe ni kwa ajili ya utalii.

Kutoa roho ya mtu ukiachana na ule ugomvi wa papo kwa papo kunahitaji maandalizi yake! Na wengi kwenye hayo maandalizi hukosea kitu kidogo sana na hatimaye kujulikana, kukamatwa kufunguliwa mashtaka na hatimaye kuhukumiwa kifo ama vifungo vingine! Kuachiwa huru ni aghalabu!

Kwa kuzingatia hili kuna kaliba ya watu kwenye mataifa mbalimbali, kwa kuzingatia sheria wamepewa kibali cha kuua pale wanapoona maslahi na usalama wa Taifa vinahatarishwa! Wauaji hawa ni tofauti kabisa na polisi na wanajeshi japo wanaweza kuwa kwenye hayo mavazi. Hawa hawaui kwa uwazi labda mpaka njia zote zinaposhindikana kabisa na muda hautoshi.

Hawa huua kwa siri ama kwa kificho na kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, halafu wanaohusika na usalama wa raia hutengeneza story kama ikibidi kufanya hivyo.

Kuna vitengo vitatu vinahusika kwenye usalama na vyote hufanya kazi kwa kutegemeana ama kushirikiana katika baaadhi ya maswala yahusuyo usalama na mengine hufichana kwa sababu maalum.

Kuna usalama wa raia---- POLISI
Kuna usalama wa nchi ----JESHI
kuna usalama wa taifa --- JESHI + POLISI + RAIA
Usalama wa taifa ndio admin wa maswala yote ya ndani na ya nje ya usalama wa nchi. Hawa wako kila mahali na juu ya kila kitu. Lakini utendaji wao ni chini ya zulia ama nyuma ya pazia. Na hawa ndio wana kibali maalum cha kuua kwa maslahi na usalama wa taifa.

Usalama wa taifa kimsingi na kiasili hauchangamani kwa namna yoyote na siasa wala wanasiasa, bali wao wapo kuwachunga na kuwaongoza! Siasa huja na kubadilika lakini usalama wa nchi na taifa hubaki vilevile kwa nyakati zote. Hivyo utendaji na watendaji wake ni vya kaliba ya juu mno, na ndio maana kazi zake si za kutangazwa kwenye vyombo vya habari bali hupatikana kwa mchakato mrefu na mgumu

Kibali cha kuua hakiko kwa watu wa kawaida tu pale inapoonekana kuna kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuhujumu nchi, kiusalama, kiuchumi na hata kijamii pia. Kibali hiki kiko hata kwa watu wa kaliba ya juu kama wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa mashuhuri, wana sanaa nguli, viongozi mbalimbali wa kijamii na hata wa kidini.

Kimsingi ni kwamba wewe bila kujali nafasi na umuhimu wako kwenye jamii na taifa kwa ujumla, ukianza kuleta zako wanakula kichwa

Ukionekana wewe ni kitisho kwenye usalama wa taifa na nchi
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye amani ya nchi na taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye umoja na mshikamano wa taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye uchumi wa nchi na taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye nyanja zingine zozote zenye maslahi ya nchi na taifa basi tambua wazi huna maisha marefu.

Usalama wa taifa ndio engine ya nchi, hawa hawako tayari kuona gari linashindwa kusonga kwasababu ya tairi, gearbox, shockup ama kifaa kingine chochote. KIBOVU KITABADILISHWA FASTA!

NB: Just a general discussion. Not aiming anything specific!
 
Unataka kusema bwana yule alimalizwa na hawa watu

Halafu kuna rais mmoja wa Zanzibar ambae sasa hivi hatajwi popote na yeye nasikia aliwekwa pembeni na hawa mabwana
Haya mengi huwa ni off records lakini kila jambo huwa na asili au chanzo kisha huja mchakato na mwishoni matokeo tarajiwa. Achan na kelele za mitandaoni. Kuna yasiyosemwa wala kuandikwa popote lakini yapo na yanatekelezwa kwa mtindo wa aina yake! Majibu mnayapata tu kwenye matokeo!
 
Kulikoni mbona leo umekuka na kitu ngumu kumesa, ila naamini sisi washirikina hatupo kwenye list.
 
Kulikoni mbona leo umekuka na kitu ngumu kumesa, ila naamini sisi washirikina hatupo kwenye list
hata wafia dini wana vitengo vya ushirikina.. Washirikina tupo popote pale ..ni kama ngozi na mfupa
 
Mbona Mseveni na Kagame wanakula bata lakini wakwetu wqkatumia mzana.Je wakwetu alikuwa anahatarisha au kwakuwa alifuatailia mambo ya wakubwa wenzake?



Kutoa roho ya mtu ni tofauti kabisa na kutoa roho ya mnyama ama mdudu... Kwa mnyama sana sana unaweza kulipishwa fidia hasa kama mnyama mwenyewe ni kwa ajili ya utalii
Kutoa roho ya mtu ukiachana na ule ugomvi wa papo kwa papo kunahitaji maandalizi yake! Na wengi kwenye hayo maandalizi hukosea kitu kidogo sana na hatimaye kujulikana, kukamatwa kufunguliwa mashtaka na hatimaye kuhukumiwa kifo ama vifungo vingine! Kuachiwa huru ni aghalabu....!!!

Kwa kuzingatia hili kuna kaliba ya watu kwenye mataifa mbalimbali, kwa kuzingatia sheria wamepewa kibali cha kuua pale wanapoona maslahi na usalama wa Taifa vinahatarishwa! Wauaji hawa ni tofauti kabisa na polisi na wanajeshi japo wanaweza kuwa kwenye hayo mavazi... Hawa hawaui kwa uwazi labda mpaka njia zote zinaposhindikana kabisa na muda hautoshi!!!! Hawa huua kwa siri ama kwa kificho na kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, halafu wanaohusika na usalama wa raia hutengeneza story kama ikibidi kufanya hivyo

Kuna vitengo vitatu vinahusika kwenye usalama na vyote hufanya kazi kwa kutegemeana ama kushirikiana katika baaadhi ya maswala yahusuyo usalama na mengine hufichana kwa sababu maalum

Kuna usalama wa raia---- POLISI
Kuna usalama wa nchi ----JESHI
kuna usalama wa taifa --- JESHI + POLISI + RAIA
Usalama wa taifa ndio admin wa maswala yote ya ndani na ya nje ya usalama wa nchi..hawa wako kila mahali na juu ya kila kitu.. Lakini utendaji wao ni chini ya zulia ama nyuma ya pazia.. Na hawa ndio wana kibali maalum cha kuua kwa maslahi na usalama wa taifa

Usalama wa taifa kimsingi na kiasili hauchangamani kwa namna yoyote na siasa wala wanasiasa .. Bali wao wapo kuwachunga na kuwaongoza! Siasa huja na kubadilika lakini usalama wa nchi na taifa hubaki vilevile kwa nyakati zote... Hivyo utendaji na watendaji wake ni vya kaliba ya juu mno, na ndio maana kazi zake si za kutangazwa kwenye vyombo vya habari bali hupatikana kwa mchakato mrefu na mgumu

Kibali cha kuua hakiko kwa watu wa kawaida tu pale inapoonekana kuna kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuhujumu nchi, kiusalama, kiuchumi na hata kijamii pia.. Kibali hiki kiko hata kwa watu wa kaliba ya juu kama wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa mashuhuri, wana sanaa nguli, viongozi mbalimbali wa kijamii na hata wa kidini...
Kimsingi ni kwamba wewe bila kujali nafasi na umuhimu wako kwenye jamii na taifa kwa ujumla, ukianza kuleta zako wanakula kichwa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye usalama wa taifa na nchi
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye amani ya nchi na taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye umoja na mshikamano wa taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye uchumi wa nchi na taifa
Ukionekana wewe ni kitisho kwenye nyanja zingine zozote zenye maslahi ya nchi na taifa basi tambua wazi huna maisha marefu...
Usalama wa taifa ndio engine ya nchi ...hawa hawako tayari kuona gari linashindwa kusonga kwasababu ya tairi, gearbox, shockup ama kifaa kingine chochote... KIBOVU KITABADILISHWA FASTA....!!!!!
 
Mbona Mseveni na Kagame wanakula bata lakini wakwetu wqkatumia mzana.Je wakwetu alikuwa anahatarisha au kwakuwa alifuatailia mambo ya wakubwa wenzake?
Just a general discussion.. Not aiming anything specific!... Ndio maana sijataja taifa lolote...!!!
 
Mbona Mseveni na Kagame wanakula bata lakini wakwetu wqkatumia mzana.Je wakwetu alikuwa anahatarisha au kwakuwa alifuatailia mambo ya wakubwa wenzake?
Sizani kama.mada inahusu hilo kundi mshana kuja huku wanakutoa lwenye reli
 
Back
Top Bottom