umeongea kinyume kaka, hakuna waasi libya ila NTC walikuwa waasi kwa gaddafi
lakini sasa hiyo ni NEW GOV ya libya na leo wamekabiziwa kiti chao rasmi UMOJA WA NCHI ZA AFRIKA
au hujui maana ya waasi? hata nyerere alikuwa muasi mbele ya mkoloni, tumia bichwa hilo sio kukariri maneno
Wale wote wanamuona Gadhafi kuwa kaonewa waangalie raia wa Libya. Libya sio Tanzania wala Libya sio Kenya ,Libya niya ya raia wa Libya wenyewe.Kamwe Mpe kila Kitu Mwanadamu lakini usimnyime uhuru wake,ndio maana wenye akili zao [THINK BIG} wamempa Jakaya Kikwete zawadi ya DK kwa kuwa wanajua mchango wake kwenye haki na ujenzi wa demokrasia,leo hii mimi na wewe tuko kwenye uelewa huu,yeye kama yeye angeweza kuwa mbabe tu kama Rais alie pita.Lakini kwa upande na uwezo wake kaamua waache wanatanzania wajue ukweli kisha wataamua wao.
Walibya walipewa kila kitu lakini wakakosa uhuru wao, uhuru wa siasa,uhuru wa kujieleza na uhuru wa kuamua ambao ni haki ya kila raia yoyote chini ya uso wa dunia kwa kuwa siasa ni sehemu ya maisha ya wanadamu.
Leo hii ni kweli kama wewe na mimi ni moja ya watu wanao fikiri zaidi [THINK BIG] hapa Nchini usione Watanzania wanafumuka
KIUFAHAMU hivi walivyo ukafikiri imekuja hivi hivi. Uhuru huo sio vya kuelea ni gharama kubwa sana kuna tafiti halisi nyingi zimefanyika [Research] juu ya nini kifanyike ili kupanua demokrasia na uhuru wa watanzania kujua Nchi iendeshweje huku kukiwa na mvutano wa kimakundi katika jamii,kama Mafisadi dhidi ya Umma,Bunge dhidi Ya Serikali,Serikali dhidi ya Wananchi na Vyama vya Kisiasa,Vyama vya Kisiasa na Umma,Makundi ya Kijamii na asasi za kiraia dhidi ya Serikali na umma,Mafisadi dhidi ya vyama vya kisiasa na kada nyingine za kiuchumi.
Hayo yote hayakuibuka bali yalifanyiwa utafiti kabla ya leo kuyaona yakiendelea,kwa kuwa kuna kitu kinaitwa STEREOTYPE sijui tafsri yake kiswahil lakini ni juu ya tabia halisi za kijumla za jamii, inajulikana kuwa Mnaigeria ni agrressive and louder,Mmarekani ni mshindani [Competitors], Leader na kimbelembele na ,Mwingereza ni boastful na Superior, Mkenya nae ni agrressive, watanzania ni wapole, na wasikivu, wavumilivu,wasio jali lakini wasioeleweka [Unidefined].
Kwa wataalamu hii ni kazi sio swala la kukulupuka na ukipata Rais msikivu na mwelewa wa tabia za raia wake basi Nchi ndio unasikia I
NAFANIKIWA SANA [PROSPER].
Uhuru tulio nao kuna viongozi wengine wanamzodoa Kikwete kuwa kashindwa lakini
UKWELI KASHINDWA KWA KUWA KATUACHA NA UHURU KUAMUA WENYEWE.Nchi haitawaliwi na Rais pekee bali pia kuna matabaka ya kimfumo na kama wanataaluma, wasomi, ambao hawajasoma,wakulima,wafanyakazi,watoto,wakina mama,wakina baba,vijana, wafanyabiashara wadoggo kwa wakubwa na nk.Ili taarifa likue kama mtoto Mdogo anavyotoka kutambaa mpaka kusimama na baade kuongea na kukimbia na kuwa Mtu kwenye jamii ndivyo vivyo Taifa linavyopita.Migongano na mifumuano kwenye Taifa ndio zao la Taifa kutoka hatua moja ya maendeleo.Hivyo kwa tabia za raia wa Nchi ndio uamua Mwenendo mzima wa misuguano ya kijamii kuwa njia zipi zitaibuka katika misuguano hiyo katika kudai haki za kimakundi na hatimae haki za Kitaifa.
Kikwete angeweza kwa uamuzi wake kuzuia kwa nguvu taarifa zozote za muhimu juu ya chochote anachoona ni cha hatari kwa Serikali yake
1: Angeweza kuwa Mkali [Strictly=Purely] kwa uhuru wa habari,taarifa na ufahamu [Ambao ni kitu Muhimu kwa ustawi wa Taifa lolote lile]
2: Angeweza kuwa Mtawala mmbabe kwa raia na yoyote atakae msema vibaya hivyo akawa anataka kusikia mazuri ya kusifiwa tuu.
3: Ama kuchagua la kuwa Mwenye kuuma na kupuliza kwa kuangalia nani zaidi kati ya Umma na Watawala na Washirika wa Kiutawala kikundi kidogo.
4: Ama angeweza kuamua kushirikiana na washirika wa watawala yaani kikundi kidogo cha wachache kuamua kuitafuna Nchi wo kama wao.
5: Ama angeamua kushirikiana na Umma [Majority] Kama Mwalimu Kujenga Nchi kwa kuangalia raia mmoja mmoja atafanikiwa vipi na kuwa na ustawi wake kama mwenye mchango katika Taifa.
6: Angeweza kuamua kuwa mfalme na kuanza kuunda mfumo wa namna ya kuwalithisha wanafamilia yake pindi akitaka kutoka madalakani.
Hayo yote ni uamuzi wa Rais kama yeye kwa kuwa amekuwa vested na Wananchi.Japo kwa kuabuse mamlaka aliopewa na wananchi ndipo misuguanao ya kimaslahi kati yake na walio mpa mamlaka hayo unapoibuka.
Ndio kuna maeneo ambayo Jakaya Kikwete ametenda ndivyo sivyo lakini kwa wenye upeo wa falsafa za maisha wanaona ndio na yeye kafikia uwezo au kikomo chake kibinadamu ulipofika na mapungufu yake kama binadamu. Mfano sehemu ambayo angepaswa kuwa mkali na kuamua amebaki kuwa mpole wa tabia ya kitanzania na asieleweka [Undefined] .Na kingine ukiludi kwenye tabia ya jumla ya
Watanzania,upole, uvumilivu na kuwa mtu usie eleweka kwa kutenda au kunena [Undefined].
Na kwa sasa raia wa Tanzania kupitia style ya uendeshaji Nchi wa Rais Kikwete Rais ajae Umma unataka Kuona ni Rias asie na Mzaa,hivyo kama wanataka Rais asie na mzaa sio kuwa hana mzaa na mafisadi bali hana mzaa na yoyote yule kwenye swala la sheria, haki na wajibu hakika ukiambiwa usikojoe hapa kisha ukakojoa ukitegemea yaleyale ya Kitanzania mwanangu poa, imekula kwako.Kila raia itabidi kutimiza sheria ukiambiwa usijenge hapa maan iwe hiyo.Ila katika mivutano ya kitabaka CCM kuendelea kuibua tabia ya kukumbatia siasa za kimakundi zimeonyesha kuwa Tanzania haitaki siasa za kimakundi na siasa za watu kujilimbikizia Mali kwa njia za kuibia Serikali na Udanganyifu kwa Umma.
Hivyo Gadhafi, Sadam ni matokeo ya walichokijenga wenyewe ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga,what goes around comes around,dunia hii mtawala atakae tawala na kuishi vyema ni yule atakae tawala kwa kutetea Raia zake walio wengi [Majority] na si kuunda kakundi ka watawala kuwadhulumu walio wengi ambacho ndicho kitu Mwalimu alikiona kabla ya uhuru na baada ya uhuru na maisha yake yote akiwa hapa dunia.