Swali, je makampuni yanayonunua madeni ya serikali yanapata manufaa gani?
Mimi nielewavyo ktk nchi zilizoendelea kuna makampuni kazi yake kununua madeni sugu kwa bei pungufu kutoka kwa mdai na kisha kampuni nunuzi ya madeni kuchukua mzigo wa kuhakikisha inalipwa pesa zote toka kwa mdaiwa ( hapa Mohammed Enterprise na kina-MMN watailipa Libya pesa pungufu halafu kuikomalia serikali ya Tanzania ilipe deni lote).
Sasa basi kama ndivyo ilivyo, je serikali ya Tanzania ina uwezo wa kuilipa Moh'd ent. au MMN kiasi gani na serikali ya Tanzania itapata unafuu gani kudaiwa na Moh'd Ent/ MMN deni hili litakalouziwa na serikali ya Libya kwa makampuni ya ki-Tanzania? Je serikali ya Tanzania italipa hawa watarajiwa wa ununuzi wa deni kwa pesa za Shillingi za Tanzania au kwa pesa za kigeni? au watapewa migodi au madini n.k kama malipo ya deni hili lililoshindikana? Jambo hili linahitaji kufafanuliwa kwa undani jinsi Moh'd ent au MMN watakavyolipwa na serikali hii iliyofilisika ya Tanzania na walipa kodi watabebeshwa zigo gani?.
Nadhani unahitaji darasa la Debt Swap maana inaonekana ni concept mpya kabisa kwako. Lakini ukweli ni kwamba kununua deni kunakupa hela ambazo riba yake ni ndogo kuliko ukikopa benki maana inerest ya benki wakati mwingine hufikia hata 25% wakati hili linaweza kuwa 8% tu. Hii inahitaji kampuni inayonunua kuwekeza katika miradi iliyochaguliwa hapa nchini kama vile viwanda au kilimo kwa nia ya kuongeza ajira na uuzaji bidhaa nje.