Libya yazima Mohammed Enterprises | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Libya yazima Mohammed Enterprises

Discussion in 'International Forum' started by nngu007, Jun 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Na Jabir Idrissa; MwanaHalisi

  [​IMG]


  UBALOZI wa Libya jijini Dar es Salaam umekana mahusiano yoyote na kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL) na mshirika wao Massoud Mohamed Nassr.

  Hatua hii inaziba mwanya wa kampuni hiyo kujipatia sehemu ya dola 121.9 milioni (sawa na kiasi cha Sh. 180 bilioni) ambazo inadaiwa ni deni la Tanzania kwa Libya linalotokana na mkopo wa mafuta.

  Fedha hizo zilitarajiwa kuchotwa kwa mtindo wa EPA wa kununua madeni yaliyoshindikana kutoka benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Tayari ubalozi umeiarifu serikali kuhusu suala hilo na nakala ya barua yake kupelekwa mahakama kuu ambako mashauri mawili yamefunguliwa na MeTL.

  Taarifa kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam zimeeleza kuwa hata ofisi hiyo tayari imetaarifiwa kuhusu suala hilo.

  Nyaraka ambazo MwanaHALISI limepata zinaonyesha kuwa mfanyabiashara maarufu wa chakula nchini, Gulamabbas Hassanali Fazal Dewji anataka kujipatia mabilioni ya shilingi kutokana na kile kilichoitwa kuuziana madeni sugu kati ya serikali za Tanzania na Libya.

  Vyanzo madhubuti vya habari vimelieleza gazeti hili kuwa serikali imezuia malipo ya mabilioni ya shilingi ambazo mfanyabiashara huyo amekuwa akijitahidi kuyadai kupitia kesi mbili alizofungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Dewji ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Mohammed Enterprises (T) Limited (MeTL), anadai zaidi ya dola 20 milioni kupitia kesi Na. 127 ya 2009 na kesi Na. 110 ya 2010.

  Wakati kesi Na. 127 ambayo MeTL ilimshitaki raia wa Libya aitwaye Massoud Mohamed Nassr au Masoud M. Nasser, iliamuliwa 26 Mei 2011, kesi Na. 110 haijasikilizwa.

  Katika uamuzi wa kesi ya awali inayodaiwa kuhusu mkataba wa kuuziana deni, Jaji Augustine Mwarija aliamuru pande husika zigawane mapato pamoja na riba yaliyotokana na uuzaji wa dhamana za serikali zinazoshikiliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Mapato hayo yanafikia Sh. 6,640,550,960 ambapo uamuzi wa Jaji Mwarija unaelekeza kuwa MeTL itaingiziwa kwenye akaunti yake Sh. 3,320,275,480.

  Lakini, kulingana na nyaraka zilizopatikana, hata mapato hayo si halali na serikali imezuia malipo.

  Serikali ya Libya, ambayo MeTL imeishitaki kama mdaiwa wa kwanza katika kesi Na. 110, imekataa kutambua mpango wa kuuziana deni la dola 121,900,000 ambalo linadaiwa kutokana na Tanzania kushindwa kulipa mkopo tangu mwaka 1983.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameiambia MwanaHALISI kwamba wizara yake haitambui makubaliano ya MeTL na Nasser na haioni uhalali wa madai yao.

  Membe ambaye alizungumza na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam juzi Jumatatu, alisema wizara yake tayari imemjulisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa serikali ya kigeni haiwezi kushitakiwa na Mtanzania kwa mikataba ambayo haikuidhinishwa.

  "Serikali ya nje haiwezi kushitakiwa bila ya kuwa na nyaraka za serikali zilizosainiwa na watu wenye kutambuliwa katika mikataba. Huyu hajalipa fedha na hana mkataba… (kama ni) deni lazima linunuliwe na serikali na kuna masharti ya kulipa," alisema.

  Akigusia maelezo yaliyotolewa na ubalozi wa Libya nchini, waziri Membe alisema ni maelezo sahihi na kwamba msimamo wa serikali ni kutokuwepo sababu yoyote wala uhalali wa kuishitaki serikali ya Libya katika suala hilo.

  Alisema Mlibya anayedaiwa kufunga mikataba ya kuuziana deni na MeTL linalohusu mafuta ambayo serikali ya Libya iliiuzia Tanzania, hakuwa na hata sasa hana mamlaka ya kuiwakilisha serikali ya Libya katika jambo lolote na "hakuwa na mkataba wowote kati ya serikali ya Libya na MeTL."

  MeTL imeishitaki Libya kama mdaiwa wa kwanza katika kesi Na. 110. Ubalozi wa Libya unasema hautambui mpango wa kuuziana deni la dola 121,900,000 uliobuniwa na MeTL kutokana na Tanzania kushindwa kulipa deni lake linalotokana na Libya kuiuzia serikali ya Tanzania mafuta kwa mkopo.

  Ubalozi wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Watu wa Libya jijini Dar es Salaam, imeeleza kwamba haitambui makubaliano ya aina yoyote kati ya serikali ya Libya na MeTL au anayejiita mwakilishi wa serikali ya Libya.

  Akijibu takwa la kuitwa shaurini mahakama kuu, ofisa wa ubalozi wa Libya anaeleza waziri wa mambo ya nchi za nje Tanzania kuwa serikali yake haijawahi kuipeleka Tanzania mahakamani.

  Katika hati yake ya maelezo yenye Kumb. N/REF 7/2/2250 ya tarehe 20 Mei 2011, ambayo nakala yake ilipepekwa mahakamani, ubalozi wa Libya unasema, katika mahusiano yake ya nje ya nchi – yawe ya kisiasa au kiuchumi – huwa inashughulika na serikali wala si mtu au taasisi binafsi hasa suala lenyewe linapohusu deni kwa biashara ya mafuta.

  "Libya, katika suala hili (la kuuza mafuta), inazingatia muktadha wa udugu na Tanzania, unaotokana na uhusiano mzuri wa kisiasa tulionao. Tunaamini Libya haistahili kushitakiwa na kampuni hii kutokana na suala hili," inasema hati hiyo.

  Serikali ya Libya, unaeleza ubalozi wake, haijapata kusaini au kuidhinisha mkataba wowote wa kibiashara na kampuni inayodai katika kesi tajwa.

  Inasema, "Ni muhimu ukafahamu kuwa mamlaka inayostahili kuiwakilisha serikali ya Libya katika Tanzania ni ubalozi wa Libya na si yeyote mwingine; iwe kwa kusaini mikataba au kuiidhinisha pale inapotokea…"

  "Ubalozi wa Libya unaiomba mahakama tukufu kutoendekeza madai haya dhidi ya Libya. Tuna matumaini makubwa ya busara na hekima kutumika katika kutenda haki kuhusu kesi hii," ameeleza wakala wa serikali ya Libya.

  Maelezo ya serikali ya Libya yaliwasilishwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kwa barua ya wizara ya mambo ya nje tarehe 30 Mei 2011 yenye Kumb. Na. GA 226/336/78 iliyosainiwa na Abdallah M. Mtibora kwa niaba ya katibu mkuu wa wizara hiyo.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kikwete hakupigana Vita vya Uganda akiwa Jeshini? haoni kuwa Ghadaffi kwa kumsaidia Amin Uchumi wa Tanzania Ulidhoofika sababu ya kununua silaha kwa third party? Tanzania kabla ya vita hatukuwa na Deni IMF; Nchi ilikuwa na Foreign Currency Reservers; after War everything went Wrong

  Sasa tunamkumbatia Ghadaffi na kutupa misaada ya kujenga Misikiti kwa Mkopo; we have to pay them later? what is this?
   
 3. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hii kitu itakuja kufumua mambo mengi sana hapo baadaye
  harafu hivi bado TUNA UBALOZI wa libya?

  jk bwana anataka kutuweka katika gunia lipi UN au EU wakitununia
  au bado anapima nguvu kama alivyofanya kwenye suhala la serengeti
  kuna faida gani kubwa kiasi cha kuhatarisha mahusiano yetu ya kimataifa
   
 4. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  sasa nimeanza kupa picha kwa mbaliiiiiiii kwa nini jk na maaskofu ni paka na panya
  yawezekana walishamwambia madeni kama haya yalipwe kwa ZAKA na SADAKA za BAKWATA
   
 5. k

  kaiya Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kumbe ghadaffi anatupa misaada ya kujenga misikiti!!! mimi hili nilikuwa silijui
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hivi Kikwete hakupigana Vita vya Uganda? Kwanini bado tuna Ubalozi wa Libya? hakuona Maumivu wakati wa hivyo vita; Ilitushushia GDP na pia tulilazimishwa kununua silaha kwa bei kali through a third party... Tanzania kabla ya VITA tulikuwa na enough foreign currency reserves hatukuwa na deni IMF after the war kila kitu kikaanguka...

  Sasa Kikwete anamkumbatia Ghadaffi anatupa pesa za kujenga Misikiti kwa Mkopo tuna Madeni nao -- Is it shame on US? Kweli Tanzania soon we will see the results of AZIMIO LA ZANZIBAR
   
 7. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Nchi hii ya Tanganyika kuna vioja vingi mno na bado tutajionea mengi tu
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wakuu ni msikiti gani wajengwa kwa pesa za Libya ? Yaani kesha hama Iran na sasa ni Libya ?Haya wacha tuangalie mwisho wake .
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Misikiti ya Iran na Saud Arabia yana Masharti Makali
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Jun 26, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  misiki iliyojengwa pembezoni mwa barabara ya Iringa ! Toka Moro hadi Mbeya.
   
 11. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Dodoma pia Gadafi kajenga msikiti mkubwa sanaa..
   
 12. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Maskini vipofu! Watu mnathubutuje kuchangia kitu ambacho hamkijui, halafu mnadai deni hili aliliingia JK ili kujenga msikiti? Kwa taarifa yenu, denu hili Tanzania ililiingia mwaka 1983, pale tulipoagiza mafuta ya thamani ya dola kama 42 milioni. Deni lilivuta riba mpaka kufikia dola 202 milioni na wakati wa serikali ya Mkapa ndipo juhudi za kulilipa deni hili zilianza kwa majadiliano yaliyofanikisha kufutwa kwa deni hili kwa 50% na iliyobaki ndiyo ambayo ilitengenezewa mpango wa malipo kwa kutumia dhamana za serikali, pamoja na kununuliwa na wafanyabiashara watakaoendesha miradi itakayopitishwa na serikali ya Libya yenyewe. Kujitokeza kwa Mohamed Enterprises na wafanyabiashara wengine ni matokeo ya mpango huo na utekelezaji ambao mikataba yake ilisainiwa mwaka 2005 October. Kwa hiyo wandugu, ni vizuri tukaelewa kwamba deni hili liliingiwa na uongozi wa awamu ya kwanza, miaka minne baada ya vita vya Amin ambavyo inadaiwa Gadaffi alimsaidia Amin, na kinachotokea leo ni utekelezaji wa makubaliano hayo ya awamu ya kwanza na baadae majadiliano ya awamu ya tatu ya uongozi. Kama kuna msikiti umejengwa na Libya, havina uhusiano na mpango huu, wala fedha hizi!
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Masharti gani hayo mjomba?
   
 14. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mzee haigharimu kitu kwa kukaa kimya kama hujui kitu. Infact ungeheshimiwa sana! Sasa tunashuku uwezo wako wa kukusanya taarifa zenye usahihi.
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Hivi ndivyo tunavyoshasimamisha makampuni yetu sisi tunaojiita wazawa??? ni magumashi magumashi tu kwa kwenda mbele. Duuuh!
   
 16. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  An irresponsible and extremely inflammatory comment! Please shed some light if you a thing or two about your contention lest you assume a status of a busy body!
   
 17. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hii ina maana hata Jaji ni bomu anapashwa kutolewa ndani ya Mahakamani ya Tanzania
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Inategemea na jinsi kesi ilivyoendeshwa na kilichopelekwa mbele yake, unless una ushahidi kwamba money changed hands.
   
 19. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,057
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Naomba tu tunapojadili masuala muhimu ya nchi tuwe serious na tuachane na upotofu na dhihaka. Tangu lini Libya, Iran au hata Saudi Arabia zikajenga misikiti kwa deni? Au katika suala hili pia wataka utie udini wako wa kunuka?
  Sikulaumu wewe, nalaumu elimu mbovu uliyopata, au kama umesoma at all.
   
 20. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unajua ndugu yangu humu kuna watu wenye nia ya kuongeza idadi ya post zao bila kujali kile wanachochangia kina mchango gani kwa taifa au jamii. Halafu hili tatizo la udini linaelekea kuwatia upofu watu kiasi cha kushindwa kufanya tathmini ya mambo kwa macho mawili. Katika historia ya nchi hii serikali haijawahi kukopa kulipia masuala ya kiimani, lakini kwa bahati mbaya kwa sababu watu walidhani ni deni lilitokana na uongozi wa rais wanayemchukia kwa sababu zao basi wakadhani huu ni wakati wa kumtia 'hatiani' kumbe maskini ni deni linaloihusu awamu inayoheshimika sana, tena kwa masuala ya kimaendeleo kwa nchi yetu! What a shame for these irresponsible people.
   
Loading...