Jamani,kama deni hili ni la mwaka 1983 ni sawa,manake zama hizo ukweli matumizi yake hayakuchakachuliwa.Na kwa upeo wa Mwalimu JK,uwezo wake wa kumtumia yule ambae wengi wamemuona kama adui [IF YOU CANT DEFEAT THEM JOIN THEM],Nyerere aliweza kuishi na kuongoza Taifa liloheshimika kwa kutochaguliwa nini cha kufanya.Libya na mafuta yake ilikua ni kitu muhimu sana kuishi nao kwa umakini sana wa KIDPLOMASIA na pamoja tofauti zote za kumsaida Idd Amini kutupiga.
Bado Mwalimu aliyahitaji mafuta yake Ghadaf kuendeshea maisha yetu watanzania.Ndio maana ilifikia hatua yeye binafsi akapokea pesa kuwasaidia Watyama wenzake wenye imani ya Kiislamu kujenga msikiti pale Butiama,kwa nia njema ya undugu na si kwa nia mbaya kama ambazo zama hizi watu wanajalibu kutuonyesha sasa.
Hivyo hakika kama deni hilo ni la mwaka huo tajwa basi ni kweli.Hongera yangu ni kwa ubalozi wa LIBYA,kwa kuzuia dili hilo la kuchakachua kumature na kuongeza mzigo wa kilio cha umaskini wa watanzania.Ndio maana kidplomasia Tanzania imekaa kimya sana kwenye swala la LIBYA na siasa zake zinazoendelea kimataifa na NATO kusimamia mchakato mzima wa kumuondoa Ghadaf baada ya matendo yake ya gadhabu ya Walibya kupambana nae kumtoa yeye Ghadaf madarakani.
Kwa kuwa ndani ya mchakato huo wa kumuondoa Ghadf kuna Mheshimiwa [Nchi] nae kwa maswala ya Interest yuko makini na kwa kuwa nasi tuna interest zetu pia kama Nchi basi tumechuna kulaumu mateso wanayopata raia wa libya kwa kuwa mtendaji wa hayo ni swahiba wetu kimaslahi japo hatupendezwi na aliyoyatenda basi tutakaa kimya.
Ila usanii kutuibia kwa kusingizia kesi hizo nashukuru walibya kwa kushituka huko,vinginevyo wasingeshituka wao jamani watu wangechakachua pesa ya kula bata na kuandaa mazingira ya kumtafuta mkuu wa kusimamia missiontown na si kiongozi wa TAIFA.
Jamani hawa watu awaamini kuwa watu wameshashituka jamani,wanafuatilia kila dili wanalofanya.Haijalishi wewe ni nani,una madaraka gani siku watu wakiamua kuwachana patakua hapatoshi.Walibya wamesema mfumo wao wa kudeal na maswala Serikali kama Nchi uwa ni Nchi na Nchi.Mfumo wa kudeal na Mtu na Nchi ni wa Watanzania pekee.
Issue hizi za kisanii jamani tuishi hivi kwa usanii wa matendo dhamila zetu zinatwambia nini ndani ya mioyo yetu,Watawala wetu wanataka kuaachive nini?Na kama wanaimani,Imani yao inatofauti gani dhidi ya imani za watanzania wengine kupitia madhehebu yao.Manake matendo hayo wakati mwingine ni tofauti na ubinadamu.
Hakika watendaji wa michongo hiyo wanajiona ni wajanja sana kuzidi watanzania wengine na kuwa wanamaarifa ya kutafuta fedha zaidi kuliko watanzania wengine.
Sawa wakati mwingine nikitafakali sana uwa naumia ukiwakuta watanzania walio mitaani haswa wenye ufahamu mdogo kulingana na uwezo wa elimu yao,wanatabia ya kuwasifia wafanyabiashara wakubwa hapa Nchini utasikia fulani anafedha kuzidi fulani laiti kama wangeambiwa ukweli japo robo sifa hizo wangeamishia kuwasifia mama zao wanaouza genge mtaani kwao.
Ni vyema pia serikali ikaasisi mfumo wa kutupatia taarifa Wafanyabiahara wetu wa kitanzania wanathamani kiasi gani ya utajiri wao na kutuonyesha shughuri zao zote halali kwa faida ya kutathimini na kuwapongeza hata kwa kuwapa nishani kwa mchango wao wa ujenzi wa Taifa kwa kutoa ajira na kuinua pato la Taifa.
Serikali ilishajitoa kuwa HAIFANYI BIASHARA,hivyo basi mapato ya serikali yanategemea kodi na vyanzo vingine,hivyo wafanyabiashara hawa ambao ni walipa kodi tuambiwe kwa mfano kwa mwaka huu Kampuni fulani inayomilkiwa na fulani mwaka huu imelipa kodi kiasi kutaokana na shughuri kadha wa kadha.Kujitoa kufanya biashara basi tushindwe kusimamia biashara na michakato ya hawa waliochiwa kufanya biashara hizo.
Mfano deni hilo la walibya hatujui lilinunuliwa na MeTL kwa bei gani?Mambo yawekwe wazi.manake sikuwatanzania watakapo yaweka wazi wenyewe basi sipati picha yatakuaje.