Libya: Mapinduzi yatumbukia nyongo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Libya: Mapinduzi yatumbukia nyongo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, May 9, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Waziri mkuu wa Libya al Keib pichani.

  Habari kuwa ofisi ya waziri mkuu wa Libya Abdurrahim al-Keib imevamia na hajulikani aliko ni pigo kwa serikali mpya NTC. Je tatizo ni nini? Tatizo ni kuchukua madaraka bila kuwa na maandalizi au tamaa ya wale waliokuwa na Muamar Gaddafi wakamgeuka?

  Je tatizo ni ukale wa mfumo ulioachwa na Gaddafi au ni umma kuanza kugundua kuwa kumbe wanasiasa si watu wa kuamini kama ilivyotokea Misri ambapo mapinduzi yametekwa na jeshi na mabaki ya Hosni Mubarak sawa na Libya?

  Kwa habari kwa kina: BONYEZA HAPA.
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hadithi yako inatufundisha nini?
   
 3. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  We unaona inafundisha nini? Kwanza hii si hadithi bali habari.
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Ni wakati muafaka kuwatoa ccm madarakani
   
 5. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sure mradi tusiwatoe bila maandalizi ya kutosha kuhakikisha kuwa mapinduzi yetu hayatekwi na mapandikizi watakaohama CCM na kujiunga na upinzani baada ya kuona upepo unabadilika.
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Tanzania si Libya!

  Hadithi hii haina uwiano wowote na TZ! Kwa Tanzania, kuna upinzani, kuna utawala wa sheria! Hata ikitokea upinzani ukachukua nchi, itakuwa labda sawa na Zambia, si Libya.

  Hii naifananisha na enzi za kutishia wananchi kwa kuwaonyesha mikanda ya vita za Rwanda na Burundi!
   
 7. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  utawala gani wa sheria ulioko?????????

  Kila sehemu rushwa tupu......sikubaliani na Invisible hata kidogo
   
 8. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mkuu thanx
   
 9. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Maandamano na mkesha wa Arusha na silaha alizokutwa nazo kiongozi fulani ambaye hakwenda kulala hotelini huo unauita ni upinzani unaofuata sheria?

  Tatizo la Libya unalielewa, ni ukanda na ukabila. Mapinduzi ya kijeshi mara nyingi huwa na visasi na uasi. Hii inatufundisha kuwa ballot boxes ndiyo njia nzuri ya kufanya mabadiliko.
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Hilo ndilo jibu. Hao walikuwa opportunist.
   
 11. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Invi.....not that easy mkuu....ni suala la kuangaliwa kwa ukaribu na thadhari ichukulliwe as well........dhamira za wanasiasa ni sawa na msitu mkuu .................never to be taken for granted ni bora kujua hatari na isitokee kuliko kuachukulia kwa urahisi kama hivi

  I beg to differ.......there are lessons in that movemement
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kabisa wappo kati yetu hawajui kabisa maana ya mapinduzi ya umma (popular revolution). Wengi wanafikiria ni sawasawa na "mapinduzi ya kijeshi". Mapinduzi ya umma yanapotokea hadi kukamilika inaweza ikapita muda kwa sababu changamoto kubwa na ya kwanza kabisa - hasaa kwenye nchi kama Libya - ni kutengeneza mifumo mipya ya utawala ambayo haimzunguki mtu. Hii ni kazi kubwa waliyonayo Walibya and so far they are doing better.

  Misri nako ni hivyo hivyo; ila angalau Misri kulikuwa na a strong military institution. Kazi ya Misri ni kutengeneza institutions nyingine za kiraia. Tunisia wao wako vizuri zaidi kwa sababu tayari walikuwa na very strong institutions ambazo hazikutetereka sana baada ya Ben Ali kukimbia. Kwao tatizo lilikuwa la mtu mmoja hasa badala ya system nzima.

  Hivyo, ni vizuri kuangalia kesi hizi kila moja kivyake vyake badala ya kujaribu kuangalia zote kwa mkupuo. Mapinduzi hayafanani, na kukamilika kwake hakufanani! Miaka hamsini baadaye bado tunahangaika na mapinduzi ya Zanzibar!!
   
 13. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwanakijiji Umesikiliza makongamano wanayofanya Wazanzibar kuhusu kupinga muungano???

  Wanadai kuwa Mapinduzi yaliyotokea Znz hawakufanya wao hata kidogo.....Yalipangwa Na Nyerere na John Okello

  Na Mapinduzi yalifanyika makusudi ili watawaliwe, na sasa hivi ndio wanadai nchi yao
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  uzuri mmoja wa historia ni kuwa hakuna anayeweza kubadilisha. Unachosikia watu wanakisema ni 'historical revisionism'. Wanajaribu kuandika upya historia ili kuhalalisha matendo yao ya leo! HIvyo, wanaweza kuwavuta wale tu ambao ni wavivu wa kujifunza historia! Hakuna ushahidi wowote kuwa Nyerere alihusika na mapinduzi ya Zanzibar kabla ya kutokea! NONE WHATSOEVER.
   
Loading...