- Source #1
- View Source #1
Wakuu
=====
Ni kweli LHRC imelaani kauli zisizo na mashiko za Maria Sarungi zenye mashiko ya uchochezi na uvunjifu wa amani? mwenye ukweli wa taarifa atupe ukweli.
=====
Ni kweli LHRC imelaani kauli zisizo na mashiko za Maria Sarungi zenye mashiko ya uchochezi na uvunjifu wa amani? mwenye ukweli wa taarifa atupe ukweli.
- Tunachokijua
- Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ni shirika la utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania. LHRC ilianzishwa mwaka 1995 kama shirika lisilo la kiserikali, la hiari, lisiloegemea upande wowote na lisilo la faida, likiwa na madhumuni ya kufanya kazi ya kuwawezesha na kuhamasisha uelewa wa kijamii, wananchi wa Tanzania kuhusu haki za kisheria na za binadamu.
Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.
Madai
Julai 28, 2025 kumeibuka na Tarifa kwa Umma ikadiwa kutolewa na kituo cha sheria na haki za binadamu ikiwa na kichwa kinachosemeka; “LHRC YALAANI KAULI ZISIZO NA MASHIKO ZA MARIA SARUNGI ZENYE MASHIKO YA UCHOCHEZI NA UVUNJIFU WA AMANI”.
Taarifa hiyo inaendelea kueleza kuwa imesikitishwa na machapisho yaliyotolewa na mwanahakati Maria Sarungi kupitia mitandao yake ya kijamii na kwamba yanachochoea fujo hivyo wanamuona kuacha kufanya hivyo na pia serikali ichukue hatua stahiki.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa si ya kweli.
Ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa hiyo haijatolewa wala kuchapishwa na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) katika mitandao yao ya kijamii. Taarifa hiyo imeghushiwa kutoka kwenye moja ya barua zilizowahi kutolea na kituo hicho.
Aidha taarifa hiyo pia imetumia mpangilio tofauti na ule ambao umekuwa ukitumiwa na LHRC katika taarifa zao kwa umma. Taarifa hiyo pia imeelezea tu kumuonya Maria Saruni na haijaeleza haswa ni machapisho yake yapi yenye mwenendo wa kufanya fujo.
Kumekuwa na mwenendo wa wa kusambazwa kwa taarifa potoshi za aina hiyo zinakiuhisha LHRC na Maria Sarungi.