wewe ni mjinga na mnafiki, watu kama ninyi ndio mnaoongoza nchi kama hii, akili kama zako ndizo zinazoongoza nchi hii na ndio maana hatuendelei. unafiki ndio unaoligarimu taifa hili na ndio maana mnafoji vyeti na kukalia viti serikalini.
watu wanaogawanya wananchi unafikiri ni nani? unajua kuwa magufuli alivyoingia madarakani alikuwa anaungwa mkono sio tu na dunia nzima, bali hata chadema etc? lakini siku zilivyoenda, watu walipokuwa wanatoa dukuduku zao na wanaona wanadharauliwa, limeibuka tabaka tayari la wachache wanaolindwa naye ambao wanajifanya hawaoni complains za wananchi, maumivu ambayo wananchi wanayapata mtaani yeye pamoja na wanaomsapoti wanajifanya hawaoni, matokeo yake chuki dhidi ya serikalini imekuwa kali mno, hivyo hakuna umoja kitaifa na anayesababisha hayo yote ni yeye mwenyewe pamoja na wanaomdanganya kuwa wanaweza kuongoza kama vile bashite.
hoja ya msingi sana hapa ni kuulinda utaifa wetu, tulinde umoja wetu, vitu vyote vinavyoweza kutugawanya, kutufanya tusiwe pamoja tuviepuke. kwa chuki serikalini namna hii, watu wamesoma hawana kazi, watu ni masikini mtaani kuliko kipindi cha kikwete, unafikiri akitokea gaidi mmoja kuamua kugawa hela watu wajiunge huko mkuranga, itashindikana? mtu akiwa frustrated, hana upendo tena na nchi yake, hana upendo na serikali, akili yake inawaza nifanye chochote ili nilishe familia etc, inakuwa rahisi sana kufanya maamuzi ya kipumbav kama hayo ya mkuranga.
jiulize, hao wa mkuranga kwani wameanza leo, si wamoja na wale wa kibiti, mapango ya ambani tanga etc?, je, nani ana wafund? hawaishi miongoni mwa raia? sio watz hao? sio watoto wetu na ndugu zetu?....ni ndugu zetu tu hao, anayetakiwa kuwafichua walipo ni raia na sio polisi, polisi atapata information toka kwa raia wa kawaida kabisa...NA KAMA KUNA CHUKI NA HAMNA UMOJA NCHINI kwenye issue ya uzalendo, unafikiri raia gani atatoa msaada kwa serikali?
enzi za nyerere kulikuwa na uzalendo mkubwa sana, mtu akifika hata kwa balozi tu kama ana uhatari wowote, taarifa hizo tayari zimeshafika serikalini, kila mtu alikuwa usalama wa taifa...lakini sasaivi bashite na genge lake ndio wanajifanya usalama wa taifa, kufanya majaribio ya kijinga kabisa. hivi jaribio la huyo gaidi utalilinganisha na la bashite? michezo ya kitoto kutumia vyombo vya usalama kufanya mambo ya kupumbav kudhalilisha tu jeshi na TISS. bashite na mkulu wote hawana background ya inteligensia yeyote za kijeshi wala usalama wa taifa, wametoka zao tu huko koromije na geita hawajui chochte. hapo ndipo tunaona umuhimu mtu kama membe ndio alitakiwa kuwa rais, na sio hawa wasiojua wanachokifanya. acheni kuharibu nchi yetu, watu wameijenga hii nchi kwa garama kubwa alafu ninyi kwa muda mchache muharibu? kwa kutokusikiliza kilio na ushauri toka kwa watu, mnaharibu nchi yetu na Mungu atawahukumu!