SI KWELI PreGE2025 LHRC waionya CHADEMA lugha za matusi

SI KWELI PreGE2025 LHRC waionya CHADEMA lugha za matusi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
LHRC waionya CHADEMA kuhusu matumizi ya lugha za matusi
LHRC 1 Aug 11.jpg
LHRC 2 Aug 11.jpg
 
Tunachokijua
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ni shirika la utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania. LHRC ilianzishwa mwaka 1995 kama shirika lisilo la kiserikali, la hiari, lisiloegemea upande wowote na lisilo la faida, likiwa na madhumuni ya kufanya kazi ya kuwawezesha na kuhamasisha uelewa wa kijamii, wananchi wa Tanzania kuhusu haki za kisheria na za binadamu.

Madai

Agosti 11, 2025 imeibuka barua/Taarifa kwa umma na kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa na utambulisho wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) ikiwa na kicha kinachosomeka;

“KEMEO LA LUGHA ZA MATUSI ZINAZOTOLEWA NA WANACHAMA WA CHADEMA DHIDI YA VYAMA VINGINE VYA SIASA NCHINI”

Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.

Utafutaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa Taarifa hiyo haijatolewa na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC). Kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram LHRC hawajachapisha taarifa yoyote kwa Umma Agosti 11, 2025.

Hadi kufikia wakati ripoti hii inaandikwa Agosti 11, 2025 taarifa kwa umma ya mwisho ilitolewa na kuchapishwa na LHRC ni ya Julai 30, 2025 wakilaani kutekwa, kuteswa na kutelekezwa kwa raia wa Kenya anayetambulikwa kwa jina la Mwabili Mwagodi.

Taarifa hiyo ni ya kughushi kutoka kwa moja ya taarifa zilizowahi kuchapishwa na LHRC katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii. Taarifa hiyo imetumia mpangilio tofauti wa maneno na uandishi ukilinganisha taarifa rasmi zilizowahi kutolewa na kituo hicho.
Back
Top Bottom