Lets talk about this...........

Lets talk about this...........

Salaam wapendwa.

Leo nimepokea kwa huzuni habari za kifo cha aunty yangu(ulale pema peponi shangazi)

Allikua anasumbuliwa na saratani ya titi,

As a coincidence ,asubuhi hii pia nimesoma habari which I think some of you might have read,

Ilikua kwenye mtandao wa Yahoo,

Mwanamke ambaye alikua anajua anakufa aliomba wahudumu wa gari la wagonjwa(paramedics) wampeleke beach/ufukweni mwa bahari for one more time,ambapo walikubali kumpeleka.

Kwa kweli hizi habari zimenifanya nifikirie kama na mimi ningekua najua siku zangu za kuishi hapa duniani karibia zinafika ukingoni,ningelichukualiaje na kubalianaje na hili swala ????................

sasa mwana JF ningependa uchukue a minute or two kulifikiria, na wewe ungekua kwenye situation hio,ungefanyaje kukabiliana na hili?

Nimeona mahali kuna sehemu / hospice ambazo ni sehemu za wagonjwa wanaokaribia kufa/siku zao kukaribia ukingoni kukaa huko na specialized doctors and nurses mpaka wanapofariki…………………………..je ungekubali kwenda???...............hii inawapunguzia familia kukuona in pain na hivyo kuwaondolea na wao kuwa traumatized na kifo chako…………

Je tuna hospice ngapi nchini??? Nyingi zinahitajika?if yes, WHY and if no, WHY…….

Usiku saa hizi sijui kama ninaeleweka….



*Again lala pema peponi aunty-a woman should be kind,prayerful and hardworker,is what I have learned in your short but remarkable life*

Pole sana kufiwa na shangazi yako! Apumzike kwa amani! Kuhusu "Hospice" sina uhakika kama Tanzania zipo, na kama zipo basi huduma zake zikoje! Kwa wenzetu "Hospice" zina lengo mahsusi la kuwasaidia wagonjwa wa magonjwa sugu kama kansa kufa kwa amani, bila maumivu, bila mateso na bila mahangaiko! Wanajua kabisa wanakufa, lakini wanapata intensive care ya huduma za kimwili na kiroho hivyo hata ukiwatembelea wanakuwa na amani sana mpaka unaweza kushangaa! Ni msaada mkubwa sana kwa mgonjwa mwenyewe na hata kwa familia yake!
 
Uncle yangu alikuwa nje kwa miaka 32 alipostaafu akarudi Tz. Sasa baada ya miaka 3 mkewe akaanza umwa fizi akawa anaenda kwenye hizi dispensary wanadai jino wanampa dawa ya kutibu meno.
Kila siku maumivu hayaponi uncle akawa anamwambia kwanini asiende hospital yeyey analeta ubishi.
Siku moja akampeleka Lugalo walipomchek wakasema inawezekana ni issue kubwa aende Muhimbili walipoenda Muhimbili wakakata kinyama wakakifanyia vipimo na majibu yakaja kuwa ni cancer.
Ma dr wakakaa kikao wakasema wanaweza mfanyia operation uncle akagona akasema wamruhusu ampeleke India na kweli wakamruhusu akampeleka India.
Kufuika kule wakamwambia kuwa wasimdanganye hiyo cancer iko final stage hakuna wanaloweza fanya zaidi ya kumpa vidonge vya maumivu so arudi nyumbani.
Uncle akasema hawezi mrudisha mkewe ashuhudie anafariki pasipo kufanya lolote so akawabembeleza abaki hospital.
Wakambakisha pale walikaa ela ikaisha akauza magari yote sita baada ya miezi sita akafariki.
Cancer ni ugonjwa mbaya sana

pole sana mkuu,

mie naona madaktari wawe wazi kuwaambia familia ,ndugu yenu hatapona,familia ijikite kumnunulia ndugu yao dawa za kupunguza maumivu badala ya kutafuta matibabu ya kuponesha,kuingia gharama kubwa. ila sidhani kama hao ndugu hata wakiambiwa ndugu yenu anakufa still watakubali kumuacha aende hivi hivi,ni kawaida yetu kudhani kila ugonjwa una dawa,hivyo watafight to the end.
 
Back
Top Bottom