Lets talk about this...........

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,618
Reaction score
33,475
Salaam wapendwa.

Leo nimepokea kwa huzuni habari za kifo cha aunty yangu(ulale pema peponi shangazi)

Allikua anasumbuliwa na saratani ya titi,

As a coincidence ,asubuhi hii pia nimesoma habari which I think some of you might have read,

Ilikua kwenye mtandao wa Yahoo,

Mwanamke ambaye alikua anajua anakufa aliomba wahudumu wa gari la wagonjwa(paramedics) wampeleke beach/ufukweni mwa bahari for one more time,ambapo walikubali kumpeleka.

Kwa kweli hizi habari zimenifanya nifikirie kama na mimi ningekua najua siku zangu za kuishi hapa duniani karibia zinafika ukingoni,ningelichukualiaje na kubalianaje na hili swala ????................

sasa mwana JF ningependa uchukue a minute or two kulifikiria, na wewe ungekua kwenye situation hio,ungefanyaje kukabiliana na hili?

Nimeona mahali kuna sehemu / hospice ambazo ni sehemu za wagonjwa wanaokaribia kufa/siku zao kukaribia ukingoni kukaa huko na specialized doctors and nurses mpaka wanapofariki…………………………..je ungekubali kwenda???...............hii inawapunguzia familia kukuona in pain na hivyo kuwaondolea na wao kuwa traumatized na kifo chako…………

Je tuna hospice ngapi nchini??? Nyingi zinahitajika?if yes, WHY and if no, WHY…….

Usiku saa hizi sijui kama ninaeleweka….



*Again lala pema peponi aunty-a woman should be kind,prayerful and hardworker,is what I have learned in your short but remarkable life*
 
Hospitali ni drs ndiyo wana maamuzi ya kuacha matibabu kama mgonjwa wana fahamu hata pona

Famila inafahamishwa kuwa sasa tuko kwenye ' end of life care' kwa wagonjwa wa cancer wanakuwa kwenye maumivu makali. Hapa mgonjwa anapewa dawa za maumivu tu ma anasaidiwa kuwa comfortable. Ndugu na jamaa wanakuwa na muda wa kuagana na mpendwa wao.
 
Pole sana mkuu. Apumzike kwa amani shangazi.

Bado nina usingizi. Nikiamka nitatoa maoni yangu.
 
Hospitali ni drs ndiyo wana maamuzi ya kuacha matibabu kama mgonjwa wana fahamu hata pona

ni daktari au mgonjwa ndio anaamua asiendelee na matibabu???au kwa vile nchi yetu ni developing country mgonjwa hana choice Sky?
 
ni daktari au mgonjwa ndio anaamua asiendelee na matibabu???au kwa vile nchi yetu ni developing country mgonjwa hana choice Sky?
Uamuzi wa daktari unazingatia hali ya mgonjwa vile vile gharama za matibabu. Hamuwezi kuenddlea kugharamia matubabu wakati hayatamsaidia mgonjwa kupona.
 
Rafiki yangu alifariki kwa Leukemia najua ni jinsi gani inavyoumiza

Kwa nchi zetu bado hatujafikia kuwa na maamuzi ya kuruhusu kifo ingawa in reality ipo hivo, tunapigana mpaka dakika ya mwisho sababu tuna misingi ya kiimani

Pole sana
 
Kaka yangu alikuwa akiishi nje ya nchi aliowa Tanzania, siku kama kesho mkewe ndio apande ndege na kwenda kwa mumewe. Ilipigwa simu na kupewa habari kuwa kaka amefariki. Sababu halisi haijulikani lakini kuna wanaosema alipewa sumu kwenye kinywaji na kuna wanaosema alipata Tetanus(tetnas). Mkewe alilia sana lakini kazi ya Mola huipanga aitakavyo mwenyewe.

Pole kwa msiba wa Aunty yako Rebecca 83
 
That's so disturbing, angalau hizo hospice care zinasaidia kupunguza machungu kwa wanandugu.

The big question is, utachukuliaje swala la namna hiyo, to be told that unakaribia mwisho wa uhai wako again it's so frustrating.
 
That's so disturbing, angalau hizo hospice care zinasaidia kupunguza machungu kwa wanandugu.

The big question is, utachukuliaje swala la namna hiyo, to be told that unakaribia mwisho wa uhai wako again it's so frustrating.
Hapa ndipo wengi hukumbuka dini, unamkuta mtu anaomba aletewe Rosary hata kuisalia hajui mradi iwe pembeni ya kitanda.
 
Uncle yangu alikuwa nje kwa miaka 32 alipostaafu akarudi Tz. Sasa baada ya miaka 3 mkewe akaanza umwa fizi akawa anaenda kwenye hizi dispensary wanadai jino wanampa dawa ya kutibu meno.
Kila siku maumivu hayaponi uncle akawa anamwambia kwanini asiende hospital yeyey analeta ubishi.
Siku moja akampeleka Lugalo walipomchek wakasema inawezekana ni issue kubwa aende Muhimbili walipoenda Muhimbili wakakata kinyama wakakifanyia vipimo na majibu yakaja kuwa ni cancer.
Ma dr wakakaa kikao wakasema wanaweza mfanyia operation uncle akagona akasema wamruhusu ampeleke India na kweli wakamruhusu akampeleka India.
Kufuika kule wakamwambia kuwa wasimdanganye hiyo cancer iko final stage hakuna wanaloweza fanya zaidi ya kumpa vidonge vya maumivu so arudi nyumbani.
Uncle akasema hawezi mrudisha mkewe ashuhudie anafariki pasipo kufanya lolote so akawabembeleza abaki hospital.
Wakambakisha pale walikaa ela ikaisha akauza magari yote sita baada ya miezi sita akafariki.
Cancer ni ugonjwa mbaya sana
 
Inasikitisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…