Lets talk about Haja Kubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lets talk about Haja Kubwa

Discussion in 'JF Doctor' started by Mphamvu, Apr 30, 2012.

 1. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,584
  Likes Received: 783
  Trophy Points: 280
  Wakuu poleni na majukumu ya ujenzi wa taifa hili, linalofaidiwa na wachache waliopewa jina la ‘wajanja’.
  Poleni sana…
  Leo nataka tusemezane kitu cha tofauti kabisa, sio kigeni kwa yeyote ila masuala yake huwa hayasemwi mara kwa mara.
  Leo nataka tuzungumzie KINYESI, unashangaa nini? Namaanisha nisemalo, leo nataka tufunguke kuhusu uchafu ambao ni matokeo ya mfumo wa umen’genyaji chakula a.k.a ‘kimba’ a.k.a mavi ukipenda haja kubwa, lakini kwa Kiswahili sanifu ni kinyesi.
  Mada yangu kuhusu haja kubwa itazingatia zaidi uhusiano kati yacho na maisha yetu ya kila siku katika muktadha halisi. Sawasawa?
  UTANGULIZI​

  Kama tunavyojua (ukibisha una yako), kwenda haja kubwa ni suala la muhimu na la lazima kwa binadamu yeyote, kama tu ilivyo kula na ndio maana ili nyumba ikamilike ni shurti iwe na jiko na choo. Hivyo tu ndio vinaipa legacy nyumba ya kuishi, sio bafu wala chumba cha kulala. Kutokana na unyeti wa suala husika, sina budi kuweka wazi mtazamo wangu juu ya masuala kadhaa kuhusu haja kubwa, ambayo pengine (weka msisitizo hapa) yanaweza kuboresha mazingira ya huduma hii muhimu kwetu baada ya chakula.
  CHOO​

  Kama ilivyodhihiri hapo juu (hutaki unaacha), choo ni kati ya sehemu muhimu zaidi katika nyumba. Ili kuwe na unyaji wa starehe na uliotukuka ni lazima choo kiwe safi na chenye mazingira rafiki kwa mtumiaji wacho. Kuna vyoo vya aina nyingi, hata ule unyaji wa kuchimba kishimo na kufukia unaweza kutafsiriwa kama choo endapo utakuwa ni wa kudumu. Kuna hivi ‘Western Type’ (vya kukaa) ambavyo wanaita vyoo vya kizungu, na kuna vyoo vya Kiafrika almaarufu kama squart toilets, au ‘drop in’, yaani vya shimo among many other types. Binafsi ni mshabiki wa vyoo vya shimo (siku hizi kina option ya kuweka shank kikafanana na cha kizungu) kwa kuwa kinaleta hali fulani ya comfortability wakati wa kukata gogo. Vyoo vya kukaa huwa vinaleta hali ya kuhisi kama unajinyea kwa vile unajisaidia huku mapaja yakiwa yamebanana, tofauti na kanuni za unyaji ambapo kunya huku umechuchumaa is much better, kiafya na kiakili. Sifa nyingine ya choo ninachokipenda (though it may sound ridiculous), ni hali ya choo kutokuwa na paa, yaani kiwe hakijaezekwa. Hii itapelekea choo (hasa kinapokuwa cha shimo) kuwa kikavu muda mwingi na hivyo kupunguza hali ya kinyaa inayopatikana chooni. Vilevile, kunakupa view nzuri ya anga wakati unakata gogo, hivyo kuchochea fikra za mnyaji. Ni mara nyingi watu wamekuwa wakisema kuwa wakati wa haja kubwa ni wakati mzuri wa kutafakari na kupanga mikakati ya kimaisha, if that is true, a blue sky is even much better. Ubaya wa feature hii ya choo ni kuwa si nzuri sana wakati wa mvua au jua linapokuwa kali sana kwani huondoa ladha ya gogo. KUNYA STAREHE BWANA!
  Mwisho, choo kiwacho chochote, lazima kiwe katika hali ya usafi muda wote, ulazima huu unatokana na ukweli kwamba kama choo sio safi, kinaweza kusababisha magonjwa kadha wa kadha ya kuambukiza.
  MIUNDOMBINU
  Asikudanganye mtu, muundombinu mkubwa wa choo ni maji, haijalishi ni cha aina gani, ingawa uhitaji wa maji kwa wale wanaotumia vyoo vya kizungu vya kuflash ni mkubwa ukilinganisha na sie wa vyoo vya kulenga. Kwa watumiaji wa ‘Western type’, kuwa na mfumo kamili wa maji katika vyoo vyao haikwepeki, kwa wanaotumia vya shimo si lazima sana kuwa na mfumo kamili wa maji, unaweza kuweka ndoo ya maji ambayo italazimu kuwa na maji muda wote, au kama umenganishwa na mfumo wa maji wa manispaa uliyomo unaweza kuweka bomba la maji chooni, au just nje ya choo. Maji haya yatakuwa kwa ajili ya kusafisha ‘privates’ baada ya kukata gogo (endapo unatumia maji), yatatumika kunawa mikono baada ya shughuli kwisha na pia yatatumika kusafidha choo (tundu, sakafu na kuta). Miundombinu mingine ni pamoja na taa na misumari ya kutundikia nguo wakati unafanya mambo yako.
  UNYAJI​

  Hi indio shuguli yenyewe sasa baada ya shuguli zote za awali za maandalizi kuwa ziko sawa na hapa ndipo kuna matatizo mengi ya kujitakia ambayo watu hawataki kuyasema. Matatizo yanaweza kuwa yamesababishwa na aina ya choo unachotumia au kutokaa sawa kwa miundombinu ya choo unachotumia, mfano, baadhi ya watu (mimi kwa mfano) huwa hawako comfortable na vyoo vya kukaa aina ya Western, kwani kujisaidia ukiwa umechuchumaa ni vizuri kwa kuwa mapaja yanakuwa yameachana vya kutosha hivyo kinyesi hutoka kwa urahisi na bila bugudha yoyote. Unyaji katika mazigira ya vyoo vya kukaa hufanya mapaja kubanana, hivyo kupelekea hatari ya maambukizi katika mapaja na kuongeza hatari ya maambukizi katika njia ya mkojo (UTI) hasa kwa wanawake.
  Katika kipengele hiki ningependa pia niseme kuhusu aina za haja kubwa na changamoto zake kwa wanyaji. Kimsingi, **** mbari kuu tatu za haja, ngumu, laini na majimaji au uharo. Aina mbili za mwanzo zinatokana na tabia za ulaji na hii ya mwisho inasababishwa na magonjwa, hasa yanayohusu tumbo. Walio wengi wanapendelea kupata choo laini, na wachache hupenda choo ngumu, pasi na shaka yoyote hakuna anayependa kuharisha kwa vile kunaambatana na kugonjeka. Choo kigumu sana kinaweza kusababisha mipasuko kwenye njia ya haja.
  Tumesema kuwa aina za haja hutokana na vyakula tulavyo, haja ngumu inatokana na kupendelea vyakula vikavu na vigumu, pia kutokunywa maji ya kutosha wakati ili upate choo laini inakulazimu kunywa maji ya kutosha (3-5 litres kwa siku), kutumia mboga na matunda jamii ya nyuzinyuzi pamoja na aina fulani ya matunda kama vile papai na parachichi. Kwa wanaopata choo majimaji au uharo, tiba ya haraka ni supu ya ngano, lakini pia wanatakiwa kunywa kiasi kikubwa cha maji ili kufidia maji yanayopotea mwilini kwa njia ya kuharisha, lakini pia ni muhimu na lazima kutibu ugonjwa wa msingi ambao umepelekea kupata choo majimaji.
  Changamoto nyingine ni ulaji wa pilipili kupita kiasi ambao husababisha muwasho katika njia ya haja kubwa wakati wa unyaji na wakati mwingine vidonda kwenye puru (sehemu ya ndani ya njia ya haja kubwa).
  USAFI​

  Kuna namna nyingi za kusafisha njia ya haja kubwa baada ya kujisaidia. Kujiswafi huku wengine huita kuchamba au kutawaza, lakini kwa ujumla ni kusafisha tundu la haja kubwa na maeneo yanayolizunguka ili kuondoa mabaki ya kinyesi.
  Namna kuu na iliyozoeleka kwenye mazingira yetu ni maji, nimesema kuwa hii ni namna kuu kwa vile hata baadhi ya vitabu vya dini vimetaja waziwazi kama namna pekee ya kujiswafi. Baadhi ya watu hutumia karatasi laini maarufu kama toilet papers na wengine hutumia vyote yaani toilet paper na maji kwa kuanza kupunguza uchafu kwa karatasi hizo na kasha baadae kumalizia na maji. Kimsingi kila njia ina faida na hasara zake, mfano, utumiaji wa karatasi huwafaa zaidi wale wasio na vinyweleo vingi katika tundu la haja kubwa na maji ni mazuri zaidi kwa wale waliojaliwa haya makatamavi. Utumiaji wa vyote viwili ni mahususi kwa wale wanaopata choo laini (sio majimaji) kwa kuwa aina hii ya kinyesi huacha mabaki mengi.
  Faida za kutumia karatasi laini ni pamoja na kuepuka kinyaa cha kushika kinyesi kwa mkono ingawa wanaopinga matumizi ya tishu wanaona kama ni sawa na kujisiliba uchafu badala ya kujisafisha. Maji ndio njia inayopendekezwa na wengi katika mtazamo wa Kiafrika, ingawa nayo huleta hali flani ya kutojisikia vizuri kwa vile unalazimika kuvaa nguo huku makalio yakiwa yamelowa maji.
  Aina nyingine za uchambaji ni pamoja na matumizi ya majani, mawe au kujisugua ukutani au kwenye shina la mti, ingawa njia hizi zinatafsiriwa na wengi kama zisizokuwa za kistaarabu.
  Cha mwisho na cha muhimu baada ya kujiswafi ni kunawa mikono kwa maji sabuni ili kuondoa uwezekano wa kuondoka na vimelea wa ugonjwa katika mikono.
  HITIMISHO​

  Kwa muda huu ni hayo tu niliyokuandalia kuhusu KINYESI, unaweza kutumia wasaa wako kutoa maoni, ushauri au maswali yako kuhusu makala hii.
  pooping.jpg
  Enjoy your shit,
  Mphamvu.​
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,194
  Likes Received: 1,590
  Trophy Points: 280
  Yaani nimesoma mwanzo hadi namaliza mwishoni, nimekumbuka kila aina ya choo ambacho nimewahi kutumia maishani mwangu. Nimeanzia kutengwa na mama, poti, na kuendelea!

  Umesahau kusema kama mandhari ya choo inaruhusu sio mbaya kuwepo majarida ya kusoma wakati unaendeleza starehe hii muhimu.

  Pia kuna issue ya ku-train your bowel movement. Ukifundisha mwili wako discipline unaweza kujikuta unakuwa na ratiba nzuri sana ambayo ni convenient.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 29,963
  Likes Received: 5,102
  Trophy Points: 280
  raha ya kunya uwe na kijarida, au unaingia jf, huku unachangia mada, huku unashusha vitu......

  King'asti, kalale mama, mie naenda kulala, jf mpaka saa tisa kumi usiku itatuua...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,118
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Puuuuu.... Hii thread inanukaaaaaaaaaaaa! khaaaa.........
   
 5. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,513
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mphamvu usiku wa saa nane ukawazaje hii mambo jameni...kweli hii ndo Jf!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,022
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  hivi kibongo bongo ipo kwenda kunya na kijarida mi nkajua tunaenda na sport tu kweli kua uyaone..
   
 7. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  khaa jf kuna mambo loh....
   
 8. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kwenda mkoa flani Magharibi mwa Tz nikawa na mizunguko ya kibiashara ktk baadhi ya vijiji, kuna siku nikalala kwa Mzee mmoja hapo kijijini , akiwa ndiye mwenyeji wangu.
  Mzee yule alikua anamiliki wake 6 , kilichoniachia historia ni pale mgeni mie nilipoomba kwenda msalani, nikapewa jembe tena bila hata kopo la maji then nikaonyeshwa chaka , hapo nikaambiwa hua wanajisaidiaga mchana, na ikiwa usiku hua wanashuka ziwani. Kwani nyumba haikua mbali na Ziwa.
  HAINA UBISHI NYUMBA CHOO.
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,796
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Duh..!
   
 10. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,967
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Dah!!! Hii thread safi sana.
   
 11. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,123
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  RIP my breakfast.
   
 12. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,094
  Likes Received: 398
  Trophy Points: 180
  Hii thread wala sijaisoma nimescroll down na kuanzakucheka..hata sijui Mphamvu uliwaza nini..nimecheka sana!
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 29,963
  Likes Received: 5,102
  Trophy Points: 280
  hakuna kitu kinaniboa kama nikisafiri, kukata gogo kwenye vyoo vya hoteli.......
   
 14. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mweeeeeeeeeee!
   
 15. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 3,274
  Likes Received: 448
  Trophy Points: 180
  ....uwiiiii.....
   
 16. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,584
  Likes Received: 783
  Trophy Points: 280
  Una miaka mingapi King'asti, maana kama umekelia poti kwa mazingira ya kibongo utakuwa mtoto sana.
  Ishu ya majarida inawezekana katika vyoo vya kukaa, ambako ni rahisi kuwa na balance ya kushikia hilo gazeti. Bowel movement, ni rahisi sana, you just eat with dicipline, kuwa na ratiba maalum ya kula, muda na kiasi cha chakula ambacho hakibadiliki badiliki kunafanya uwe na muda mahususi wa kukata gogo. And thats pretty cool!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,336
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  zis is JF....:yo:
   
 18. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  nilifikiri hapa tunaongelea magonjwa kumbe..................................!!!!!!!!!!!!!!!
   
 19. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,584
  Likes Received: 783
  Trophy Points: 280
  Rudisheni topic yangu mulikoitoa, mimi sio taahira mpaka nikaiweka pale.
  Nina uzoefu wa miezi 12+ humu JF, zaidi ya post 3500 bila kusahau ban 5 katika maisha yangu ya JF.
  Twafadhall?
   
 20. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,615
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Thanx ni nzuri ina mafundisho.
   
Loading...