Let's share the story: experince ilikuwaje ulipofanya maamuzi magumu ya kuacha kazi ya kuajiriwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Let's share the story: experince ilikuwaje ulipofanya maamuzi magumu ya kuacha kazi ya kuajiriwa?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rich Dad, Mar 25, 2012.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wana Jf, Heshima kwenu nyote.
  Mimi ni muajiriwa kwenye kampuni ya private. Ninajituma sana kwenye kazi, na huwa niko proactive kwenye kupanga mambo yangu ya kikazi. Huwa sipendi mambo yatokee kwa surprise afu nianze ku react kutafuta soln.
  Bidii imenifanya niweze kupitia levels mbali mbali za kikazi kwenye management ya kampuni.
  Tatizo linakuja pale ambapo huwa ninaanza kutafakari hatima ya maisha yangu. Huwa sikubaliani na wazo la kufanya kazi mpaka nistaafu. Huwa najiuliza, hivi nikiamua kufanya shughuli yangu mwenyewe ( hasa biashara) sitatoka kimaisha kutokana na bidii yangu? Nilishawahi fanya biashara fulani ambayo ilikuwa inalipa sana, tatizo lilikuja kwenye supervision .....most of the time nakuwa kazini. Na kama mnavojua watu sio waaminifu, basi ile biashara ilikuja ikafa.
  Naombeni yeyote mwenye experience ya kuajiriwa kisha kuamua kuacha kwa hiari na kwenda kujiajirii atusaidie kutuelezea ilikuwaje akafikia uamuzi huo?

  Mambo mengine kama vile "Kujipanga kwanza kabla ya kuacha kazi ..yapo kwenye mchakato tayari".

  shukrani
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  MKUU UKWELI NI KWAMBA MTU AKISHAINGIA KWENYE AJIRA YA MWISHO WA MWEZI, KUJA KUACHA NA KUINGIA KWENYE BIASHARA NI NGUMU SANA MKUU, INAHITAJI MAAMUZI YA ZIADA.

  1, Ukisha ajiriwa ni sawa na mtumiaji wa madawa ya kulevya, mtumiaji wa madawa ya kulevya akisha yazoea madawa na yakaingia kwenye damu yake kuacha ni ngumu sana na huwa asipo tumia anakuwa kama mjinga vile, na katika kazi ni hivyo hivyo mkuu,

  - Na mtu asikudanganye kwamba anaingia kwenye kazi kutafuta mtaji halafu ataacha kazi, no ukisha ingia kutoka si rahisi kabisa

  - Na wengi wanao acha kazi na kuanzisha biashara ni wale ambao either huko kazini kwao kuna matatizo, either contact imeisha, au amefukuzwa, au mazingira ya kazi ni magumu sana,

  - Ila wale ambao wako kwenye ajira na hawana mamatatizo yoyote kuacha ni kugumu ni mpaka afukuzwe au mkataba uishe,

  - N a wengi huwa wanafanya part time business yaani wana biashara na wanafanya kazi

  SO WHAT

  - Mkuu inawezekana kuacha kazi hata kama unalipwa sh ngapi na kuingia kwenye biashara, ila ni uamuzi ambao nina uhakika unatakiwa uufanye wewe mwenyewe na usijaribu kuwashirikisha ndugu, jamaa, marafiki, majirani na kazalika make ukiwashirikisha nina uhakika hutaacha kazi daima,

  -KAMA NI USHAURI WA KUACHA KAZI NA KUINGIA KWENYE BIASHARA, WATUMIE WATU WALIOKO KWENYE BIASHARA NDO WAKUSHAURI USIOMBE USHAURI KWA WATU WANAOTEGEMEA MWISHO WA MWEZI MAKE HAO WATAKUAMBIA ACHANA NA MAWAZO YA KUACHA KAZI
  - Hapa inatakiwa uwe angalau umeisha kusanya mtaji wa kuanzia biashara,

  - Na usiache ghafula, fanya maandalizi yote ikiwemo kufungua kampuni yako kabisa na kuanza operation ili utakapo acha uweze kuingia moja kwa moja kwenye business,

  - Na nilazima uwe na biashara ambayo ina return kubwa ili kama ulikuwa unalipwa mshahara nmkubwa basi hiyo return itakufanya uone kazi si chachote,

  INAWEZEKANA NA KAMA NILIVYO SEMA, NI UAMUZI MGUMU SANA NA WENYE UCHUNGU WA HALI YA JUU MNO NA NI LAZIMA KABULA YA KUACHA UTAMBUE NA KUZIPIKEA CHALENGE NYINGI SANA AMBAZO UNAHISI ZITAKUTOKEA
   
 3. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Du unanikumbusha nilipotoa 24hrs notes Vodacom ilikuwa 2009.thanks Jesus now Im on my own Bata daily and got nothing to loose
   
 4. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana mkuu kwa mchango wako uliojitosheleza, nimependa hapo kwenye kuwaomba ushauri walioko kwenye bishara tayari. Mara nyingi sana watu walioajiriwa huwa wako negative kwenye pindi watoapo ushauri wa kibiashara kwa beginners.
   
 5. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu uli change job kwenda kwa new employer au ulikuwa na mchakato wako binafsi?

   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280

  mkuu na si kwa waajiriwa pekee, hata ndugu,jamaa na marafiki, kama ndugu zako wengi ni waajiriwa usijaribu kuwahusisha kamwe, na marafiki zako pia kama wengi wao ni waajiriwa achana nao katika kuwahusisha.

  Make watanzania wengi tunaamini maisha yako kwenye ajira pekee na kwenye biashara ni kutafuta kifo,

  Huwa nashangaa sana utakuta semina za ujasirimali zinatolewa na wafanyakazi, ni jambo la ajabu sana, na huwa wako bise kufundisha watu waanzisha biashara wakati wao wanaogopa kuanzisha biashara kama ukoma na hawana hata kibanda cha kuuza vocha.
   
 7. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,682
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Imenikumbusha mbali hiki kitu, Kama miaka mi 2 iliyopita nilipoamua kuacha kazi ya procurement Manager Tanzania kwenye kampuni very profitable.

  Kila mtu alinipinga hata mke wangu mwenyewe, sikuwalaumu niliwaambia Wana haki kabisa maana Haya ni maamuzu yangu.

  Nilishakuwa na kampuni ya utalii, ya kinyonge ila ilikosa usimamizi. Nilitafuta hela ya Kutunza familia mwaka mzima na Kuacha kazi.

  Nakumbuka bosy wangu aliniambia nenda kaki miezi mi 3 Kama utakuwa bado na mawazo hayo hayo uje usign barua yako na uache kazi.

  I was paid like 1.7m net, nikawa namesake hela kiasi za maisha. In short I have employed 5 proffesionals now, my company is big, I am free, and Last year only I have. Gross sales of $ 147,000.

  Natoa angalizo tu kwamba mtu asilishauri uache kazi, wala usiigize mtu, do what you believe in, Ajira ni utumwa.

   
 8. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Mimi bado ni muajiriwa ila naomba nikushauri kitu kimoja usiache kazi ndo ukaanze biashara,anza kwanza biashara ikisha take off ndo unaacha kazi kwenda kuisimamia na kuikuza biashara sio mtaji tu but experience also hata kama itakuwa ndogo wakati upo kazi utakuwa umejifunza abcs zake from there you can quit the rat race and go
   
 9. kande kavu

  kande kavu JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu sijaacha kazi, ila nakubaliana na wewe kuwa kuajiriwa ni kupoteza na hasa pale unapokuwa mtu wa kujisimamia na kujituma. Always you do not get the deserved return. I am counting my days and eggs!
   
 10. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Mkuu hatutofautiani sana kimawazo mi niko step ahead kwani biashara yangu inakaribia kuanza kutengeneza faida na nimejipa mwaka mmoja zaidi kubakia kwenye ajira. Kikubwa unatakiwa kuchukia kuajiriwa. Hebu chukua haya maushauri toka kwa waliofanikiwa...

  "Experiment and learn from those experiences. Don't wait for the perfect plan. Look for opportunities where you can truly bring a better offering forward to the customer and market you serve. Following someone else's lead is usually not the answer. MICHAEL DELL

  "One make sure that u have viable and sustainable business proposition. Make sure u are fulfilling some need that has been unmet and make sure its differentiated from everything else out there and that it is difensible". FRED SMITH of Federal Express

  "Target a specific niche. Where there is an ache, you want to be like aspirin, not vitamin. Aspirin solve a very particular problem someone has, whereas vitamins are a general 'nice to have' market. REED HUSTINGS of Netflix
   
 11. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  story yako imeni inspire Mno! thanks for sharing
   
 12. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  sio kila kitu waweza endesha kwa remote..........mimiini moja wapo nimeacha kazi.on very shaky feet now lakini as long hela ya kula inaingai najua I will take off!
   
 13. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu waajiriwa wenzangu kumbe tupo wengi ambao tunafanya kazi lakini tunatamani kuacha...
  wakati nimemaliza masomo na kuajiriwa nilijisemea moyoni kua nitafanya kazi hadi ntakapokua na umri wa 45yrs lakini kwa muda wa miaka yangu minne ambao nimekaa kwenye ajira nimeona kuajiriwa kutanifanya niendelee kuwa mtumwa na naweza nikafa bila kuwaachia wanangu urithi wa kueleweka japo sina mtoto kwa sasa
  Mie niliamua kununua shamba huko porini bagamoyo la heka nne kwa bahati nilipata eneo ambalo lina miti mingi nimeamua niikate hiyo miti ili nichome mkaa baada ya hapo pesa itakayopatikana nitaiingiza ktk kilimo na biashara nyingine ndogo ya chips na chakula. huu ni mwanzo wa safari ambayo nimeianzisha ili kuondokana na hali hii
  Ushauri wenu na uzoefu wenu unahitajika ndugu zangu.
  Asanteni
   
 14. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bado inawezekana mtu kuacha kazi na akaanza from the scratch inawezekana kabisa ni swala la mtu mwenyewe kuamua
   
 15. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,059
  Likes Received: 7,273
  Trophy Points: 280
  Hii thread ukweli kwangu naweza kuiita "thread ya mwaka"
  Huu mwezi ukiisha salama nategemea kutoa notisi ya 30 days ili nipate wasaa wa kushughulikia biashara zangu baada ya miaka mitano ya kuajiriwa na kuwatumikia watu.
  Pia najiimarisha kimasomo nikiwa mwanafunzi wa MBA- Mzumbe kampas ya Upanga.
  Ni wazo ambalo ndugu zangu wamelipinga sana hivyo nimeamua liwe siri yangu mradi hela ya kuishi hainipigi chenga!!!
   
 16. Wun

  Wun JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 353
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu ni maamuzi magumu sana yanayotaka kwanza ujielewe.mimi binafsi baada ya kumaliza chuo nimejiunga mmoja kwa moja kwenye shughuli zangu mwenyewe mwanzo nilikuwa na wasiwasi but now najisikia furaha na kujiamini katika mipango yangu japo biashara zangu siyo kubwa kutokana na kipato changu nilicho azia kuwa ni kidogo
   
 17. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,824
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Mkuu mie nimejilipua mwenyewe nikaacha kazi ya UN nilikuwa na nafasi nzuri tu yenye mshahara mzuri na marupurupu kibao! Asikwambie mtu ajira ni utumwa! Mtu unafanyishwa kazi kama mwendawazimu vile. Nimeamua kusimamia NGO yetu wenyewe ambako najipangia mwenyewe saa ngapi niingie ofisini na kitu gani nifanye kwa muda upi? Ukitaka kuacha kazi usitake ushauri hutakaa uache! Kwangu ilibidi nijisimamie mwenyewe maana kila mmoja alibaki mdomo wazi kwa uamuzi wangu! JILIPUE MKUU!
   
 18. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  kosa nililolifanya mimi ilikuwa ni kuwashirikisha wanafamilia na marafiki ambao wote ni waajiriwa na hakuna aliye na hata kabiashara ka duka. Mkuu tangulia tupo njia moja.

  nilima mpunga kijijini baada ya kukoboa nilipata gunia zaidi ya 50 za mchele niliingiza around ---- 12.2m
  niliilima mahindi na kuyasaga nilipata gunia kama 130 za sembe 900 per kg nilipata zaidi ya --------10m
  ufugaji wa ng'ombe wa maziwa, nauza lita 1000-1200/= na kila siku napata lita si chini ya 75 ---- naingiza 2.5m kila mwezi--- kwa mwaka ng'ombe wananipa ---27m

  ufugaji wa nguruwe kwasasa ninao kama 80 na 8 wana mimba----- kila mwaka natarajia kuuza 150--- roughly let say nitapata around 40m
  nalima maharagwe, njugu, matikiti kiasi, maembe nk nayo yanaingiza fedha nzuri sana japo sijui mahesabu yake halisi
  Majumuisho
  total = 10m+10m+27m+40m= 87mil

  ukitoa operating costs profit will be around let say 45m kwa makisio ya chini kabisa na hapa ni baada ya kuibiwa sana mazao ya kilimo na mifugo na hii nguvukazi yangu ambayo haina uaminifu hata kidogo yaani kila nikibadili vijana wa kazi wanakuwa na uadilifu kwa miezi 3 ya mwanzo baada ya hapo matatizo ni yaleyale wizi kwa kwenda mbelee.. watu wameoa, wamejenga kwa jasho langu.
  Mkuu hebu angalia hapa maziwa nispokuwepo yanapatikana lita 50-70 nikiwepo mwenyewe na kusimamia ukamuaji zinapatikana lita 90 mpaka 100. Mchele nikiacha gunia 10 nikienda mjini na kurudi kijijini nakuta zimebaki gunia 7 nikiuliza sipati majibu.. inaniuma sana sana.. nataka kwenda kusimamia kazi zangu mwenyewe
   
 19. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante kwa kuendelea kutupatia uzoefu. Waajiriwa tuamke.....
  Si kwamba kuajiriwa ni utumwa lakini je baada ya muda wako wa ajira kwisha utakua na nini?
  Asanteni wenzetu ambao mmeamua kuajiriwa mkajiajiri wenyewe
   
 20. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wengi tumejawa na hofu ya ku face - challenges ...lakini ni muhimu sana kuwa na biashara yako hata kama umeajiriwa.
   
Loading...