Giving up vs letting go

Charmaine

Member
Jan 4, 2023
61
160
Mapito ya maisha yana nyakati za hali tofautitofauti, nyakati ambazo aidha hutufanya tukate tamaa katika jambo (giving up), ama tujiengue kwenye mchakato na kuacha jambo liende (letting go).

Katika kufikiria harakaharaka unaweza kuhisi hakuna utofauti kati ya “giving up” na “letting go”, ama ukahisi kuna mstari mwembamba sana baina ya maneno haya mawili. Lakini ukweli ni kwamba kuna utofauti mkubwa sana baina ya maneno haya.

Naomba walau nidokeze kidogo utofauti uliopo:

1} Kukata tamaa ni pale ambapo ukomo wako wa kufikilia umefika mwisho na huna uwezo wa kufanya maamuzi katika jambo ambalo umenasa/linakutatiza. WAKATI kuacha liende ni pale ambapo unajiengua na kujiweka huru dhidi ya jambo ambalo halina afya/msaada wowote kwako katika kukujenga, kukuimarisha, na kukufanya uwe bora zaidi kila iitwapo leo.

2} Kukata tamaa ni kifungo cha mwili, akili, na roho. Yaani ukishakata tamaa utaona kila kitu hakiwezekani nje ya kile kinachokutatiza. WAKATI kuacha liende ni kujikomboa kimwili, kiakili, na kiroho baada ya kuanza maisha mapya nje ya kile kilichokuwa kinakutatiza.

3} Kukata tamaa ni kupunguza siku za kuishi, kwani giza huwa ni nene na milango yote ya kwenda mbele huonekana imefungwa. WAKATI kuacha liende ni kuongeza siku za kuishi, kwani nuru huwa angavu na milango ya kusonga mbele huwa iko wazi ili uweze kupiga hatua mpya katika jambo.

4} Kukata tamaa ni kushindwa WAKATI kuacha liende ni kushinda.

Mfano, kijana aliyesota na bahasha ya khaki mkononi kwa miaka mi5 mfululizo kusaka ajira na bado hajapata, unakuta kakata tamaa kabisa ya maisha, haoni fursa zozote zile nje ya kusaka ajiri. Lakini siku akizinduka usingizini na kuamua ku-let it go of kuzunguka na bahasha kila siku, ataona milango mingi sana ya fursa iliyokuwa iko wapi muda mrefu.

Atawaza, “kumbe hata nikiwa na elfu10 tu naweza kujidamka kwenda Karume saa 10 za alfajiri kuchukuwa t-shirts 10 za mitumba kwa bukubuku. Halafu baadae nazitembeza mitaani na kuziuza kwa bei kati ya 2,500/- hadi 3,500/- kwa kila t-shirt!” Kwahiyo unaweza kuona hapa, “giving up” huwa inafunga milango, wakati “letting go” huwa inafungua milango.

Nina rafiki yangu mmoja ambae anapitia changamoto nyingi sana katika mahusiano yake ya kimapenzi, kwa muda mrefu sasa. Ana mzazi mwenzake (hawajaoana ingawa wana watoto) ambae hamthamini, hamjali, na wala hana dalili za kumuoa. Sasa dada huyu anauwezo wa kuchagua, aidha a-give up, ama a-let it go .

Letting go itamfanya ajiengue kwenye mahusiano haya ambayo hayana afya kwake, hayamuimarishi, hayamjengi, na wala hayampi fursa ya ku-excel mchango wake halisi na thabiti katika mahusiano. Lakini akiendelea kujikatia tamaa kwamba pengine haya ndiyo maisha anayostahili kuishi, basi hatakaa aione thamani yake katika mahusiano, na wala hatakaa aione thamani yake katika maisha kwa ujumla.

So, ni nyakati zipi ambazo “letting go” ina mashiko?

Letting go ina mashiko pale ambapo jambo unalojihusisha nalo halina afya wala msaada wowote tena kwako katika kukujenga, kukuimarisha, na kukufanya uwe bora zaidi kila iitwapo leo.

Letting go ina mashiko pale ambapo umekaa sehemu, ukafanya kazi kwa nguvu zako zote, akili yako yote, na katika ubora wako wote halafu bado ukapuuzwa, ukakejeliwa, ukadharauliwa, n.k.

Mfano, kuna rafiki yangu mmoja aliwahi kuajiriwa kwenye kampuni moja hivi, aliajiriwa kama “Trainee”. Kwakuwa alikuwa na kichwa chepesi cha kuelewa mambo, ilimchukuwa miezi 6 tu kuwa competent kabisa katika ile kazi. Lakini cha ajabu aliendelea kulipwa mshahara wa “trainee” kwa miaka 4, ilihali mchango wa kazi yake ni mkubwa kuliko hata wafanyakazi wakongwe (aliowakuta) pale kazini.

Kuna siku alikaa na kuwaza sana, akaona hataaa enough is enough ! Akaamua wacha liende (letting go), na siku aliyoacha kazi kwenye kampuni ile, ndipo thamani yake ilipopanda mara dufu. Kampuni ileile iliyomlipa mshahara wa trainee kwa miaka mi4 mfululizo, ilikuwa kila siku inamfuata kumbelembeleza ili wamuajiri tena kwa dau nono.

Kwahiyo, nihitimishe kwa kusema, “letting go” ni hatua muhimu sana ya self-care, ni hatua muhumi ya kujitathimini na kujiimarisha, ni hatua muhimu inayokuwezesha kuiona nuru na kesho iliyo angavu. Letting go ni ushindi.
 
Back
Top Bottom