Leteni stori jamani!

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,105
2,499
Jumapili nimeamkia salama kabisa namshukuru Mungu, church nimehudhuria kama kawa, nimerudi nimefungua jf kuchungulia nipate mawili matatu, ila kwa lunch ya mchana bado sijapata ila nimepanga kukandamiza ugali dagaa siku ipendeze, kwema lakini huko mliko wakuu?
 
Ugali dagaa? aisee huo msosi nauzimikia ile mbaya...Mimi nimekandamiza ugali na kitu yai...kama umebaki nirushie kwenye PM
 
Kwetu kwema, tumanyunyu na radi za kutosha tu!

Ehe; church umetoka na ujumbe gani?
 
Kitaani kwetu Lambeti kakimbia, ana kesi ya kulala na binti wa darasa la sita, polisi wanamsaka.
Whats up kitaa kwenu, Papa Mopao?
 
Last edited by a moderator:
Ugali dagaa? aisee huo msosi nauzimikia ile mbaya...Mimi nimekandamiza ugali na kitu yai...kama umebaki nirushie kwenye PM

We njoo tu unakaribishwa kabisa ndugu yangu, dagaa roast na za kukaangwa kwa ugali ndo ugonjwa wangu kabisa!
 
We njoo tu unakaribishwa kabisa ndugu yangu, dagaa roast na za kukaangwa kwa ugali ndo ugonjwa wangu kabisa!

Lakini usiwe umetiwa ma-karoti na mazagazaga mengi....Only nyanya na vitunguu mafuta kwa mbali......Nina brother wangu tullivyokuwa wadogo akitumwa kununua nyama buchani atajifanya amesahau na kuleta dagaa!!!
 
Kwetu kwema, tumanyunyu na radi za kutosha tu!

Ehe; church umetoka na ujumbe gani?

Aaah safi sana, leo ujumbe ulikuwa mzuri sana Kaunga,

Ujumbe nilioupata church ni huu: Kulikuwa na Punda anambeba mtu anampitisha sokoni, sasa Punda wakati anapita hapo akashuhudia watu wanashangilia sana msafara wake wa kupita pale sokoni, akajiuliza hivi, "Nashangiliwa mimi au la?"

Kesho yake punda akataka kujua kama aliyeshangiliwa ni yeye ama yule aliyembeba jana yake pale sokoni, akapita pale sokoni peke yake akaona kimya watu wapo wapo tu wanaendelea na shughuli zake, baadaye punda akawauliza watu walioko pale sokoni, "mbona jana mlinishangilia sana na iweje leo mko kimya?" Watu wako kimya kana kwamba hawana habari naye.

Akasikitika, akaenda kumuuliza mama yake, "Mama mbona jana nilishangiliwa sana na leo sijashangiliwa sana kama jana?" mama punda akamjibu, "Aliyeshangiliwa ni yule uliyembeba jana siyo wewe, wewe ni kama punda wengine huna thamani yoyote ukiwa peke yako bila kumbeba yule uliyembeba jana, bila kumbeba yule huwezi fanya chochote upo upo tu"

Ujumbe: Punda anawakilisha sisi wanadamu, Yule mtu aliyebebwa anawakilisha Yesu Kristu, so kiroho ni kwamba tukiwa sisi kama sisi bila Yesu hatuwezi kufanya chochote, Tukimbeba Yesu ktk safari zetu za maisha yetu ndo tunaonekana wa thamani sana maishani mwetu na kila kitu kinawezekana!

So tumbebe Yesu Kristu katika safari zetu za maisha ya hapa duniani.

Hope umenipata Kaunga!
 
Lakini usiwe umetiwa ma-karoti na mazagazaga mengi....Only nyanya na vitunguu mafuta kwa mbali......Nina brother wangu tullivyokuwa wadogo akitumwa kununua nyama buchani atajifanya amesahau na kuleta dagaa!!!

Bila kusahau pilipili hoho kuongeza hamu ya kumalizia! Na maji ni muhimu sana kwa afya zetu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom