Leteni Maswali ya Kiafya Niwasaidie

Bwana Mafish Pole sana,Hata hivyo huko unakoita Chumvini ni sehemu yenye wadudu wengi sana kuanzia fungus,Herpes,bacteria n.k hivyo iwapo una hali mbaya mdomoni unaweza kuwa umepata fungus au vimelea wengine kutoka huko na kwa njia ya fecal oral route namaanisha baada ya kuingia chumvini ukashindwa kujisafisha vizuri mikono na mwili wako unaweza kupeleka maambukizi katika kinywa,hata hivyo nahitaji maelezo zaidi kama kuna vidonda kinywani au utando wowote kwa sas unaweza kuwa unatumia Mouth wash Solution ili kuondoa haufu mbaya kama kuna utando mweupe unaweza kutumia Nystatin cream 1mls mara nne kwa siku( in case ni fungus) otherwise nipe maelezo zaidi.

Pili tatizo la kutotumia Kondomu baada ya goli la pili is more psychological than physical hivyo,Jifunze kulinganisha thamani ya maisha yako na raha ya muda mfupi unayoipata huku ukiwa na uwezekanifu wa kupata maambukizi.Nakushauri pi uwe na mpenzi mmoja mwaminifu na mpime virusi ili hata kama usipotumia kondomu uwe salama
Mwisho Chumvini si mahali pa salama kabisana hapakuumbwa kwa kazi hiyo.Jitahidi kutumia viunga vya mwili kadri Mungu anavyotaka vitumie
Shukrani
 
Ni ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa insulin mwilini au Insulin kushindwa kufanya kazi ipasavyo kutokana ra Receptor kuwa insensitive kwa insulini
Aina
TYPE 1-Au insulin dependent hutokana na kuharibika kwa beta cells katika Islets of Langhans ambayo ndiyo inayotengeneza insulin hivyo insulin haiotatengenezwa
-huathiri zaini watoto na vijana
-Mgonjwa nahitaji kuchoma sindano za insulin mara kwa mara
-Mgonjw hufundishwa kujichoma mwenyewe sindano
-Mara nyingi mgonjwa huwa mwembamba
-Complication kubwa ni kupata Diabetic Ketoacidosis ambapo mgonjwa nakuwa na sukari nyingi > 250g/dl na anakuwa na 'ketone bodies, katika mkojo,acidosis na kuwa na upungufu wa maji

TYPE 2-au non Insulin dependent-hii hutokana na isulin kutofanya kazi vizuri mwilini kwa kuwa receptor zake zimeharibika
-Mara nyingi unene kupita kiasi hupunguza sensitivity ya insulin receptor
-Huwaathiri zaidi watu wazima na wanene
-Vipo vidonge kama vile Biguanides,Sulphonyl ureas husaidia
-Kufanya mazoezi na kumonitor diet ni vitu vya msingi

Pili,Kisukari kutibika moja kwa moja si rahisi sana ,kwa mfano mgonjwa wa type 1 anahitaji Insulin maisha yake yote na sijasioma sehemu kuona mgonjwa wa Type 2 amepona kabisa,ila unaweza kupunguza uwezekano wa kupata madhara na ukaishi muda mrefe
Madhara ya kisukari
-Kupungukiwa nguvu za kiume
-KUTOONA VIZURI
-Vidonda kutopona haraka hasa vya miguuni
-NEURONES kuharibika na kuharibu sensations za mwili
-Matatizo katika figo
-Kupungukiwa kinga ya mwili
SIKU JEMA
 
Shukrani Paloma kwa kutojali Avator yangu hata hivyo kwa kuwa nina muda mfupi leo nitakujibu kwa ufupi sana ila naahidi kukujibu kwa kirefu zaidi nikipata Muda,
Ni kweli unapokuwa na Grave's disease kuna baadhi ya vyakula ambavyo unashauriwa usile,kwa kuwa thyroid hormones (T3 na T4) zinakuwa nyingi mwilini,ni vema kuepuka vyakula ambavyo vitasababisha thyroid hormone zizidi mwilini,kumbuka pia hyperthyroidism inaweza kutokana na Iodine deficiency kwa hiyo vyakula vyenye madini hafifu ya Iodine havitasaidia,lakini hata vyakula vinavyo interfere Iodine metabolism pia si vizuri,vyakula hivyo huitwa Goitrogenic foods na mfano halisi kabisa ni kama Kabeji.Kuhusu antithyroid hakuna dawa isiyo na madhara,kwa mfano ukitumia antithyroid kwa muda mrefu unaweza kupata hypothyriodism ambayo dalili zake kubwa ni 'Cold intorelance' na kuna athari kubwa zaidi zinazoitwa thyroid crisis ambazo unahitaji kuwasiliana na daktari wako mara kwa mara.
Hata hivyo ni vema daktari akupe elimu ya kutosha kuhusu madhara ya dawa hizo hasa katika nguvu za kiume n.k
Nikipata nafasi ya kutosha nitakujibu kwa kirefu
Ubarikiwe.

Daktari niwie radhi kuingilia fani yako lakini naona hapa unatuchanganya. Mie sio daktari lakini nafahamu lugha. Kijineno (prefix) "hyper" humaanisha "-liyozidi" na "hypo" humaanisha "_liyopungua"(labda kama ninyi madaktari mnavitumia kinyume!) Sasa unapotuambia hyperthyroidism inaweza kutokana na iodine deficiency, wakati wataalamu wengine wanatuambia tutumie chumvi yenye iodine ili kuepuka hypothyroidism (yaani tusipungukiwe thyroid hormone) sisi tushike lipi? Uelewa wangu hadi sasa ni kuwa iodine husaidia kuongeza utengenezaji wa hiyo thyroid hormone, na mtu akiikosa huwa anapata hypothyroidism. Huyo mwenzetu anasema ana ugonjwa wa hyperthyroidism, yaani imezidi, sasa sielewi inavyoweza kusababishwa na iodine deficiency! Hebu fafanua dokta! Mimi hapo nilielewa labda mwenzetu atakuwa kazidiwa na hiyo iodine, kwa hiyo aiepuke kabisa! Pia hujamjibu mwenzetu swali lake, anauliza atumie vyakula gani? Hilo bado hujajibu, umeishia tu kumwambia vyakula kadha havitamsaidia, anataka kujua vyakula vitakavyomsaidia ni vipi (ili avitumie), na visivyomfaa ni vipi (ili aviepuke). Hebu jitahidi kuwa makini zaidi daktari ili tuweze kufaidi huo utaalamu wako. Shukran.
 
Aisee mganga. Mimi nimekaa nime-relax, ghafla ankle inauma ghafla hata siwezi kutembea. Sijacheza kabumbu kwa wiki kadhaa. Maumivu ni ghafla tu, wala hamna uvimbe. Sijaanguka kwenye baa ya baba Chuwa wala nini. Hii haijawahi tokea. Ni nini? Yaani noma, hata movement ya nanihii ni matatizo kidogo.

Nyoka hii nahisi imesababishwa na mchezaji mwenzako unayemuweka benchi, inakubidi uende bagamoyo na wewe!
 
Salau mkuu,
hebu nisidie hapa kuna mtu anaumwa sana miguu, hasa sehemu za unyayo, anasema anahisi kama vile miguu huko inawaka moto, sasa saidia afanyeje.
 
Hiyo inaitwa PERIPHERAL NEUROPATHY. Sababu zake ni nyingi
1. Acheki ngoma
2. Je anakula vyakula vyenye kumpa Vitamin B ya kutosha? Acheki damu inaitwa FULL BLOOD PICTURE waangalie size ya RED BLOOD CELLS
3. Acheki sukari

Naweza kumshauri pia atumie NEUROBION au NEUROTON kwa kipindi
 
Hiyo inaitwa PERIPHERAL NEUROPATHY. Sababu zake ni nyingi
1. Acheki ngoma
2. Je anakula vyakula vyenye kumpa Vitamin B ya kutosha? Acheki damu inaitwa FULL BLOOD PICTURE waangalie size ya RED BLOOD CELLS
3. Acheki sukari

Naweza kumshauri pia atumie NEUROBION au NEUROTON kwa kipindi

Tatizo la peripheral neuropathy ni pana sana na nilinaweza kusababishwa na moja ya yafuatayo:
# Ajali au maumivu ya nerve
# Kansa
# Utumiaji wa kemikali au toxins eg Zebaki, shaba, organophosphates nk
# autoimmune disease
# Upungufu wa vitamin
# Matimizi makubwa ya pombe
# Matumizi ya dawa eg TB na Kansa
# Magonjwa ya muda mrefu eg Diabetes, Kaswende, Renal failure nk

Matibabu yanategemea kujua chanzo cha tatizo. Dawa zilizotajwa na injinia zinasaidia kupunguza makali ya ugonjwa.
 
Dr. Mchumia Juani;

Humu JF kama kuna watu wanaopenda kuanzisha umbeya na mifarakano na pia wana mitazamo hasi (Negative Attitude), Tutawasaidiaje?

Je ugonjwa huo unaitwaje, Dalili zake ni zipi na matibabu yake ni yapi?
 
Hata mimi Daktari nahisi ndoa yangu iko mashakani...kwani nimegundua mama watoto ana uhusiano nje na jamaa mdogo wa umri wa 1st Born wetu!

Je nifanyeje Doctor?
 
Pole Mzalendo Halisi,
Mimi siku zoote naamini kuwa iwapo mama watoto wako atakuwa anaenda nje ya relationship kuna kitu ambacho hujafanikiwa kumpa na anajaribu kukitafuta nje-ni imani yangu tu ambayo si lazima na wewe uamini hivyo.
Naamini hivyo kwa sababu kama mkeo unaweza kumtosheleza kwa kila kitu kuanzia mahitaji ya kila siku na ya kimwili,i mean kitandani hata siku moja hawezi kwenda nje.Hili ni tatizo ktk familia nyingi na hasa kwa watu ambao wamekutana tu na kwa tamaa zao kimwili wakaamua kuoona pasipo kupata nafasi ya kuchunguzana kutambua nini mwenzio anapenda au hapendi.Lakini sasa tatizo limeshatokea hebu tuangalie ufumbuzi.Kuongea ni njia mojawapo kubwa ya kutatua matatatizo,nakupa tips kidogo tu.
1.Kama unafanya kazi jaribu kuchukua likizo
2.Bila kinyongo muombe mkeo na mwanao msafiri kwend sehemu nzuri kama vile mbuga za Wanyama e.t.c
3.Mkiwa huko kuwa mstaarabu na mpole mna mwonyeshe Mapenzi ya dhati
4.Ukijiridhisha kuwa ametulia tafuta sehemu tulivu na muulize ni kitu gani anapenda umfanyie lakini ambacho hujaweza kumfanyia hasa wakati mnafanya Mapenzi(hii inafaa zaidi kuwa sehemu ya maongezi ya mwanzo mnapojiandaa kufanya mapenzi-wanawake wengi hupenda kuelezea mambo wayapendayo .Kwa njia hiyo utajua chanzo cha yeye kutoka nje ya uhusiano kwa maana chanzo chaweza kuwa ni wewe.
5.Ukijiridhisha kuwa tatizo ni wewe jaribu kuangalia jinsi gani ya kubadilika na kuendelea na Maisha lakini kama tatizo liko kwake-kwani kuna wanawake wenye matatizo fulani yanayotokana na malezi ambayo hata ukimridhisha vipi atatoka tu nje ya uhusiano japo si njia nzuri sana lakini kumwacha ni solution.Kumbuka pale Mimba inapopitia ndipo hapo hapo virusi vya ukimwi vinapitia.Na mpaka mkeo azae na jamaa nje ni kielelezo tosha kuwa hakujali na muda wowote aweza kukuua kwa UKIMWI.
IWAPO NJIA HII HAITAFAA TUWASILIANE NITAKUIBIA TIPS KIDOGO TOKA KTK KITABU CHANGU KIPYA NNACHOKIANDAA CHA MAHUSIANO.
 
Kamanda
Kuhusu jamaa yako anayeumwa miguu naona Madaktari wenzangu wamekujibu na majibu yao yote ni sahihi.Mimi naongezea tu kwamba Magonjwa ambayo commonly yanakuwa na presentation kama hiyo yaani Peripheral Neuropathy kwa Tanzania ni Upungufu wa Vitamini B12 hasa kutokana na unywaji pombe uliokithiri,Kisukari na HIV.Haya ndo Common sana kwa kuwa Umeuliza cha kufanya nashauri afanye hivi;
1.Aache au apunguze kunywa pombe na azidi kula vyakula vingi vyenye madini ya vitamini B 12 kama vile nyama,maini n.k
2.Anaweza kutumia vidonge vya Vitamini B Complex kimoja mara tatu kwa siku kwa zaidi ya mwezi mzima.Hivi vipo tu ktk famasi na ni over counter prescription.
3. AU NEUROBIN FORTE KIMOJA MARA MBILI KWA SIKU
4.Pima Sukari kama utaambiwa iko juu fuata ushauri nilio wahi kuutoa wakati nimeongelea kisukari
5.Pima HIV,Kama ni positive unaweza kucheki na CD4 cell kama zinaruhusu kuanza dawa za kurefusha maisha
6.Amitryptilline tabs nazo husaidia sana
Ukijaribu mambo yote haya ikashindikana tuwasiliane zaidi
 
SPIDER MAN
Swali lako ni gumu sana kulijibu lakini niseme tu kwamba majungu,Umbea na mitizamo hasi vinaathiriwa na mambo mengi sana kama ifuatavyo:
1.Watu wanaokuzunguka-Kama watu wanaokuzunguka kila siku ni watua ambao umbea au majungu kwa ni hali ya kawaida wanaweza kuku infect na wewe kuwa mtu wa majungu au umbea
2.Uelewa duni wa Mambo kwa mfano kama wewe fani yako ni siasa halafu ukaja kuongelea mambo ya afya ambayo huna utaalamu nayo siku zote habari zako zitakuwa ni za kusikia watu wengine walivyosema na wewe ukaja ukaziropoka kwa wengine pasipokujua ni sahihi au la.
3.Masilahi Binafsi- kwa mfano kama wewe ni mla rushwa ni rahisi san kutetea hoja za wala rushwa na kuponda wale wanaopinga rushwa kwa kujaribu kulinda heshima ya territory yenu ya wala rushwa.
4.Hallucinations-ni tatizo la kisaikolojia ambalo wewe unaona mambo vile ambavyo wengi wanaona hayako hivyo na lazima utakuwa na Negative thinking.Hallucination yenyewe haitoshi kumweka mtu katika category yoyote na disease ila ukiwa na hallucinations na tabia nyingine kama woga,wasiwasi,mashaka n.k unaweza ukawekwa kwa watu wenye Depression
5.Stress za kimaisha,kimahusiano n.k
6.Mazingira uliyokulia,Malezi uliyolelewa,Hali yako ya kiuchumi.,Uwezo duni wa kuchambua na kuelewa Mambo n.k vyote vinasababisha mtu awe na tabia hizo za umbea.
CHA KUFANYA
.Ni kumuelimisha zaidi muhusika
.Kumpa Support kifikra
.Kumshauri apunguze Stress n.k
 
MJ,
Habari za kwako Mkuu?

Mimi swali langu ni kama ifuatavyo:
Kwanini binadamu huweza kukumbuka tukio lililotokea hata miaka mingi labda 30 au na zaidi na wakati mwingine hushindwa hata kukumbuka tukio lililotokea muda mfupi, kama vile wapi ameweka funguo nk?

Je, ni kweli kila tunachokiona na kusikia kinahifadhiwa katika kumbukumbu zetu kwa maana kwenye ubongo? Kama ndivyo, je tufanye nini ili tuweze ku-retrive hizo kumbukumbu?
 
Mtaalamu, kuna swali aliwahi kuuliza mdau kuhusiana na maumbile ya wadada. Na aliuliza kuhusu wanawake wenye sehemu ndogo wanatibiwaje...?? Manake wasiwasi mkubwa ni wakati aidha wa kujifungua na kwa wengine hata tendo la ndoa linakuwa utata.

Swali hili halikujibiwa, ningependa kuona solution ya hili tatizo.
 
Sasa doctor vipi kuhusu Sinus inakuwaje na inaambukizwaje na side effect zake ni zipi na dalili zake ni zipi na kwa Tanzania ikoje au ni Ulaya tu?
 
Dr, avatar yako inavutia yani ukiiona unashtuka kwanza kisha unataka uendelee kuitizama....nadhani ni therapy inayosaidia ubongo ukae sawasawa.....(sijui?!?!?)

Dr, mtaani kwetu...huku uswahilini barabara ya 11...aliniambia kitu nikashtuka! Ati wakati fulani waifu wake alipokuwa mjamzito dalili zote za mimba zilihamia kwa huyu bwana. Yani kichefuchefu chake, asubuhi anatapika yeye, juisi ya ukwaju anywa yeye, na udongo pia (wao wauita pemba) alikuwa anakula! N hata siku ya kujifungua yeye alikuwa hoi kwa kuumwa hata kazini hakwenda wala kumsindikiza mkewe hospitali hakuweza-naye alipata uchungu wa aina yake!

Hebu nisaidie kwani nachanganyikiwa!
 
Mimi ni mgonjwa wa PUMU kwa muda mrefu. Madawa ambayo nimekuwa nikitumia, miaka nenda rudi, ni aminophylline na ephedrine.

Je, hakuna ugunduzi wa dawa nyingine uliofanyika katika kipindi chote hiki? Ningeomba unieleze wapi zinaweza kupatikana.
 
Back
Top Bottom