Leonardo Da-Vinci


...........kuna mungu mwingine kamtoa kafara mwanae wa pekee auawe kifo kibaya cha laana !:shock: @Eiyer
 
Njoo tujadili apocrypha!

Mkuu ukitaka tujadili vitabu vya Apocrypha kwa mrengo wa kwamba walio viondoa walikosea tutakuwa tunakosea sana....M
Maana hata Martin Luther aliondoa vitabu 7 vya Agano la kale akabakiwa na vitabu 66.....Pia alitaka kuondoa kitabu cha James ila reformer wenzake wakina Calvin walimkataza....
Huenda leo kuna wakristo wangekuwa na vitabu 26 vya agano Jipya..

Sasa cha msingi ni kujua kwann waliviondoa.....Kwann waliviita Heretical....Kwasababu hata Injili zilikuwa 24 ila kwenye mtaguso wa Effeso walichambua wakabakiza 4...Sasa mm naamini kuna sababu nzuri tuu ya kuvikataa vitabu hivyo..

Kumbuka Biblia ni mkusanyiko..

Eiyer tafadhali usiharibu mjadala maana naona huna unalolifahamu zaidi ya hisia kali na ushabiki huku ukijawa na maswali ambayo hata wewe huwezi kuyajibu japikuwa umeyauliza..
 
Last edited by a moderator:
...........kuna mungu mwingine kamtoa kafara mwanae wa pekee auawe kifo kibaya cha laana !:shock: @Eiyer

kwa kufuata iman au din yako mambo gani ni mema?

Je mnatumia fact au kipimo kipi kubaini wema wa hayo mambo?
 
Kwa haya maandiko yako yanaonesha ujinga [kutokujua] mkubwa ulionao kuhusiana na maandiko na kilichofanya yakawepo kwa utaratibu uliopo

Lakini cha kushangaza zaidi ya kushangaa kwenyewe ni kuwa umenilaumu mimi kwa "kuamini" kuwa kila kilichopo kwenye biblia kuwa kimetoka kwa Mungu bila kutiwa mikono na watu wakati watu hao hao ndio walioandika,halafu ukaweka kioja kingine kuwa "original manuscript" eti iliishia sijui 16:8,hapo kuna vioja viwili

1: Inaonekana hujui mtu anamaanisha nini anaposema hayo ni maandiko kutoka kwa Mungu kwasababu kitendo chako cha kudai kuwa unashangaa wakati maandiko yenyewe yameandikwa na watu inaonesha umaimuna mkubwa sana ulionao kuhusiana na suala zima la uandishi na kauli ya "maneno kutoka kwa Mungu"

2: Umedai kuwa kuna "original manuscript",sijui huo u-original unautoa wapi na kipa hiyo manuscript yako kutokana na hiyo dhana hapo juu,kama maandiko yote yameandikwa na wanadamu basi either yote ni original au yote ni fake kutokana na context ya maelezo yako hapo juu na sijui kama una uwezo wa kung'amua hili

Kwa kifupi umohoroja tu hapa na hakuna ulichosema chenye mantiki
Iron Lady yuko sawa kabisa.
Nadhani hata hujui maana ya "sawa" wewe

Hivi hujui hata wewe uko sawa?

Mtu yoyote yuko sawa kutokana na kile anachokisema ila kuthibitisha asemacho ni suala lingine

Nikikuambia uthibitishe haya maelezo yako tutakesha hapa

Na kikubwa sana hapa hatutafuti mshindi bali tunaweka maelezo ambayo kama kuna msomaji ataona yana mashiko basi atayachukua na kuyafanyia kazi,kama unatafuta aliye sawa na asie sawa utakesha kwa kuwa hata hiyo sawa yenyewe inategemea na mtu mwenyewe anaeona jambo kuwa sawa

Wewe unaweza kuona ni sawa kujisaidia shambani mwako ili hiyo mbolea inayotoka tumboni mwako irutubishe mazao utakayokuja kulima baadae na kuna mwingine hataona ni sawa kufanya hivyo na nyote mkawa sawa kwa mujibu wa kila mmoja
Biblia tunayoijua leo,ni tofauti na Biblia za mwanzo.Kuna vitabu viliondolewa na ukiuliza kwanini viliondolewa,watakwambia ni heretical.Ukiuliza wamejuaje ni heretical na kwanini hivi vilivyopo visiwe heretical?Hutapata majibu ya kuridhisha.
Kabla ya kuanza kutupigia gitaa lako la "hii biblia tuliyonayo leo haiko sawa na ya mwanzo" inabidi kwanza uthibitishw uwepo wa hiyo biblia na pia uthibitishe kuwa mwanzo ni kitu gani halafu thibitishe madai yao kuwa ni heretical kuwa sio ya kweli maana wao kutokukupa majibu ya "kukuridhisha" wewe sio uthibitisho wa kuwa hayo maandiko ambayo kwanza hata hujayathibitisha kama yapo kuwa sio heretical
Tatizo lako kubwa ni wewe kudhani kuwa kitendo cha mtu kuongea na mitume basi akiandika barua basi nayo ni neno la Mungu

Mbona humsemi Timotheo?
Hivi unajua kuwa ni wangapi waliongea na mitume?
Unataka maandiko yao wote yawepo kwenye biblia ili iweje?

Sio kila walichokiandika kinawekwa kwenye maandiko matakatifu na ndio maana nakuambia kuwa wewe una umaimuna mkubwa sana kwenye eneo hili na kibaya zaidi hujajua hilo
Njoo tujadili mkuu kama una muda japo tuko nje ya mada husika!
Tayari nimeshajadili!
 
Eiyer tafadhali usiharibu mjadala maana naona huna unalolifahamu zaidi ya hisia kali na ushabiki huku ukijawa na maswali ambayo hata wewe huwezi kuyajibu japikuwa umeyauliza..

Ndugu umenifanya nicheke sana

Sijui kama umeufuatilia huu mjadala

Lakini kikubwa sijui hata umejuaje kuwa sina ninachokijua na kituko kikubwa zaidi ni kuwa huyo ambae hana anachokijua anawezaje kuuliza maswali ambayo hayana majibu

Kwa ushahidi huu wewe ndio unaeharibu mjadala!
 
eiyer sasa naona unaaza ku-atack baadala ya kujenga hoja
 

Kwanza sio kweli kuwa "ametupatia mfalme" bali yule ni muovu,halafu kingine ni kuwa sio kweli ana nguvu kutushinda sisi bali sisi tuna nguvu kumshinda yeye kupitia kwa Mungu mwenyewe ambae ni Yesu Kristo

Kuna kitu kinaitwa basis,huwezi kujua chochote kile kama hujajua basis za kitu husika,hapa kuna right and wrong,hivi vyote vina basis zake zinazovifanya kuwa tofauti

Nje ya Mungu hakuna uovu na wema kwakuwa kipimo pekee cha huo ubaya na wema ni Mungu mwenyewe na yeye ndie ametupa basis za kujua uovu ni upi na wema ni upi na zaidi sana ameturahisishia kwa kutuambia siri za muovu kuwa hana chochote cha kutushinda sisi!
 
eiyer sasa naona unaaza ku-atack baadala ya kujenga hoja

Unajua hoja ni nini ndugu?

Halafu hii tabia ya kuongea bila kuonesha vile ambavyo nime attack sio uungwana kwa mtu ambae anajidai kutaka hoja

Nikija nikasema hapa kuwa wewe unaabudu jiwe bila kuthibitisha nitakuwa sahihi kweli?
 
kwa kufuata iman au din yako mambo gani ni mema?

Je mnatumia fact au kipimo kipi kubaini wema wa hayo mambo?

Jibu:

'Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu (Qur'an) na Manabii (woote !), na ana wapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima, na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi (kutoa mtu katika utumwa) na akawa ana shika Sala, na akatoa Zaka na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa Vita. Hao ndio waliosadikisha, na hao ndio wajilindao.
Qur'an: 2:177.
 
Da Vinci ana vitu vingi vilivo-fail pia kwa hiyo sio kila alichofanya kionekane kikubwa kama wenzetu wanavokuza.. mfano alichora mashine ya kutumia gravity kugenerate perpetual motion (kwamba itaendelea kuzunguka siku zote) na hii ina maana basi mashine hii ingeweza kuproduce umeme wa bure kabisa... It was an epic fail..
 
Mutabaruka huna maana ! ..........stori za vijiweni unaleta JF !:loco:
 
Last edited by a moderator:
........post yako No. 309 ulikuwa na tatizo gani !?
Nimekuuliza kama wewe una tatizo na hilo ulilolisema na wala sijakuuliza kama post yangu hiyo ina tatizo

Unaweza kuelewa kweli wewe?
 

Tunamshinda kupitia Mungu? Sasa unasemaje kama ana nguvu chache kuliko sie!

Wakati we pass through someone to win ! Naweza amin vip kama nina nguv wakati nashindiwa na mtu!
 
Tunamshinda kupitia Mungu? Sasa unasemaje kama ana nguvu chache kuliko sie!

Wakati we pass through someone to win ! Naweza amin vip kama nina nguv wakati nashindiwa na mtu!
Kwani sisi ni nani na tunaishi kwa uwezo wa nani mkuu?

Tuna chochote kwenye maisha yetu ambacho tumekipata kwa uwezo wetu [kama tunao]?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…