Leo zamani (kabrasha la kumbukumbu)

Tar 4/10 ni siku ya 278 bado siku 88 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya kitaifa
1911 safari za treni Dar Tanga zilianza rasmi kwa kutumia treni ya mvuke uliotokana na makaa ya mawe
Kimataifa
1966 ni uhuru wa nchi ya Lethoto iliyozungukwa pande zote na nchi ya Afrika kusini
1910 nchi ya ureno yajitangaza kuwa jamhuri baada ya kumng'oa na kumtimua mfalme Manuel
 
Leo ni tar 6 ni siku ya 280 bado siku 86 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya kitaifa
1958 mkutano mkuu wa TANU waanza na kuweka lengo la Kufukuza wote wanaokisaliti chama , mmojawapo wa aliyeathirika ni Zuberi Mtemvu
1986 waziri wa afya Aaron Chiduo atoa rai ya kutumia dawa za asili kwenye kutibu malaria kwenye mkutano wa kimataifa wa dawa za asili Arusha
Kimataifa
1981 rais wa Misri Anwar Sadat apigwa risasi siku moja tu baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo
 
Leo ni tar 22 siku ya 296 baki siku 70 kumaliza mwaka 2016

Matukio ya kitaifa
1959 mwalimu alizindua hotuba kwenye hafla ya uwashaji mwenge
Baadhi ya maneno kwenye hotuba hiyo ni sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro umulike hata nje ya mipaka yetu ulete tumaini...
 
Leo ni tar 24 ni siku ya 298 bado siku 68 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya kitaifa
Mwaka 1970 kuanza kwa safari ya kwanza ya treni ya TAZARA kutoka Zambia Kapiri Mposhi kuja Tanzania
Treni hiyo ilizinduliwa jana yake tarehe 23

Matukio ya kimataifa
Mwaka 1964 kumbukumbu ya uhuru wa Zambia ambapo rais wake wa kwanza alikuwa Kenneth Kaunda chini ya chama cha UNIP
 
Leo ni tar 25 ni siku ya 299 bado siku 67 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya kitaifa
Mwaka 1958 Dustan Omani awa DC wa kwanza mweusi Tanganyika
Mwaka 1961 Chuo kikuu (UDSM) chazinduliwa kwenye jengo la SUKITA
Mwaka 1969 Grey Likungu amshawishi mtu mmoja huko jijini Nairobi aungane na Kambona katika mipango ya kuipindua serikali..Chipaka na Bi Titi Mohamed pia walihusishwa kwenye kadhia hii

Kimataifa
1881 kuzaliwa kwa Pablo Picasso mchoraji maarufu duniani, michoro ya Picasso ni ghali na maarufu mpaka leo
 
Leo ni tar 26 ni siku ya 300 bado siku 66 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya kitaifa
-Mwaka 1970 uzinzi wa ujenzi wa reli ya TAZARA waanza rasmi reli hii yenye urefu wa km 1859 ilizinduliwa na rais Kenneth Kaunda huko Yombo
-mwaka1980 Rais wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi achaguliwa tena kuwa rais
-mwaka1955 Mwalimu Nyerere arejea Dar toka Musoma baada ya kuacha kazi ya ualimu kwa hiari Pugu sekondari mwaka mmoja
 
Charles Taylor sio Tyler
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…