Leo usiku ilinitokea hali ya kukabwa na jinamizi

Ni baada ya usingizi kukata nikabadili mkao wa kulala kwa kusogeza kichwa na shingo juu ya mto.

Baada ya kupitiwa na usingizi tena ndani ya dakika kadhaa.

Ghafla nikaona kunamwanga amepitisha mkono ndani ya shuka akaniwekea shingoni mkono wake akawa ananikaba bila kutumia nguvu kubwa.

Nikawa najaribu kuamka ili nijinasue ila na shindwa nikaishia kufurukuta tu huku nikiwa na hofu kubwa sana

Nikawa najiuliza maswali kwanini mchawi anikabe wakati nili sali ? . Tena nili sali mara mbili kwa usiku mmoja kabla na baada ya kushtuka.

{ Kwa hofu nikawza au hua na sali kimakosa ? Maana mimi sina dini naiombaga roho yangu mwenyewe }.

Nikarudia kusali upya !

Muda huo bado jinamizi limenishika.

Baada ya kusali tena ndipo nikashtuka na kuamka. Ila baada ya kuamka nikajua tu nilijibana shingo kisa kuhegamia mto.

Lakini kilicho nitoa hofu tayari nilikua naelimu ya hali hiyo nilichofanya kikajiweka vizuri nikalala tena.

{ Huenda kwa mtu asiye ijua hali hiyo angeamini kua alikabwa kweli }

✍️
OK broo. Kama umeweza kubaini tatizo na kuondokana na imani ya kukabwa kweli; sasa umeleta hoja hapa ili sisi tufanyeje? By the way, asante kwa darasa zuri.
 
Jinamizi la kike au la kiume?
Kama ni wa kike nipe no zake
 
Ni baada ya usingizi kukata nikabadili mkao wa kulala kwa kusogeza kichwa na shingo juu ya mto.

Baada ya kupitiwa na usingizi tena ndani ya dakika kadhaa.

Ghafla nikaona kunamwanga amepitisha mkono ndani ya shuka akaniwekea shingoni mkono wake akawa ananikaba bila kutumia nguvu kubwa.

Nikawa najaribu kuamka ili nijinasue ila na shindwa nikaishia kufurukuta tu huku nikiwa na hofu kubwa sana

Nikawa najiuliza maswali kwanini mchawi anikabe wakati nili sali ? . Tena nili sali mara mbili kwa usiku mmoja kabla na baada ya kushtuka.

{ Kwa hofu nikawza au hua na sali kimakosa ? Maana mimi sina dini naiombaga roho yangu mwenyewe }.

Nikarudia kusali upya !

Muda huo bado jinamizi limenishika.

Baada ya kusali tena ndipo nikashtuka na kuamka. Ila baada ya kuamka nikajua tu nilijibana shingo kisa kuhegamia mto.

Lakini kilicho nitoa hofu tayari nilikua naelimu ya hali hiyo nilichofanya kikajiweka vizuri nikalala tena.

{ Huenda kwa mtu asiye ijua hali hiyo angeamini kua alikabwa kweli }

✍️
Watu hukabwa kupitia hali zao.
 
Wewe ni AI. AI pekee ndio anaweza kutoa maelezo kama yako kwasababu kawekewa data. Naomba nikupe practical moja urudie zoezi. Uende kwenye nyumba moja ipo Mbagala ulale hapo siku moja. Kesho utupe mrejesho. Kama upo tayari sema hapa.
 
Back
Top Bottom