Leo tuwaenzi na kuwakumbuka wazazi wetu waliotangulia mbele za haki

To yeye

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
28,210
65,813
Kama umelelewa na ndugu, watu baki, au na mama pekee au baba pekee kutokana na kufiwa na mama, au baba ama wazazi wote. Tuwakumbuke na kuwaombea waendelee kulala mahali pema peponi. Nasi tutafuata japo hatujui kama tutakutana njia moja. Tuendelee kumwomba Mungu atupe mwisho mwema.

Nimejikuta siko sawa kwa muda baada ya kumkumbuka marehemu baba aliyekufa nikiwa na miaka mitatu. Kumbukumbu niliyobaki nayo ni kuambiwa na mama kwamba baba alikuwa ananipenda sana😭😭😭.

Mliojaaliwa kulelewa na wazazi wote wawili hongereni na msiache kuwapenda wazazi wenu, wahudumieni msichoke. Hivyo unavyobania kuwapa wazazi katu hutozikwa navyo, watachezea na kutapanya wengine.

Mungu ambariki mama yangu, aendelee kujaaliwa afya njema, amepambana sana mpaka nimefikia hapa.

Poleni sana wahanga, duniani tunapita wote pambaneni na maisha mpaka tone la mwisho la jasho na damu👊.

Andika R.I.P kwa mzazi aliyekwisha tangulia mbele za haki, kuna member atakupa pole kwa kureply comment yako, utajisikia vyema.🙏🙏🙏

Mungu awabariki sana 🙏
 
Nilimpoteza Mzee wangu nikiwa na miezi 10, kutokea hapo nimelelewa na Mama pekee.

Bahati mbaya kabla sijapata kazi naye akafariki bila kuonja hata elfu 1 yangu.

Graduation ya form six na chuo kikuu zote nimezifanya bila uwepo wao.

Kuna wakati huwa nahisi huyu Mungu anapendelea. Kwanini awachukue Wazee wangu wote asiniachie hata mmoja wakati kuna wenzangu wana wazazi wote ama hata mmoja tu.

Anyways, safari ni yetu sote but it really pains 😭😭😭

Wale wenye Wazazi msiache kuwaombea na tafadhalini jaribuni kuwajali hata kwa kidogo mlichonacho.
 
😭😭😭😭Kuna muda unajikuta unalia tu....but it's okay
 
Kama umelelewa na ndugu,watu Baki,au na mama pekee au baba pekee kutokana na kufiwa na mama,au baba ama wazazi wote.Tuwakumbuke na kuwaombea waendelee kulala mahali pema peponi....nasi tutafuata japo hatujui kama tutakutana njia Moja.Tuendelee kumwomba Mungu atupe mwisho mwema.

Nimejikuta siko sawa Kwa muda baada ya kumkumbuka marehemu baba aliyekufa nikiwa na miaka mitatu....kumbukumbu niliyobaki nayo ni kuambiwa na mama Kwamba baba alikuwa ananipenda sana😭😭😭

Mliojaaliwa kulelewa na wazazi wote Wawili hongereni na msiache kuwapenda wazazi wenu,wahudumieni msichoke....hivyo unavyobania kuwapa wazazi katu hutozikwa navyo,watachezea na kutapanya wengine.
Mungu ambariki mama yangu, aendelee kujaaliwa afya njema....amepambana sana mpaka nimefikia hapa.

Poleni sana wahanga....duniani tunapita wote pambaneni na maisha mpaka tone la mwisho la jasho na damu👊
Andika R.I.P Kwa mzazi aliyekwisha tangulia mbele za haki....Kuna member atakupa pole Kwa kureply comment yako.....utajisikia vyema.🙏🙏🙏
Mungu awabariki sana 🙏
Asante To yeye kwa kukumbusha hili
 
Back
Top Bottom