Live Kutoka Mbinguni/ Welcome back to Heaven

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,162
22,684
INTRODUCTON:

Shalom!!

Nawakaribisha tena Mbinguni, Mbinguni ndiko tulikokuwako milele kabla ya Mungu kutuleta duniani kupitia pumzi ya uhai Kwa baba na mama zetu wa duniani.

Mbinguni ni wapi?

Hapa tunapoishi ni Mbingu ya kwanza, Mbinguni tunapoongelea Leo ni Mbingu ya tatu. Ukiigawa katika matabaka inajulikana ni Mbingu ya saba. Huko ndipo tutakapokuwa tukipaangazia katika mada hii Kwa muda mrefu sana. Ni lifetime experience, maana Yesu huwachukua watu wengi sana na kuwapeleka Mbinguni Kisha huwarudisha Ili walete shuhuda Ili kuwaimarisha WATAKATIFU walioko duniani.

MY LIFE EXPERIENCE.

Nilipokuwa mdogo sikumbuki miaka, lakini nakumbuka kumbukumbu hiyo nzuri kuwahi kuipata katika Maisha yangu hapa duniani.

Nalikuwa katika njonzi, ghafula, kufumba na kufumbua, nilikuwa katika Nchi nzuri ambayo uzuri wake hauelezeki.

Palikuwa na Nuru njema sana iliyong'aa, mwonekano wa Nuru Ile ,haukufanana na Nuru ya mchana Wala Nuru ya mbalamwezi wakati wa usiku.

Niliangaza kulia na kushoto, nyuma Ili nione asili ya Nuru Ile bila mafanikio, nilijaribu kupiga hatua nione wapi Nuru Ile njema ilikotokea, Nuru Ile haikuchoma kama mwanga wa jua, palikuwa tulivu na pazuri sana, moyoni nilijawa na furaha tele kuwapo katika Nchi Ile ambayo haikuwa na Jua Wala mwezi lakini ilijaa Nuru nzuri yenye kuvutia sana.

Kila nilipoongeza hatua kuikaribia Nuru Ile nzuri yenye RANGI nzuri ambazo kamwe Hadi Leo hii sijawahi kuziona katika Ulimwengu huu, Nuru Ile ilizidi kuwa mbali nami na nilizidi kuifuata lakini kamwe sikuweza kufika mwisho, Mahali pale na Nchi Ile nilitamani sana kuendelea kuwepo. Lakini Kwa Bahati mbaya nilistuka nikiwa nimelala kitandani na nilipatwa na huzuni kurudi katika mazingira haya ya hapa tulipo.

Katika mada hii nitakuwa nikikuletea shuhuda za Raia waliotoka Mbinguni, waliopelekwa tena Mbinguni na kuonyesha uzuri wa Mbinguni Ili kuja kuwatia moyo WATAKATIFU Duniani waendelee kuvumilia Ili siku ikifika waingie mji Ule mzuri.

LIVE KUTOKA MBINGUNI. ( Na Adam Mbaya).

Nilipokuwa katika kusoma BIBLIA, BWANA Yesu alinitokea na kuniambia kuwa, Leo nitakupeleka Mbinguni, Mahali pazuri makazi ya WATAKATIFU.

Ghafula nikajiona nimegawanyika, niliona mwili wangu Ukiwa chumbani na Mimi nikiwa naelekea juu sana Kwa Kasi ya ajabu.

Tukiendelea na safari Ile Hadi tulipofika Mahali ambapo palikuwa na mpaka kati ya uumbaji nyuma yetu, na umilele mbele yetu.

Nyuma yetu Mahali pa uumbaji niliweza kuona nyota nyingi, lakini mbele yetu katika umilele, hapakuonekana mwisho wake.

MAPOKEZI YA MBINGUNI/HUDUMA YA NYUMBANI.

Tulipofika Mahali hapa, naliona Malaika wengi sana na WATAKATIFU ambao walikuwa wanapokelewa Ili kujiandaa kupanda Mbinguni juu zaidi.

Mahali pale palikuwa pazuri sana ambapo uzuri wake Si Rahisi kuelezea,

MUZIKI.

Malaika walikuwa wakiimba huku wakipiga vifaa mbalimbali vya MUZIKI ambavyo vipo hapa duniani na vingine ambavyo SIKUWAHI kuviona kabla.

Mahali hapa palikuwa na furaha tele,WATAKATIFU waliopokelewa Mahali pale walikuwa wenye furaha tele na walipongezana na kukumbatiana Kwa furaha. Palisikika mziki mkubwa na mzuri sana wa kumsifu Mungu.

Zilisikika nyimbo nzuri za kusifu na kuabudu ambazo huimbwa hapa duniani, nilishangaa kusikia nyimbo hizo Mahali pale na nilimuuliza BWANA Yesu kuwa kwanini wanaimba nyimbo zetu.
Yesu alijibu, duniani Kuna uchafuzi mkubwa hivyo Mungu hutuma neno lake kupitia nyimbo Ili kubariki WATAKATIFU.

MIILI YA WATAKATIFU.

Mwonekano wa miili hiyo ya WATAKATIFU ilionekana kama miili ya kioo, transparent , iliyong'aa sana. Na umri wa WATAKATIFU walipofika pale mapokezi ya Mbinguni ilionekana sawa wote walionekana wenye umri sawa kama miaka 30 hivi. Hapakuwa na Mzee aliyeingia Mbinguni na uzee wake,hapakuwa na mgonjwa Wala mlemavu, walipewa miili Bora. Hapakuwa na njaa, Wala huzuni Wala DHIKI.

MIILI ya WATAKATIFU ilizidiana kungaa, wahubiri INJILI waling'aa sana miili Yao, waliotunza na kuhudumia wajane, yatima, maskini,wagonjwa Kwa pesa zao pia waling'aa sana.

NDOA.

Mmoja wa WATAKATIFU aligeuka na kumwona aliyekuwa mume wake alifika Mahali pale pa mapokezi na walikumbatiana Kwa furaha na kulia machozi ya furaha.

Hapakuwa na NDOA Mahali pale kama duniani,mke na mume waliitana kaka na dada, na tamaa za mwili hazikuwepo Mahali pale, palifunikwa na furaha na utukufu wa Mungu.

VYAKULA.

Malaika wengine walikuwa wakiwahudumia WATAKATIFU MATUNDA YA MWILI WA DHAHABU. Niliona pia Malaika wakimimina juice Kwa watakatifu ambayo ilikuwa ya kipekee.

Nilitamani kunywa juice Ile lakini Yesu aliniambia kuwa juice Ile ni spesho Kwa washindao ambao ni WATAKATIFU.

Nilimwona pia Malaika mmoja akiwa anakula EMBE!! Nilimuuliza, BWANA, Pana maembe huku?

Yesu alinijibu vyakula vyote vilivyoko duniani, vipo Mbinguni na zaidi ya hapo. Pana miti mingi ya matunda mengi ambayo mengine hayapo duniani, Mbinguni ni kizuri sana.

Yesu aliniambia huku Kuna Kila chakula Cha asili kulingana vyakula WATAKATIFU walivyokula duniani, na Malaika walihudimia WATAKATIFU, walipika na kuwahudumia maana ni Wana wa ufalme. Malaika walivutiwa sana kuwaona WATAKATIFU maana wakishinda Hila na majaribu ya mwovu duniani.

NJIA ZA MBINGUNI.

Palikuwa na njia 12 zilizokuwa na Majina ya Wana wa Israel/ Yakobo.


MALANGO YA MBINGUNI.

Pia palikuwa na Malango 12 ya Mbinguni yaliyoandikwa Majina 12 ya Wana wa Israeli kama zilivyokuwa njia zile 12. Na Kila lango alisimama Malaika mlangoni mwenye upanga mkubwa.

MAGARI YA MBINGUNI.

Baada ya mapokezi ya mahali pale, Malaika alipuliza tarumbeta kuwaarifu WATAKATIFU waliokuwa mapokezi ya Mbinguni kupanga foleni Ili kupanda magari ya Mbinguni kuwapeleka juu zaidi Mbinguni.

Yalishika magari ya Dhahabu, yenye kuwaka moto mtakatifu yaliyokuwa yakiendeshwa na Malaika, na Malaika waliwaongoza WATAKATIFU kupanda magari hayo yaliyokokotwa na farasi. Mahali pale na uzuri Ule hauelezeki.

ITAENDELEA......
 
Achana na hadithi zisizo na kichwa wala miguu hakuna kitu kinaitwa Mungu wala mbinguni.

Achana na ndoto za mchana.
Kwa hili unajifurahisha mkuu na hutupotoshi ng'ooooooo maana nyie wachawi, walozi, waganga na waganguzi ndio mnakuja humu kudanganya vijana kuwa hakuna Mungu wala Mbingu wala uchawi ili muwashughulikie. Angalia tu ID yako inaeleza Mengi.
 
Achana na hadithi zisizo na kichwa wala miguu hakuna kitu kinaitwa Mungu wala mbinguni.

Achana na ndoto za mchana.
Wewe kinachokusumbua na kukupa kiburi inawezekana unakanafasi ya kujipatia ugali hivyo unawakika wa kula na kujamba,pia hujakutana na misukosuko ya kiafya na maisha sana hapa duniani..hivyo kiburi chako hutoka huko ..tupe facts na evidence basi kwa unachachoamini kwasababu kuna ushaidi ya uwepo wa Mungu mpaka sasa..mfano uwepo wa mwanadamu,viumbe vyote,vitabu vya dini,dunia n.k

Ipo siku Mungu atagusa hiyo afya yako kidogo alafu tukuone ukijiponya.
 
Kwa hili unajifurahisha mkuu na hutupotoshi ng'ooooooo maana nyie wachawi, walozi, waganga na waganguzi ndio mnakuja humu kudanganya vijana kuwa hakuna Mungu wala Mbingu wala uchawi ili muwashughulikie. Angalia tu ID yako inaeleza Mengi.
Ubarikiwe.
 
Achana na hadithi zisizo na kichwa wala miguu hakuna kitu kinaitwa Mungu wala mbinguni.

Achana na ndoto za mchana.
Ubarikiwe pia.

Nakuombea usiishie kusikia habari za Mbinguni na Mungu, nakuombea akutane nawe binafsi.

Amen.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom