Leo TANESCO mmetuweza

Leo TANESCO mmetuweza

Endeleeni kuwa wavumilivu gas imefika mkuranga baada ya wiki ijayo bomba litakuwa limesha jaa gas ya kutosha kuendesha mitambo yetu ya ubungo
 
Katika watu siwezi kuwaamini ni viongozi wetu wote wa ukawa. Ni waongo kupindukia
 
Watu umeme unakatika siku moja mnalalamika tuulizeni sisi huku Mbeya balaa linalotukuta ni full matatizo
 
Hizi hasira tunzeni hadi tareh 25 zinaweza saidia kufanya maamuzi magumu.
 
Tabata nako watu tunatembea na tochi muda huu kutokana na giza totoro tangu ukatike saa kumi alfajiri ya leo
 
Yaan Leo nimezunguka Kariakoo, mwenge, Tabata, magomeni, maeneo ya chuo natafuta umeme nikamilishe ishu flani hivi lakini kooote huko holaa.., Tanesco wamenitesa na kunitia hasara kubwa Sana Leo.., nafanya mawasiliano na mwanasheria kwa ushauri zaidi
 
Nakumbuka Nigeria chama tawala walipohisi kupigwa chini na wananchi baada yakuchoshwa na ufisadi wa chama hicho mafuta yalianza kuwa adimu nchini humo, hiyo ikawa kama juu ya kidonda msumari wa moto, wananchi wakamalizia hasira zao kwenye sanduku la kura.......

Nyie subirini, mwaka huu jua litachomozea Magharibi
 
Mtoni kwa aziz ally tangu jana usiku mpaka sasa haujarudi
 
hali hiyo ndo nyie mpo mjini sasa sisi wakulima huku vijijini tulishaona nijambo la kawaida tu ila tunashukulu tuna cm za tochi zinasaidia
 
Yaani umeme nchi hii imekuwa kama vile tunapewa hisani tu na sio haki yetu.Na ndio maana umeme ukirudi tu utasikia "huooooooo"kwa kuwa tunahisi ni kama zawadi tu ambayo tunastahili kupewa au kutokupewa.
 
Back
Top Bottom