Leo nitaelezea kwa uchache sana juu ya suala la Ugoni, moja ya jambo linalofanyika sana kwenye jamii zetu

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
UGONI NI NINI KISHERIA?

Leo nitaelezea kwa uchache sana juu ya suala la Ugoni, moja ya jambo linalofanyika sana kwenye jamii zetu.

Kumekuwepo na jambo linaloitwa ugoni (Adultery) ambalo kimsingi ni kosa kisheria.

Ugoni ni ile hali ya kuwepo mahusiano ya kimapenzi ya hiari kati ya mtu aliyefunga ndoa na mtu ambaye si mwenzi wa mtu huyo.

Kwa lugha nyingine huitwa "Uzinzi kwa mwanandoa" huu Ugoni huonwa na sheria kama kosa linalodhuru maadili ya umma na unyanyasaji wa uhusiano wa ndoa.

Sasa basi.....

Ni mazingira gani kisheria utafsirika kama ugoni?

Mazingira ambayo mahakama inaweza kujiridhisha kuwa kweli Kuna ugoni umefanyika ni kupitia katika mazingira mawili ambayo ni kama ifuatavyo,

(A) Kwa ushahidi wa kuwakamata Moja Kwa moja (Right handed).

(B) Kwa ushahidi wa kimazingira pia mahakama inaweza kujiridhisha kuwa kweli Kuna ugoni, ushahidi huo wa kimazingira ni kama..

1- Watu kuwa pamoja mazingira ya nyumba za wageni (guest).
2- Kuwaona watu hao wakiwa katika madanguro.
3- Mwanamke kuzaa na mume mwingine ambaye sio mume wake.
4- Pia kuna mazingira ya njia za mtandao kama meseji katika simu na masuala mengine.
5- Mke au mume kuhama nyumba na kuhamia Kwa mke au mume mwingine tofauti na mume wake wa ndoa anayetambulika.

Baada ya kuthibitishwa hayo mahakama inaweza kuamua amri na nafuu zifuatazo:

1- Kulipa fidia Kwa Mtu aliye kamatwa ugoni (adulterer), Rejea kifungu cha 73 cha Sheria Ya Ndoa Sura 29 ya mwaka 1971 (marejeo ya mwaka 2019).

Kwa mfano:
JUMA ana mke wake wa ndoa, Mke wa Juma anakamatwa ugoni akiwa na JOHN, basi John atapaswa kumlipa Juma.

Hivyo Juma atapaswa kufungua kesi ya madai mahakamani akiomba fidia kutoka kwa John kwa kuwa amefanya mapenzi na mkewa halali wa ndoa wa Juma.

2- Kutolewa kwa taraka (Divorce) ikiwa itabainika kuwa mke amezaa na mume mwingine, katika mazingira hayo basi muathirika anaweza kuomba taraka mahakamani na mke asipate haki ya chumo la pamoja (division of matrimonial properties), Rejea kifungu cha 72, 73, 107, 109, vya Sheria Ya Ndoa Ya Mwaka 1971).

Najua hapo kwenye namba (2) utaniuliza vipi na ikiwa Mwanaume ndie atakamatwa ugoni?

Itaendelea.....

Ndimi Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
 
Ok! mke amegombana na mkewe aka kimbilia kwa Ndugu wa Mmewe je hapo ni kosa??? mke na huyo ndugu wa mumewe wanajuana tangia kitambo!...na wote hawa ni ndugu yaani ndugu wameoa ndugu!! wameoa Mkubwa na huyu kaoa mdogo!
 
Back
Top Bottom